Mabakuli Saba Ya Ghadhabu Ya Mungu
1Kisha nikasikia sauti kuu kutoka Hekaluni ikiwaambia wale malaika saba, “Nendeni mkamwage duniani yale mabakuli saba ya ghadhabu ya Mungu.”
2 Malaika wa kwanza akaenda akalimimina bakuli lake ardhini na madonda mabaya yenye maumivu makali yakawapata wote waliokuwa na alama ya yule mnyama na walioabudu sanamu yake.
3 Malaika wa pili akamimina bakuli lake baharini , ikawa kama damu ya mtu aliyekufa na kila kiumbe hai kilichokuwa ndani ya bahari kikafa.
4 Malaika wa tatu akamimina bakuli lake katika mito na chemchemi za maji, nazo zikageuka kuwa damu. 5 Nami nikamsikia malaika wa maji akisema, “Umefanya haki katika hukumu hizi uli zotoa, wewe uliyeko na uliyekuwako, Mtakatifu. 6 Maana walimwaga damu ya watakatifu na manabii, na wewe umewapa damu wanywe, kama walivyostahili.” 7 Nikasikia madhabahu ikiitikia, “Naam, Bwana Mungu Mwenyezi, hukumu zako ni za kweli na haki.!”
Mungu Mwenyezi, hukumu zako ni za kweli na haki.!”
8 Malaika wa nne akamimina bakuli lake kwenye jua nalo lika pewa nguvu za kuwachoma watu kwa moto wake mkali. 9 Watu wakaun guzwa na moto huo nao wakalaani jina la Mungu aliyekuwa na uwezo juu ya maafa haya, wala hawakutubu na kumtukuza.
10 Malaika wa tano akamimina bakuli lake kwenye kiti cha enzi cha yule mnyama, na ufalme wake ukawa gizani. Watu wakauma ndimi zao kwa uchungu 11 wakamlaani Mungu wa mbinguni kwa mau mivu yao na madonda yao, wala hawakutubu kwa ajili ya matendo yao maovu.
12 Malaika wa sita akamimina bakuli lake kwenye mto mkubwa wa Efrati, maji yake yakakauka ili kuwatayarishia njia wafalme kutoka mashariki. 13 Nikaona roho wachafu waliofanana na chura wakitoka katika kinywa cha lile joka na katika kinywa cha yule mnyama, na katika kinywa cha yule nabii wa uongo. 14 Hizo ni roho za pepo zitendazo miujiza. Nazo huwaendea wafalme wa ulim wengu wote na kuwakusanya tayari kwa vita, siku ile kuu ya Mungu Mwenyezi. 15 “Sikiliza! Ninakuja kama mwizi! Amebarikiwa aliye macho, akiziweka tayari nguo zake ili asiende bila nguo na watu wakam wona uchi!” 16 Kisha wakawakusanya wafalme pamoja mahali ambapo huitwa “Armageddoni” kwa Kiebrania.
17 Malaika wa saba akamimina bakuli lake angani na sauti kuu ikatoka Hekaluni katika kile kiti cha enzi ikisema, “Imekwisha timia!” 18 Kukawa na miali ya umeme, sauti, ngurumo za radi na tetemeko kuu la ardhi. Hapajawahi kuwa na tetemeko la ardhi kama hilo tangu mwanadamu kuwapo, kwani lilikuwa tetemeko kubwa ajabu.
19 Ule mji mkuu uligawanywa katika sehemu tatu na miji yote ya mataifa ikaanguka. Mungu akakumbuka Babiloni kuu akainywesha kikombe cha divai ya hasira na ghadhabu yake. 20 Kila kisiwa kikatoweka wala milima haikuonekana. 21 Mvua kubwa ya mawe, mawe mazito karibu kilo hamsini, ikanyesha kutoka mbinguni ikawaangu kia wanadamu. Wanadamu wakamlaani Mungu kwa ajili ya maafa ya mvua ya mawe. Kwa maana lilikuwa ni pigo kuu la kutisha.