Nafasi Ya Pekee Ya Waisraeli
1Ninasema kweli katika Kristo na dhamiri yangu inanishuhudia kwa njia ya Roho Mtakatifu kuwa sisemi uongo. 2 Nina huzuni sana na uchungu usiokwisha moyoni mwangu. 3 Kwa maana ningetamani hata mimi nilaaniwe na kutengwa na Kristo kama kufanya hivyo kungeweza kuwasaidia ndugu zangu tulio wa kabila moja. 4 Nazungumza kuhusu Waisraeli ambao Mungu aliwateua kuwa wana wake, wakapewa utukufu wake, maagano yake, sheria yake, ibada ya kweli, na ahadi zake. 5 Wao ni wa uzao wa mababu wa kwanza, na katika taifa lao Kristo alitoka kama mwanadamu; yeye ambaye ni Mungu aliye juu ya vyote, atukuzwaye milele! Amina.
6 Lakini hii haina maana kwamba ahadi ya Mungu kwa wana wa Israeli imeshindwa. Kwa maana si wote ambao ni wa uzao wa Israeli ambao ni wa Israeli. 7 Wala si wazaliwa wote wa kizazi cha Abra hamu ambao ni watoto wake. Ahadi ya Mungu kwa Abrahamu ilikuwa: “Watoto wako watatoka katika uzao wa Isaki.” 8 Kwa maneno men gine, si wale watoto waliozaliwa na Ibrahimu kimwili ambao ni wana wa Mungu; bali ni wale watoto wa ahadi ambao wanahesabiwa kuwa kizazi cha Abrahamu. 9 Kwa maana ahadi yenyewe ilisema, “Nitarudi tena wakati kama huu na Sara atapata mtoto wa kiume.”
10 Na si hivyo tu bali pia wakati Rebeka alipozaa watoto na mume mmoja, Isaki, 11 hata kabla watoto wake mapacha hawajazal iwa wala kutenda jema au baya ili mpango wa Mungu wa kuchagua uendelee, si kwa kutegemea matendo mema bali kwa kufuatana na wito wake - 12 Rebeka aliambiwa, “Mkubwa atamhudumia mdogo.” 13 Kama Maandiko yasemavyo: “Nimempenda Yakobo, bali Esau nimemchukia.”
Mungu Hana Upendeleo
14 Tusemeje basi? Kwamba Mungu ana upendeleo? La, sivyo. 15 Kwa maana Mungu alimwambia Musa, “Nitamrehemu nipendaye kumrehemu; na nitamhurumia nipendaye kumhurumia.” 16 Kwa hiyo haitegemei mapenzi ya mtu au jitihada ya mtu, bali hutegemea huruma ya Mungu. 17 Kwa maana katika Maandiko Farao anaambiwa, “Nilikuinua kwa makusudi ya kudhihirisha nguvu zangu kwako na jina langu lipate kutangazwa duniani pote.” 18 Kwa hiyo basi, Mungu humhurumia mtu ye yote apendaye kumhurumia na huufanya mgumu moyo wa mtu ye yote atakaye.
19 Bila shaka mtaniuliza, “Kama ni hivyo, kwa nini Mungu anatulaumu? Kwa maana ni nani awezaye kushindana na mapenzi yake? 20 Lakini wewe mwanadamu, una haki gani ya kumhoji Mungu? Je, kilichotengenezwa kinaweza kumwuliza aliyekitengeneza, “Kwa nini umenitengeneza hivi?” 21 Je, mfinyanzi hana haki ya kufa nya apendavyo na udongo wake? Je, si anaweza kabisa kutumia sehemu ya udongo huo kutengeneza chombo kimoja kitumikacho kwa kupamba na kutoka katika udongo huo huo akatengeneza kingine kwa matumizi ya kawaida?
22 Tunajuaje kama Mungu, kwa kutaka kuonyesha ghadhabu yake na nguvu yake, amewavumilia kwa uvumilivu mkuu wale waliomkasi risha, ambao wameandaliwa kuangamizwa? 23 Na tunajuaje kama Mungu alifanya hivi ili kuwadhihirishia utajiri wa utukufu wake wale anaowahurumia, ambao aliwaandaa tangu mwanzo kupokea utu kufu? 24 Na sisi ndio hao walioitwa, si kutoka kwa Wayahudi tu bali pia kutoka kwa watu wa mataifa mengine.
Yote Yalitabiriwa Katika Maandiko
25 Hivi ndivyo Mungu asemavyo katika kitabu cha Hosea, “Wale ambao hawakuwa watu wangu, nitawaita ‘watu wangu,’ na wale ambao hawakuwa wapendwa wangu, nitawaita ‘wapendwa wangu’.” 26 Na pale pale walipoambiwa,“Ninyi si ‘watu wangu,’ ndipo watakapoitwa, ‘Wana wa Mungu aliye hai’.” 27 Na Isaya anasema hivi kuhusu Israeli: “Ijapokuwa wana wa Israeli watakuwa wengi kama mchanga wa bahari, ni wachache tu miongoni mwao watakaooko lewa;
28 kwa maana Mungu ataitekeleza hukumu yakejuu ya ulimwengu mara moja na kuikamilisha.” 29 Na tena kama alivyotabiri Isaya,“Kama Bwana wa majeshi asingetuachia uzao, tungalikuwa kama Sodoma, na kufanywa kama Gomora.”
30 Kwa hiyo tusemeje basi? Watu wa mataifa ambao hawakuta futa kupata haki wamepewa haki kwa njia ya imani. 31 Lakini Waisraeli ambao wametafuta kupata haki kwa msingi wa sheria, hawakuipata kwa maana hawakutimiza sheria. 32 Kwa nini? Kwa sababu hawakuitafuta kwa imani bali kwa kutegemea matendo. Wali jikwaa kwenye lile ‘jiwe la kujikwaa.’ 33 Kama ilivyoandikwa kwe nye Maandiko,“Tazama naweka jiwe huko Sayuni ambalo linawafanya watu kujikwaa na mwamba utakaowaangusha, na wale watakaomtegemea hawataaibika kamwe.”