Utawala Wa Miaka Elfu Moja
1Kisha nikaona malaika akija kutoka mbinguni akiwa ameshika ufunguo wa lile shimo la kuzimu, na mnyororo mkubwa mkononi. 2 Akalishika lile joka, yule nyoka wa kale ambaye ni Ibilisi au Shetani, akamfunga kwa muda wa miaka elfu moja. 3 Akamtupa kuzi muni; akamfungia huko na kumzibia kabisa, asipate nafasi ya kudanganya mataifa tena mpaka hiyo miaka elfu moja iishe. Baada ya hapo ataachiliwa kwa muda mfupi.
4 Kisha nikaona viti vya enzi. Na kwenye viti hivyo vya enzi waliketi wale waliopewa mamlaka ya kuhukumu. Pia nikaona roho za wale watu waliokatwa vichwa kwa ajili ya kumshuhudia Yesu na kwa ajili ya neno la Mungu. Wao hawakuwa wamemwabudu yule mnyama wala sanamu yake na hawakuwa wamepokea alama ya yule mnyama kwenye vipaji vya nyuso zao wala mikononi mwao. Walifufuka kutoka kwa wafu wakatawala pamoja na Kristo kwa muda wa miaka elfu moja. 5 Wafu waliosalia hawakufufuka mpaka miaka hiyo elfu moja ilipok wisha. Huu ndio ufufuo wa kwanza. 6 Wamebarikiwa na ni watakatifu wale watakaoshiriki huo ufufuo wa kwanza. Mauti ya pili haina nguvu kwa hawa bali watakuwa makuhani wa Mungu na wa Kristo, nao watatawala naye kwa muda wa miaka elfu moja.
Kushindwa Kwa Shetani
7 Miaka hiyo elfu moja itakapokwisha, shetani atafunguliwa kutoka kifungoni mwake, 8 naye atakuja kuyadanganya mataifa yali yopo katika pembe nne za dunia, yaani, Gog na Magog na kuwakusa nya tayari kwa vita. Idadi yao ni kama mchanga wa bahari. 9 Nao walitembea juu ya eneo lote la dunia, wakaizunguka kambi ya wata katifu na ule mji mwema, lakini moto ulishuka kutoka mbinguni, ukawateketeza. 10 Na yule Ibilisi aliyewadanganya alitupwa katika ziwa la moto na kiberiti walipokuwa yule mnyama na yule nabii wa uwongo. Nao watateseka huko usiku na mchana, milele na milele.
11 Kisha nikaona kiti kikubwa cha enzi cheupe, pamoja na huyo aliyeketi juu yake. Dunia na anga zilikimbia kutoka machoni pake zikatoweka wala hazikuonekana tena. 12 Nikaona wafu, wakubwa kwa wadogo, wamesimama mbele ya kiti cha enzi, na vitabu vikafunguliwa. Pia kitabu kingine ambacho ni kitabu cha uzima kikafunguliwa. Na hao wafu wakahukumiwa kutokana na yale yaliy oandikwa ndani ya vitabu hivyo, kuhusu matendo yao. 13 Bahari zikawatoa wafu waliokuwamo ndani yake, na kifo na kuzimu nazo zikawatoa wafu waliokuwamo ndani yake, na wote wakahukumiwa kwa matendo yao. 14 Kisha mauti na kuzimu zikatupwa katika ziwa la moto. Hiki ndicho kifo cha pili, yaani ziwa la moto. 15 Na kama jina la mtu halikukutwa katika kitabu cha uzima, alitupwa katika lile ziwa la moto.