Mfano Wa Karamu Ya Harusi
1Yesu akazungumza nao tena kwa kutumia mifano, akasema, 2“Ufalme wa mbinguni unaweza kufananishwa na mfalme mmoja ali yemwandalia mwanae karamu ya harusi. 3Akawatuma watumishi wake wakawaite wageni walioalikwa lakini wakakataa kuja. 4Akawatuma watumishi wengine akisema, ‘Waambieni waalikwa kwamba karamu iko tayari, nimekwisha chinja fahali wangu na ng’ombe wanono kwa ajili yenu, karibuni karamuni.’ 5Lakini waalikwa wakadharau, mmoja akaenda shambani kwake, mwingine akaenda kwenye miradi yake, 6na wengine wakawakamata wale watumishi wakawatendea mambo ya aibu na kuwaua.
7“Yule mfalme akakasirika, akapeleka jeshi lake likawaanga miza wale wauaji na kuteketeza mji wao. 8Kisha akawaambia watum ishi wake, ‘Karamu ya harusi ni tayari, lakini wale niliowaalika hawakustahili kuja karamuni. 9Kwa hiyo nendeni katika njia panda mkawaalike harusini wote mtakaowakuta.’ 10Wale watumishi wakaenda mabarabarani wakawakusanya wote waliowakuta, wema na wabaya. Ukumbi wa sherehe ya harusi ukajaa wageni.
11“Lakini mfalme alipoingia kutazama wageni, alimwona mle ndani mtu mmoja ambaye hakuwa amevaa vazi la harusi. 12Mfalme akamwuliza, ‘Rafiki, umeingiaje humu bila vazi la harusi?’ Yule mtu hakuwa na la kusema. 13Basi mfalme akawaambia watumishi wake, ‘Mfungeni mikono na miguu mkamtupe nje kwenye giza. Huko kutakuwa na kilio na kusaga meno.’ 14Kwa maana walioitwa ni wengi lakini walioteuliwa ni wachache.”
Kuhusu Kulipa Kodi
15Mafarisayo walifanya mbinu za kumtega Yesu katika mafundi sho yake. 16Wakatuma wanafunzi wao pamoja na Maherode wakam wambie, “Mwalimu, tunajua kwamba wewe ni mtu wa haki na unafundisha njia za Mungu kwa uaminifu bila kumjali mtu, kwa maana cheo si kitu kwako. 17Basi tuambie, wewe unaonaje? Ni halali, au si halali kulipa kodi kwa Kaisari?”
18Yesu alifahamu hila yao kwa hiyo akawaambia, “Ninyi wanafiki, kwa nini mnajaribu kunitega? 19Nionyesheni sarafu mnayolipia kodi.” Wakamletea sarafu. 20Yesu akawauliza, “Picha hii na sahihi hii ni za nani?” 21Wakamjibu, “Ni za Kaisari.” Basi Yesu akawaambia, “Mpeni Kaisari yaliyo ya Kais ari; na ya Mungu mpeni Mungu.”
22Waliposikia haya wakashangaa; wakamwacha, wakaondoka.
Ufufuo Wa Wafu
23Siku hiyo hiyo Masadukayo, wale wanaoamini kwamba wafu hawafufuki, walikuja kwa Yesu wakamwuliza, 24“Mwalimu, Musa alitufundisha kwamba mtu akifariki pasipo kupata watoto, ndugu yake amwoe huyo mjane ili ampatie kaka yake watoto. 25Hapa kwetu walikuwapo ndugu saba. Wa kwanza alioa mke, kisha akafariki na kwa kuwa hakuwa na watoto, yule mjane alichukuliwa na ndugu yake. 26Ikatokea hivyo hivyo kwa yule ndugu wa pili hadi wote saba wakamwoa huyo mjane bila kupata watoto. 27Baadaye, yule mjane naye akafariki. 28Sasa tuambie, siku ile ya ufufuo, ata hesabiwa kuwa ni mke wa nani? Maana aliolewa na wote saba!”
29Yesu akawajibu, “Mnakosea kwa sababu hamjui Maandiko wala uwezo wa Mungu. 30Wakati wa ufufuo, watu hawataoa wala kuolewa; kwa maana watakuwa kama malaika wa mbinguni. 31Na kuhusu ufufuo wa wafu, hamjasoma Mungu alivyowaambia kwamba, 32‘Mimi ni Mungu wa Ibrahimu, Mungu wa Isaka na Mungu wa Yakobo’? Yeye si Mungu wa wafu bali ni Mungu wa walio hai.”
33Ule umati wa watu waliposikia hayo, walishangazwa sana na mafund isho yake.
Amri Kuu Kuliko Zote
34Mafarisayo waliposikia kwamba Yesu alikuwa amewanyamazi sha Masadukayo, walikutana wakamjia pamoja. 35Mmoja wao, mtaalamu wa sheria akajaribu kumtega kwa kumwuliza, 36“Mwali mu, ni amri ipi iliyo kuu kuliko zote?”
37Yesu akamjibu, “Mpende Bwana Mungu wako kwa moyo wako wote, na kwa roho yako yote na kwa akili zako zote.’ 38Hii ndio amri kuu, tena ni ya kwanza. 39Na ya pili inafanana nayo, nayo ni hii: ‘Mpende jirani yako kama nafsi yako.’ 40Amri hizi mbili ndio msingi wa sheria zote na Maandiko ya manabii.”
Kristo Ni Mwana Na Bwana Wa Daudi
41Mafarisayo walipokuwa pamoja Yesu aliwauliza, 42“Mnaonaje kuhusu Kristo? Yeye ni mwana wa nani?” Wakamjibu, “Yeye ni mwana wa Daudi.”
43Akawaambia, “Inakuwaje basi kwamba Daudi anapozungumza kwa Roho anamwita Kristo ‘Bwana,’ kwa kusema, 44‘Bwana alimwam bia Bwana wangu: keti upande wangu wa kulia mpaka nitakapowaweka adui zako chini ya miguu yako.’ 45Kama Daudi anamwita ‘Bwana 46Hakuna aliyeweza kumjibu Yesu hata neno moja. Na tangu siku hiyo hakuna aliyethubutu tena kum wuliza maswali.