Waebrania 7

Kuhusu Melkizedeki, Kuhani Mkuu

1Huyu Melkizedeki alikuwa ni mfalme wa Salemu na kuhani wa Mungu aliye juu. Abrahamu alipokuwa akirudi kutoka vitani ambako aliua wafalme wengi, Melkizedeki alikutana naye, akambariki. Abrahamu akampatia Melkizedeki sehemu ya kumi ya vitu vyote. Kwanza, jina hilo Melkizedeki maana yake ni “Mfalme wa haki” na pia yeye ni “Mfalme wa Salemu,” maana yake, “Mfalme wa amani.”

Yeye hana baba wala mama wala ukoo; hana mwanzo wala hana mwisho, bali kama alivyo Mwana wa Mungu, yeye adumu kuwa kuhani milele.

Angalieni jinsi alivyo mkuu! Hata Abrahamu, baba yetu mkuu, alimpa sehemu ya kumi ya nyara zake. Hata wana wa Lawi ambao ni makuhani, wameamriwa na sheria ya Mose kuwatoza Waisraeli ndugu zao, ambao ni wazao wa Abrahamu, sehemu ya kumi ya mapato yao. Ingawa huyu Melkizedeki si wa ukoo wa Lawi, alipokea sehemu ya kumi kutoka kwa Abrahamu , na akambariki huyu ambaye alikwisha pokea ahadi za Mungu. Wala hakuna ubishi kuwa mtu mdogo hubarikiwa na mtu aliye mkuu kuliko yeye. Kwa upande wa makuhani wa ukoo wa Lawi, sehemu ya kumi inapokelewa na binadamu ambao hufa; lakini kwa upande huu wa Melkizedeki, sehemu ya kumi inapokelewa na mtu ambaye tunahakikishiwa kuwa anaishi. Mtu anaweza kusema kwamba Lawi, ambaye hupokea sehemu ya kumi, alitoa sehemu ya kumi kupitia kwa Abrahamu, 10 kwa maana Melkizedeki alipokutana na Abrahamu, Lawi alikuwa bado hajazaliwa. Mbegu yake ilikuwa bado iko mwilini mwa Abrahamu babu yake.

Yesu Na Melkizedeki

11 Kama ukamilifu ungaliweza kupatikana kwa njia ya ukuhani wa Walawi, kwa maana watu walipewa sheria kupitia kwao, ilikuwapo haja gani tena ya kuwepo kuhani mwingine, yaani kuhani kama Mel kizedeki, ambaye si kama Aroni? 12 Kwa maana yanapotokea maba diliko kwenye ukuhani, ni lazima pawepo na mabadiliko katika she ria. 13 Maana Bwana wetu ambaye ndiye anayesemwa katika mambo haya, alikuwa ni wa kabila lingine, na hakuna mtu katika kabila lake aliyewahi kuhudumu katika madhabahu. 14 Inafahamika wazi kuwa Bwana wetu alitoka katika kabila la Yuda, na Mose hakuwahi kusema lo lote juu ya makuhani kutoka katika kabila hilo. 15 Na hili tunalosema linakuwa wazi zaidi anapotokea kuhani mwingine kama Melkizedeki; 16 ambaye ukuhani wake hautokani na kanuni za ukoo wake, bali hutokana na uwezo wa maisha yasiyoharibika. 17 Kwa maana ameshuhudiwa hivi: “Wewe ni kuhani milele, kama wa Melkizedeki.”

Melkizedeki.”

18 Sheria ya mwanzo imewekwa kando kwa kuwa ilikuwa dhaifu na tena haikufaa. 19 Kwa maana sheria haikufanya kitu cho chote kuwa kikamilifu, na sasa tumeletewa tumaini bora zaidi ambalo linatuwezesha kumkaribia Mungu.

20 Na tumaini hilo halikutolewa pasipo kiapo! Wale waliofa nywa makuhani huko nyuma hapakuwepo kiapo. 21 Bali Yesu alipofa nywa kuhani aliwekewa kiapo wakati Mungu alipomwambia: “Bwana ameapa wala hatabadili nia yake, ‘Wewe ni kuhani milele.”’

22 Kwa ajili ya kiapo hiki, Yesu amekuwa mdhamini wa agano lililo bora zaidi.

23 Makuhani wa zamani walikuwa wengi kwa sababu kifo kiliwa zuia kuendelea daima na huduma yao. 24 Lakini yeye anaendelea na ukuhani wake daima kwa maana anaishi milele. 25 Kwa hiyo anaweza kwa wakati wote kuwaokoa wale wanaomkaribia Mungu kupitia kwake, kwa sababu yeye anaishi daima ili kuwaombea.

26 Huyu ndiye kuhani mkuu tunayemhitaji: yeye ni mtakatifu, asiye na lawama, asiye na dosari, aliyetenganishwa na wenye dhambi na aliyeinuliwa juu ya mbingu. 27 Yeye hahitaji kutoa dhabihu kila siku kwa ajili ya dhambi zake kwanza kisha dhambi za watu, kama wale makuhani wakuu wengine. Yeye alitoa dhabihu mara moja kwa wakati wote, alipojitoa mwenyewe. 28 Kwa maana sheria ya Mose huchagua watu wenye udhaifu kuwa makuhani wakuu. Lakini neno la Mungu la kile kiapo ambalo lilikuja baada ya sheria, lil imteua Mwana, ambaye amefanywa kuwa mkamilifu milele.