Watu 144,000 Wawekewa Muhuri
1Baada ya haya nikaona malaika wanne wamesimama katika pembe zote nne za dunia wakizuia pepo nne za dunia, ili upepo usivume nchi kavu wala baharini wala kwenye mti wo wote. 2 Kisha nikaona malaika mwingine akija kutoka mashariki akiwa na muhuri wa Mungu aliye hai. Akawaita kwa sauti kuu wale malaika waliokuwa wamepewa mamlaka kuidhuru nchi na bahari, akisema, 3 “Msiidhuru nchi wala bahari, wala miti, mpaka tutakapoweka mihuri kwenye vipaji vya nyuso za watumishi wa Mungu wetu.”
4 Ndipo nikasikia idadi ya wale waliowekewa mihuri, watu 144,000 kutoka katika kila kabila la Waisraeli. 5 Kabila la Yuda, 12,000, kabila la Rubeni 12,000, kabila la Gadi 12,000, 6 kabila la Asheri 12,000, kabila la Naftali 12,000, kabila la Manase 12,000, 7 kabila la Simioni 12,000, kabila la Lawi 12,000, kabila la Isakari 12,000, 8 kabila la Zabuloni 12,000, kabila la Yusufu 12,000, kabila la Benyamini 12,000.
Umati Wa Watu Waliokombolewa
9 Kisha nikatazama, nikaona umati mkubwa wa watu ambao hakuna mtu awezaye kuwahesabu: watu wa kila taifa, kila kabila, kila jamaa na kila lugha, wamesimama mbele ya kile kiti cha enzi na mbele ya Mwana-Kondoo. Walikuwa wamevaa mavazi meupe na wameshika matawi ya mitende mikononi mwao. 10 Nao walikuwa wakisema kwa sauti kuu, “Ukombozi hutoka kwa Mungu wetu aketiye katika kiti cha enzi, na kwa Mwana-Kondoo!” 11 Na wale malaika wote wakasi mama kuzunguka kile kiti cha enzi na wale wazee na wale viumbe hai wanne, wakaanguka chini mbele ya kile kiti cha enzi wakamwab udu Mungu, 12 wakisema, “ Amina! Sifa na utukufu na hekima na shukrani na heshima na nguvu na uweza ni za Mungu wetu milele na milele! Amina”. 13 Kisha mmoja wa wale wazee akaniuliza, “Hawa watu waliovaa mavazi meupe, ni kina nani? Nao wametoka wapi?” 14 Nikamjibu, “Bwana, wewe ndiye unayefahamu.” Naye akasema, “Hawa ni wale waliotoka katika ile dhiki kuu; wameosha mavazi yao katika damu ya Mwana-Kondoo yakawa meupe kabisa. 15 Kwa hiyo, wanakaa mbele ya kiti cha enzi cha Mungu na kumtumikia katika Hekalu lake usiku na mchana; naye aketiye katika kile kiti cha enzi atakuwa pamoja nao na kuwalinda. 16 Kamwe hawataona njaa wala kiu tena; jua wala joto kali halitawachoma tena. Kwa maana Mwana-Kondoo aliye katikati ya kiti cha enzi atakuwa mchun gaji wao. Naye atawaongoza kwenye chemchemi za maji ya uzima; na