Kutokuamini Kwa Waisraeli
1Ndugu zangu, shauku ya moyo wangu na maombi yangu kwa Mungu ni kwamba Waisraeli waokolewe. 2Ninashuhudia wazi kwamba wao wanajuhudi kubwa ya kumtumikia Mungu, lakini juhudi yao haitokani na kuelewa. 3Wameshindwa kuelewa haki itokayo kwa Mu ngu, na badala yake wakajaribu kujiwekea ya kwao; kwa hiyo hawa kutii haki ya Mungu. 4Kwa maana Kristo amekamilisha sheria ili kila mtu mwenye imani ahesabiwe haki.
Wokovu Ni Kwa Wote
5Musa anaandika kwamba mtu anayejaribu kutenda haki kwa msingi wa sheria ataishi kwa sheria. 6Lakini haki itokanayo na imani husema hivi, “Usiseme nafsini mwako, ‘Ni nani atapaa mbi nguni?”’ yaani kumleta Kristo duniani, 7au “‘Ni nani atashuka kuzimuni?”’yaani kumleta Kristo kutoka kwa wafu. 8Bali inasema hivi, “Neno la Mungu liko karibu nawe; liko mdomoni mwako na moyoni mwako,” yaani, neno la imani tunayohubiri. 9Kama ukikiri kwa kinywa chako kuwa Yesu ni Bwana na ukiamini moyoni mwako kuwa Mungu alimfufua kutoka kwa wafu, utaokoka. 10Kwa maana mtu ana poamini moyoni mwake huhesabiwa haki, na anapokiri kwa kinywa chake, huokolewa. 11Kama yasemavyo Maandiko, “Hakuna amwami niye ambaye ataaibika.” 12Kwa maana hakuna tofauti kati ya wote naye huwabariki wote wamwitao. 13Kwa maana, “Kila mtu atakayeliita Jina la Bwana, ataokoka.”
14Lakini watu watamwitaje yeye ambaye hawajamwamini? Na watamwaminije yeye ambaye hawajawahi kumsikia? Na watamsikiaje kama mtu hakuwahubiria? 15Na watu watahubirije kama hawaku tumwa? Kama ilivyoandikwa, Ni mizuri mno miguu ya hao wanaohubiri Habari Njema!”
16Lakini si wote walioipokea Habari Njema. Kwa maana Isaya alisema:“Bwana, ni nani aliyeamini ujumbe wetu?” 17Basi, chanzo cha imani ni kusikia, na kusikia huja kwa kuhubiri neno la Kristo. 18Lakini nauliza, hivi wao hawajasikia? Hakika wame sikia; kwa maana Maandiko yanasema: “Sauti yao imeenea duniani kote, na maneno yao yamefika miisho ya ulimwengu.” 19Nauliza tena, je, Waisraeli hawakuelewa? Kwanza Musa anasema, “Nitawa fanya muone wivu kwa ajili ya wale ambao hawajawa taifa bado; nitawafanya mkasirike kwa ajili ya taifa la watu wasio elewa.” 20Na Isaya anasema kwa ujasiri, “Wale ambao wali kuwa hawanitafuti, wamenipata. Nimejidhihirisha kwa wale ambao walikuwa hawaniulizii.” 21Lakini kuhusu wana wa Israeli anasema: “Mchana kutwa nimewanyooshea mikono watu wakaidi na wasiotii.”