Warumi 8

Maisha Ya Kiroho

1Kwa hiyo basi, sasa hakuna tena hukumu kwa wale walio ndani ya Kristo Yesu. Kwa maana sheria ya Roho wa uzima katika Kristo Yesu imeniweka huru kutokana na sheria ya dhambi na mauti. Mungu amefanya lile ambalo sheria ilishindwa kufanya kwa sababu ya udhaifu wa mwili wetu wa asili. Mungu aliihukumu dhambi kwa kumtuma Mwana wake wa pekee katika hali ya mwili kama sisi, ili awe sadaka kwa ajili ya dhambi. Kwa kufanya hivyo, Mungu ametutimizia matakwa ya haki ya sheria kwa kuwa sasa maisha yetu yanaongozwa na Roho na wala hatuishi tena kwa kufuata mata kwa ya mwili.

Kwa maana wale waishio kwa kuongozwa na asili yao ya dhambi, hukaza mawazo yao kwenye mambo ya mwili; bali wale waishio kwa kuongozwa na Roho hukaza mawazo yao katika mambo ya Roho. Matokeo ya mawazo yaliyotawaliwa na tamaa za mwili ni kifo lakini mawazo yaliyotawaliwa na Roho huleta uzima na amani. Watu wenye mawazo yaliyotawaliwa na mambo ya mwili ni adui wa Mungu. Watu kama hao hawakubali kutii sheria ya Mungu, na kwa kweli hawawezi. Watu wanaotawaliwa na mwili, hawawezi kum pendeza Mungu .

Lakini ninyi hamuishi kwa kufuata matakwa ya mwili, bali mnaongozwa na Roho; ikiwa kweli Roho wa Mungu anaishi ndani yenu. Mtu ye yote ambaye hana Roho wa Kristo, yeye si wa Kristo. 10 Lakini kama Kristo anaishi ndani yenu, ingawa miili yenu imekufa kwa sababu ya dhambi, roho zenu zinaishi kwa sababu mmek wisha kuhesabiwa haki. 11 Na ikiwa Roho wa Mungu ambaye alimfu fua Yesu kutoka kwa wafu anaishi ndani yenu, Mungu aliyemfufua Kristo Yesu kutoka kwa wafu ataipatia uzima miili yenu ambayo hufa, kwa njia ya huyo Roho wake ambaye anaishi ndani yenu. 12 Kwa hiyo ndugu zangu, hatuwajibiki tena kuishi kama miili yetu inavyotaka. 13 Kwa maana mkiishi kama mwili unavyotaka mta kufa,lakini kama mkiangamiza matendo ya mwili kwa nguvu ya Roho, mtaishi.

14 Kwa maana wote wanaoongozwa na Roho wa Mungu ni wana wa Mungu. 15 Hamkupewa Roho anayewafanya kuwa tena watumwa wa hofu. Lakini mmepokea Roho anayewafanya kuwa wana. Na kwa Roho huyo tunaweza kumwita Mungu, “Abba! Baba!” 16 Ni Roho mwenyewe anayeshuhudia pamoja na roho zetu kwamba sisi ni wana wa Mungu. 17 Na ikiwa sisi ni wana, basi tu warithi. Sisi ni warithi wa Mungu tutakaorithi pamoja na Kristo iwapo tutateseka pamoja naye ili pia tutukuzwe pamoja naye.

Utukufu Ujao

18 Nayahesabu mateso tunayopata sasa kuwa si kitu yakilin ganishwa na utukufu utakaodhihirishwa kwetu. 19 Viumbe vyote vinangoja kwa hamu kudhihirishwa kwa wana wa Mungu. 20 Kwa maana viumbe vilifanywa kuwa duni kabisa, si kwa kupenda kwake, bali kwa mapenzi ya Mungu; hata hivyo kulikuwa na matumaini 21 kwamba siku moja viumbe vyote vitawekwa huru kutoka katika utumwa wa kuharibika na vipewe uhuru na utukufu wa watoto wa Mungu.

22 Tunajua kwamba mpaka sasa viumbe vyote vimekuwa vikilia kwa uchungu mkali kama ule wa uzazi. 23 Na si hivyo tu, hata sisi ambao tuna matunda ya kwanza ya Roho tunalia kwa uchungu tukisu biri kwa hamu kufanywa kuwa wana wa Mungu, miili yetu itakapowek wa huru kabisa.

24 Kwa maana tuliokolewa kwa tumaini hili. Lakini kama kinachotumainiwa kikionekana hakiwi tumaini tena. Je, kuna mtu anayetumaini kupata kitu alichonacho? 25 Lakini tunapotumaini kupata kitu ambacho hatunacho, basi tunakingoja kwa subira.

26 Hali kadhalika Roho hutusaidia katika udhaifu wetu. Kwa sababu hatujui kuomba ipasavyo, lakini Roho mwenyewe hutuombea kwa uchungu usioelezeka kwa maneno. 27 Na Mungu ambaye ana chunguza mioyo yetu anafahamu mawazo ya Roho kwa maana Roho huwaombea watakatifu kufuatana na mapenzi ya Mungu. 28 Nasi tunajua ya kuwa katika mambo yote Mungu hutenda kazi pamoja na wote wampendao, wale ambao wameitwa kufuatana na mapenzi yake. Mungu hufanya hivyo kwa faida yao. 29 Wale ambao Mungu alikwisha kuwachagua tangu mwanzo, pia aliwateua wafanane na Mwanae, ili Mwana awe mzaliwa wa kwanza miongoni mwa ndugu wengi. 30 Na wale ambao Mungu aliwateua tangu awali pia ali waita; na wale aliowaita pia aliwahesabia haki; na wale aliowahesabia haki aliwapa utukufu wake.

Upendo Wa Mungu

31 Tuseme nini basi kuhusu haya yote? Ikiwa Mungu yuko upande wetu ni nani atakayetupinga? 32 Ikiwa Mungu hakumwacha Mwanae bali alimtoa kwa ajili yetu sote, hatatupatia pamoja na Mwanae, vitu vyote? 33 Ni nani atawashtaki wale ambao Mungu amewachagua? Ni Mungu mwenyewe ambaye anawahesabia kuwa hawana hatia. 34 Ni nani basi atakayewahukumu? Yesu Kristo mwenyewe ndiye aliyekufa, na zaidi ya hayo, yeye ndiye aliyefufuliwa akawa hai, na ambaye sasa amekaa upande wa kulia wa Mungu, naye anatuombea. 35 Ni nani atakayetutenganisha na upendo wa Kristo? Ni shida? Au taabu? Au mateso? Au njaa? Au umaskini? Au hatari? Au Kifo? Hapana. 36 Kama Maandiko yasemavyo: “Kwa aji li yako tunauawa mchana kutwa, tumehesabiwa kama kondoo wa kuchinjwa.” 37 Lakini katika mambo yote haya sisi ni washi ndi, naam, na zaidi ya washindi, tukiwa ndani yake yeye aliyetu penda. 38 Kwa maana nina hakika kuwa, si kifo wala uzima; si malaika wala mashetani; si mambo ya sasa wala mambo yajayo au mamlaka nyingineyo yote; 39 si mambo yaliyo juu wala yaliyo chi ni sana; wala hakuna kitu kingine cho chote kati ya vitu vyote alivyoumba Mungu kitakachoweza kututenga na upendo wa Mungu ulio ndani ya Kristo Yesu Bwana wetu.