Mwana- Kondoo Avunja Mihuri Saba
1Kisha nikamwona Mwana -Kondoo akifungua mhuri wa kwanza kati ya ile mihuri saba. Nikasikia mmoja wa wale viumbe wanne akisema kwa sauti kama ya ngurumo: “Njoo!” 2 Nikaangalia, na hapo mbele yangu nikaona farasi mweupe na aliyempanda alikuwa na upinde, na alipewa taji akatoka kama mshindi akaendelee kushinda.
3 Mwana-Kondoo alipofungua muhuri wa pili, nikamsikia yule kiumbe hai wa pili akisema, “Njoo!” 4 Akatoka farasi mwingine mwekundu sana na aliyempanda alipewa uwezo wa kuondoa amani duniani na kuwafanya watu wauane. Yeye alipewa upanga mkubwa.
5 Mwana-Kondoo alipofungua muhuri wa tatu, nilimsikia yule kiumbe hai wa tatu akisema, “Njoo!” Nikaangalia na mbele yangu nikaona farasi mweusi, na aliyempanda alikuwa na mizani mkononi mwake. 6 Nikasikia kitu kama sauti kati ya hao viumbe wanne hai, ikisema, “Kibaba kimoja cha ngano kwa mshahara wa siku moja! na vibaba vitatu vya shayiri kwa mshahara wa siku moja! Lakini usi haribu mafuta wala divai!”
7 Mwana-Kondoo alipofungua muhuri wa nne, nilisikia sauti ya yule kiumbe hai wa nne ikisema, “Njoo!” 8 Nikaangalia na mbele yangu nikamwona farasi mwenye rangi ya kijivu. Aliyempanda huyo farasi aliitwa mauti, naye alikuwa akifuatana na kuzimu. Nao wal ipewa mamlaka juu ya robo ya dunia, kuua kwa upanga, njaa, tauni na kwa wanyama wakali wa dunia.
9 Mwana-Kondoo alipofungua muhuri wa tano, niliona chini ya madhabahu, roho za watu waliouawa kwa ajili ya neno la Mungu na kwa ushuhuda wao. 10 Wakalia kwa sauti kuu wakisema, “Bwana Mwenyezi, uliye mtakatifu na mwaminifu, utakawia mpaka lini kuwa hukumu na kulipiza kisasi juu ya watu wote waishio duniani kwa ajili ya damu yetu?” 11 Kisha kila mmoja wao akapewa kanzu nyeupe. Wakaambiwa wasubiri kidogo zaidi mpaka idadi ya ndugu zao na watumishi wenzao wanaopaswa kuuawa kama wao walivyouawa, ita kapotimia.
12 Nilitazama Mwana-Kondoo alipokuwa akifungua muhuri wa sita. Pakatokea tetemeko kuu la nchi na jua likawa jeusi kama gunia lililotengenezwa kwa manyoya ya mbuzi. Mwezi wote ukawa mwekundu kama damu. 13 Nyota zikaanguka ardhini kama vile mat unda ya mtini yasiyokomaa yaangukavyo wakati mti wake unapoti kiswa na upepo mkali. 14 Anga ikatoweka kama vile karatasi inav yosokotwa; na kila mlima na kila kisiwa vikaondolewa mahali pake.
15 Ndipo wafalme wa duniani, wakuu wote, majemadari, mata jiri , wenye nguvu; na kila mtu, mtumwa na aliye huru, wakajifi cha mapangoni na kwenye miamba ya milima. 16 Wakaisihi milima na miamba wakisema, “Tuangukieni, mkatufiche tusionwe na uso wake yeye aketiye kwenye kiti cha enzi na mtuepushe na ghadhabu ya Mwana-Kondoo. 17 Kwa maana siku ile kuu ya ghadhabu yao imekuja, na ni nani awezaye kusalimika?”