Waebrania 9

Agano La Kwanza Na Agano Jipya

1Basi hata lile agano la kwanza lilikuwa na kanuni zake za ibada pamoja na mahali pa kuabudia hapa duniani. Hema la kuabu dia liliandaliwa likiwa na chumba cha kwanza ambamo mlikuwa na chombo cha kuwekea taa, na meza na mikate iliyowekwa wakfu. Chumba hiki kiliitwa Patakatifu. Nyuma ya pazia la pili, pali kuwa na chumba kiitwacho Patakatifu pa Patakatifu. Chumba hiki kilikuwa na madhabahu ya dhahabu ya kufukizia uvumba na sanduku la agano ambalo lilifunikwa kwa dhahabu pande zote. Sanduku hili lilikuwa na chombo cha dhahabu chenye ile mana na ile fimbo ya Aroni iliyochipuka, na yale mawe ya agano. Juu ya sanduku kulikuwa na makerubi wa utukufu ambao kivuli chao kilifunika kiti cha rehema. Lakini mambo haya sasa hatuwezi kuyaeleza kwa undani.

Vitu vyote vilipokwisha kupangwa namna hii, makuhani wal iingia mara kwa mara katika kile chumba cha kwanza kutoa huduma yao ya ibada. Lakini ni kuhani mkuu peke yake ambaye aliruhu siwa kuingia katika chumba cha ndani mara moja tu kwa mwaka. Tena ilibidi aingie huko na damu ambayo aliitoa kwa ajili yake mwe nyewe na kwa ajili ya dhambi za watu walizotenda pasipo kujua. Kwa njia hii, Roho Mtakatifu alikuwa akionyesha kwamba maadamu hema ya kwanza ilikuwa bado imesimama, njia ya kuingia katika Patakatifu pa Patakatifu ilikuwa bado haijafunguliwa. Hii ili kuwa ni kielelezo kwa wakati wa sasa, kuonyesha kwamba sadaka na dhabihu zilizotolewa zilikuwa haziwezi kutakasa dhamiri ya mtu anayeabudu. 10 Hizi zilikuwa ni sheria zinazohusu chakula na vinywaji na taratibu mbalimbali za utakaso wa nje, kanuni ambazo zingetumika mpaka wakati wa matayarisho ya utaratibu mpya.

Damu Ya Kristo Husafisha Dhamiri

11 Kristo alipokuja kama kuhani mkuu wa mambo mema ambayo tayari yamekwisha wasili, alipitia kwenye hema ya kuabudia ambayo ni kuu zaidi na bora zaidi na ambayo haikujengwa na binadamu, yaani ambayo si sehemu ya ulimwengu huu ulioumbwa. 12 Yeye aliingia patakatifu pa patakatifu mara moja tu kwa wakati wote, akichukua, si damu ya mbuzi na ndama, bali damu yake mwenyewe, na hivyo kutupatia ukombozi wa milele.

13 Kwa maana ikiwa damu ya mbuzi na mafahali na majivu ya ndama hunyunyizwa juu ya watu wachafu kidini ikawatakasa kwa kuwaondolea uchafu wao wa nje, 14 damu ya Kristo ambaye kwa njia ya Roho wa milele alijitoa mwenyewe kwa Mungu kama sadaka isiyokuwa na doa, itazisafisha dhamiri zetu zaidi sana kutokana na matendo yaletayo kifo, na kutuwezesha kumtumikia Mungu aliye hai.

15 Kwa sababu hii Kristo ni mjumbe wa agano jipya ili wale walioitwa wapokee urithi wa milele ulioahidiwa na Mungu; kwa kuwa alikufa awe fidia itakayowaweka huru na dhambi walizotenda chini ya agano la kwanza.

16 Ili hati ya urithi itambuliwe ni lazima pawepo na uthi bitisho kwamba huyo aliyeiandika amekwisha kufa. 17 Kwa maana hati ya urithi huwa na uzito tu wakati mtu amekwisha kufa; haiwezi kutumika wakati yule aliyeiandika angali hai. 18 Hii ndio maana hata lile agano la kwanza halikuweza kutekelezwa pasipo damu kumwagika. 19 Wakati Musa alipowatangazia watu amri zote za sheria, alichukua damu ya ndama na ya mbuzi, pamoja na maji na sufu nyekundu na hisopo akanyunyizia kitabu cha sheria na watu wote, 20 akasema, “Hii ndio damu ya agano ambalo Mungu amewaamuru kulitii.” 21 Vivyo hivyo akanyunyizia damu hiyo kwe nye lile hema na vifaa vyote vilivyotumika kwa ibada. 22 Hakika katika sheria, karibu kila kitu hutakaswa kwa damu; na pasipo kumwaga damu, hakuna msamaha wa dhambi.

23 Kwa hiyo ilikuwa muhimu vitu hivi ambavyo ni mfano wa vile vya mbinguni vitakaswe kwa njia hizi, lakini vitu halisi vya mbinguni vilihitaji dhabihu bora kuliko hizi. 24 Kwa maana Kristo hakuingia kwenye hema ya kuabudia iliyotengenezwa na bina damu kama mfano wa hema halisi. Yeye aliingia mbinguni penyewe, ambapo sasa anatuwakilisha mbele za Mungu. 25 Wala hakuingia mbinguni kujitoa mwenyewe mara kwa mara, kama kuhani mkuu ain giavyo Patakatifu pa Patakatifu kila mwaka na damu ambayo si yake. 26 Ingekuwa hivyo, ingalimpasa Kristo kuteswa mara nyingi tangu kuumbwa kwa ulimwengu. Lakini ilivyo ni kwamba ametokea mara moja tu kwa wakati wote, katika siku hizi za mwisho, ili atokomeze dhambi kwa kujitoa mwenyewe kuwa dhabihu. 27 Na kama ambavyo mwanadamu ameandikiwa kufa mara moja tu, na baada ya hapo kukabili hukumu; 28 hali kadhalika Kristo alitolewa kama dhabihu mara moja tu ili azichukue dhambi za watu wengi; naye atakuja mara ya pili, si kuchukua dhambi, bali kuwaletea wokovu wale wanaomngojea kwa hamu.