Kuzingatia Mafundisho
1Kwa hiyo, hatuna budi kuzingatia kwa makini mambo tuliyof undishwa tusije tukatanga-tanga mbali na yale tuliyosikia. 2 Kwa maana kama ujumbe ulioletwa na malaika ulithibitika kuwa kweli, na kila aliyeasi na kutokutii akaadhibiwa ilivyostahili, 3 sisi je? Tutaepukaje kama tusipojali wokovu mkuu namna hii? Wokovu huu kwanza ulitangazwa na Bwana, na ulithibitishwa kwetu na wale wal iomsikia. 4 Mungu pia aliushuhudia kwa ishara na miujiza na maaj abu mbalimbali, pamoja na karama za Roho Mtakatifu alizogawa kufuatana na mapenzi yake.
Wokovu Umeletwa Na Kristo
5 Maana Mungu hakuuweka ulimwengu ujao, tunaouzungumzia, chini ya mamlaka ya malaika. 6 Bali kama inavyothibitishwa katika sehemu fulani ya Maandiko, “Mwanadamu ni kitu gani hata umfi kirie, au mwana wa binadamu ni nani hata umjali? 7 Umemfanya kuwa chini kidogo ya malaika; wewe umemvika taji ya utukufu na heshima, 8 umemfanya kuwa mtawala wa vitu vyote.” Mungu ali poweka vitu vyote chini ya mamlaka ya mwanadamu, hakubakiza cho chote ambacho mwanadamu hakitawali. Lakini kwa wakati huu hatuoni kama kila kitu kiko chini ya mamlaka yake. 9 Lakini tunamwona Yesu, ambaye kwa muda mfupi alifanywa kuwa chini kidogo ya mal aika, sasa akiwa amevikwa taji ya utukufu na heshima kwa sababu aliteseka na kufa, ili kwa neema ya Mungu, aonje mauti kwa ajili ya watu wote.
10 Kwa maana ilikuwa ni sawa kabisa kwamba Mungu, ambaye kwa ajili yake na kwa uweza wake vitu vyote vimekuwepo, amfanye Mwan zilishi wa wokovu wao kuwa mkamilifu kwa njia ya mateso, ili awalete wana wengi washiriki utukufu wake. 11 Maana yule anayetakasa na wale wanaotakaswa, wote wanatoka katika uzao mmoja. 12 Ndio maana Yesu haoni aibu kuwaita wao ndugu zake, akisema: “Nitalitangaza jina lako kwa ndugu zangu, katikati yao nitakusifu.” 13 Na tena anasema, “Nitamwekea Mungu tumaini langu.” Na tena, “Niko hapa, mimi pamoja na watoto niliopewa na Mungu.”
Mungu.”
14 Basi, kwa kuwa watoto hao wana mwili na damu, yeye pia alishiriki katika ubinadamu wao, ili kwa kufa kwake apate kumwan gamiza yule mwenye mamlaka juu ya kifo, yaani shetani; 15 na hivyo awaweke huru wale ambao walikuwa utumwani maisha yao yote kwa sababu ya kuogopa kifo. 16 Maana ni wazi kwamba hakuja kuwa saidia malaika bali kuwasaidia uzao wa Ibrahimu. 17 Kwa sababu hii ilibidi awe kama ndugu zake kwa kila hali, apate kuwa kuhani mkuu mwenye huruma na mwaminifu katika huduma ya Mungu, ili aweze kujitoa kama sadaka kwa ajili ya dhambi za watu. 18 Na kwa kuwa yeye mwenyewe ameteswa na kujaribiwa, anaweza kuwasaidia wanaoj aribiwa.