Warumi 3

Uaminifu Wa Mungu

1Basi kuna faida gani kuwa Myahudi? Je, kutahiriwa kuna faida yo yote? Ndio, zipo faida nyingi. Kwanza, Mungu aliwaka bidhi Wayahudi maagizo yake. Na hata kama baadhi yao hawaku amini,je, kutokuamini kwao kutamfanya Mungu aache kuwa mwaminifu? Hata kidogo!Mungu ataendelea kuwa wa kweli hata kama kila mwan adamu atakuwa mwongo. Kama ilivyoandikwa katika Maandiko,“Wewe Mungu, uthibitishwe kuwa wahaki katika maneno yako, na mshindi katika hukumu.”

Lakini iwapo uovu wetu unadhihirisha wazi kwamba Mungu ni mwenye haki, tusemeje basi? Je, tuseme kuwa Mungu hana haki kutuadhibu? Hapa ninasema kibinadamu. La hasha! Mun gu ana haki kabisa kutughadhibikia! Kama sivyo, Mungu angewezaje kuuhukumu ulimwengu? Mtu anaweza kusema,“Kama uongo wangu unasaidia kuonyesha ukweli wa Mungu na hivyo kudhihirisha utukufu wake, kwa nini basi ninahukumiwa kama mwenye dhambi?” Kwa nini tusiseme, kama wengine wanavyotusingizia kuwa tunasema, “Tutende maovu ili wema udhihirike”? Hakika hukumu wanayoipata ni ya haki.

Wote Wametenda Dhambi

Tusemeje basi? Sisi Wayahudi tunayo nafuu yo yote? Hata kidogo! Kama tulivyokwisha kusema, Wayahudi na Wagiriki, wote wanatawaliwa na nguvu ya dhambi. 10 Kama Maandiko yase mavyo:“Hakuna hata mmoja mwenye haki; 11 hakuna hata mmoja mwe nye kuelewa, hakuna hata mmoja amtafutaye Mungu. 1 2Wote wamepotoka na kwa pamoja hawana thamani yo yote; hakuna atendaye mema hata mmoja. 13 Makoo yao ni kama makaburi wazi, wanatumia ndimi zao kudanganya. Kwenye midomo yao mnasumu kama ya nyoka. 14 Vinywa vyao vimejaa laana na ukali. 15 Miguu yao huen da mbio kumwaga damu, 16 njia zote wanazopita huacha uharibifu na huzuni kuu, na 17 wala njia ya amani hawaifahamu. 18 Kumcha Mungu hakupo machonipao.”

Mungu hakupo machonipao.”

19 Basi tunafahamu ya kwamba maagizo yote ya sheria ya Musa yanawahusu wale walio chini ya sheria hiyo. Kusudi la sheria ni kuwafanya watu wote wasiwe na kisingizio na kuuweka ulimwengu wote chini ya hukumu ya Mungu. 20 Kwa hiyo hakuna binadamu hata mmoja atakayehesabiwa kuwa na haki mbele za Mungu kwa kufuata sheria; bali sheria hutufanya tutambue dhambi.

Haki Kwa Njia Ya Imani

21 Lakini sasa, njia ya Mungu ya kuwahesabia watu haki pasipo sheria, njia ambayo sheria na manabii huishuhudia, imekwisha dhihirishwa. 22 Haki hii itokayo kwa Mungu hupatikana kwa kumwaminiYesu Kristo. Mungu huwatendea hivi watu wote wamwa minio Kristo pasipo kubagua, 23 kwa maana wote wametenda dhambi na kupungukiwa na utukufu wa Mungu; 24 wote wanahesabiwa haki bure kwa neema yake kwa ukombozi ulioletwa na Yesu Kristo. 25 Mungu alimtoa awe dhabihu ya upatanisho kwa njia ya imani katika damu yake. Alifanya hivi ili kuonyesha haki yake, kwani kwa uvumilivu wake hakuziadhibu dhambi za zamani. 26 Pia alifanya hivi ili kuonyesha kwa wakati huu kuwa yeye ni wa haki na kwamba yeye ndiye anayewahesabia haki watu wote wamwaminio Yesu.

Umuhimu Wa Kuwa Na Imani

27 Sasa kujivuna kwetu kuko wapi basi? Hakupo. Je kumeondo lewa kwa msingi gani? Kwa msingi wa kutimiza sheria? La. Kumeon dolewa kwa msingi wa imani. 28 Kwa maana tunasisitiza kwamba mwanadamu anahesabiwa haki kwa njia ya imani na wala si kwa kutenda maagizo ya sheria. 29 Je, Mungu ni Mungu wa Wayahudi peke yao? Je, yeye si Mungu wa watu wa mataifa mengine pia? Ndio, yeye ni Mungu wa watu wa mataifa mengine pia. 30 Basi kwa kuwa Mungu ni mmoja, atawahesabia haki wale waliotahiriwa kutokana na imani yao na wale wasiotahiriwa kutokana na imani yao. 31 Je, ina maana kwamba tunaifuta sheria kwa imani hii? La, sivyo. Kiny ume chake: tunaithibitisha sheria.