Waebrania 6

1Basi sasa tutoke katika yale mafundisho ya msingi kuhusu Kristo, tupige hatua kufikia ukamilifu katika kuelewa kwetu. Hatupaswi tena kuwaeleza ninyi yale mafundisho ya msingi kuhusu kutubu na kuacha matendo yaletayo kifo, na kuhusu kumwamini Mungu pamoja na maagizo kuhusu ubatizo, kuwekea watu mikono, kufufuka kwa wafu na hukumu ya milele. Mungu akitujalia tutaendelea mbele.

Kwa maana haiwezekani tena kuwarejesha katika toba watu ambao waliwahi kuongoka, ambao wameonja uzuri wa mbinguni, wakashiriki Roho Mtakatifu, ambao wameonja wema wa neno la Mungu na nguvu za nyakati zijazo, kama wakikufuru. Kwa sababu wanamsulubisha tena Mwana wa Mungu mioyoni mwao na kumwaibisha hadharani. Ardhi ambayo baada ya kupata mvua ya mara kwa mara, hutoa mazao yanayowanufaisha wale ambao wanailima na kupokea bar aka kutoka kwa Mungu. Lakini kama ardhi hiyo itaotesha magugu na miiba, haina thamani, na inakaribia kulaaniwa. Mwisho wake ni kuchomwa moto.

Wanaopokea Ahadi Za Mungu

Ingawa tunasema hivi, ndugu zangu, kwa upande wenu tuna hakika ya mambo mazuri zaidi, yanayoandamana na wokovu. 10 Mungu si dhalimu hata asahau kazi yenu na upendo mliomwonyesha mlipowa saidia watu wake na mnavyoendelea kuwasaidia. 11 Tunapenda kila mmoja wenu aonyeshe bidii hiyo hiyo mpaka mwisho ili mpate kupo kea tumaini lenu. 12 Hatutaki muwe wavivu bali muige wale ambao kwa imani na subira hupokea yale yaliyoahidiwa na Mungu.

Uhakika Wa Ahadi Ya Mungu

13 Mungu alipompa Ibrahimu ahadi, aliapa kwa jina lake mwe nyewe kwa kuwa hapakuwa na mkuu kuliko yeye ambaye angeweza kuapa kwa jina lake. 14 Alisema, “Hakika nitakubariki na kukupatia watoto wengi.” 15 Na hivyo baada ya kungoja kwa subira, Abra hamu alipata ahadi hiyo.

16 Watu huapa kwa mtu aliye mkuu kuliko wao, na kiapo hicho huthibitisha kinachosemwa na humaliza ubishi wote. 17 Kwa hiyo Mungu alipotaka kuwahakikishia warithi wa ahadi yake kuhusu maku sudi yake yasiyobadilika, aliwathibitishia kwa kiapo. 18 Mungu alifanya hivyo ili, kwa kutumia mambo haya mawili yasiyobadilika, na ambayo Mungu hawezi kusema uongo, sisi tuliokimbilia usalama kwake tutiwe moyo, tushikilie kwa uthabiti tumaini lililowekwa mbele yetu.

19 Tunalo tumaini hili kama nanga ya roho zetu yenye nguvu na imara. Tumaini hili linaingia hadi ndani ya pazia 20 ambamo Yesu ameingia akitutangulia; ameingia huko kwa niaba yetu. Yeye amekuwa kuhani mkuu milele, kama Melkizedeki.