Mto Wa Maji Ya Uzima
1Kisha yule malaika akanionyesha mto wa maji ya uzima ung’aao kama kioo na kutiririka kutoka kwenye kiti cha enzi cha Mungu na cha Mwana-Kondoo, 2 kupitia katikati ya barabara kuu ya mji huo. Katika pande zote za mto huo kulikuwa na mti wa uzima utoao matunda ya aina kumi na mbili, na kuzaa matunda yake kila mwezi. Majani yake ni ya kuwaponya watu wa mataifa. 3 Katika mji huo hakutakuwa na kitu cho chote kilicholaaniwa, bali kiti cha enzi cha Mungu na cha Mwana-Kondoo kitakuwamo humo na watumishi wake watamwabudu. 4 Watamwona uso wake na jina lake litakuwa kwe nye vipaji vya nyuso zao. 5 Usiku hautakuwapo tena; wala hawata hitaji mwanga wa taa au wa jua, maana Bwana Mungu atakuwa nuru yao, watatawala milele na milele.
Bwana Yesu Anakuja
6 Kisha yule malaika akaniambia, “Maneno haya ni ya kuami nika na ya kweli. Bwana, Mungu wa roho za manabii, amemtuma mal aika wake kuwaonyesha watumishi wake yale ambayo hayana budi kutokea karibuni. 7 Tazama, ninakuja upesi! Amebarikiwa anayesh ika maneno ya unabii yaliyomo katika kitabu hiki.”
8 Mimi Yohana, ndiye niliyesikia na kuona mambo haya. Na nil ipokwisha kuyasikia na kuyaona, nilianguka kifudifudi penye miguu ya yule malaika aliyenionyesha mambo hayo, nimwabudu. 9 Lakini yeye akaniambia, “Usifanye hivyo! Mimi pia ni mtumishi pamoja na wewe na ndugu zako manabii na wote wanaoshika maneno ya kitabu hiki. Mwabudu Mungu!”
10 Kisha akaniambia, “Usiyawekee muhuri maneno ya unabii yaliyomo katika kitabu hiki maana wakati umekaribia. 11 Mwache atendaye uovu aendelee kutenda uovu, na aliye mchafu aendelee kuwa mchafu; na atendaye mema aendelee kutenda mema na aliye mta katifu aendelee kuwa mtakatifu.”
12 “Tazama, Ninakuja upesi! Nakuja na tuzo yangu, nimpe tuzo kila mtu kulingana na matendo yake. 13 Mimi ni Alfa na Omega, wa kwanza na wa wisho, Mwanzo na Mwisho.” 14 Wamebari kiwa wanaoosha mavazi yao ili wapate haki ya kushiriki mti wa uzima na wapate kuingia katika ule mji kupitia kwenye milango yake. 15 Huko nje wako mbwa, na wachawi, na wazinzi, na wauaji, na waabuduo sanamu, na kila mtu apendaye udanganyifu na kuutenda. 16 Mimi Yesu nimemtuma malaika wangu kuwashuhudia mambo haya kwa ajili ya makanisa. Mimi ni Shina na Mzao wa ukoo wa Daudi. Mimi ni Nyota ya asubuhi ing’aayo.”
17 Roho na bibi harusi wanasema, “Njoo!” Na kila mtu asi kiaye na aseme, “Njoo!” Na mtu ye yote mwenye kiu na aje, na kila anayetaka na apokee zawadi ya maji ya uzima bure. .
18 Namwonya kila mtu asikiaye maneno ya unabii yaliyomo katika kitabu hiki: mtu ye yote akiyaongezea cho chote, Mungu atamwongezea maafa yaliyoandikwa katika kitabu hiki. 19 Na kama mtu ye yote akipunguza cho chote katika maneno ya unabii yaliyomo katika kitabu hiki, Mungu atamnyang’anya sehemu yake katika mti wa uzima na katika mji mtakatifu, ambayo yameelezwa katika kitabu hiki.
20 Yeye anayeshuhudia mambo haya anasema, “Hakika ninakuja upesi!” Amina. Njoo, Bwana Yesu!