Yesu Ni Mkuu Kuliko Musa
1Kwa hiyo, ndugu zangu watakatifu, ambao mmeshiriki wito wa mbinguni, mtafakarini Yesu, mtume na kuhani mkuu wa imani tunay oikiri.
2Kwa maana Yesu alikuwa mwaminifu kwa Mungu aliyemchagua, kama vile Musa alivyokuwa mwaminifu katika nyumba ya Mungu. 3Lakini Yesu amehesabiwa kuwa anastahili utukufu zaidi kuliko Musa, kama vile mjenzi wa nyumba anavyopewa heshima zaidi kuliko nyumba aliyoijenga. 4Maana kila nyumba hujengwa na mtu fulani bali aliyejenga vitu vyote ni Mungu. 5Ni kweli kwamba Musa ali kuwa mwaminifu katika nyumba yote ya Mungu kama mtumishi, akishu hudia juu ya yale mambo ambayo Mungu angeyatamka baadaye, 6lakini Kristo alikuwa mwaminifu katika nyumba ya Mungu kama mwana. Na sisi ni nyumba yake, ikiwa tutashikilia ujasiri wetu na lile tumaini tunalojivunia.
Jihadharini Na Kutokuamini
7Kwa hiyo, kama Roho Mtakatifu asemavyo, “Leo, mkiisikia sauti yake, 8msiifanye mioyo yenu kuwa migumu kama mlivyofanya wakati wa uasi , siku ile ya majaribio jangwani, 9ambapo baba zenu walinijaribu wakaona kazi zangu kwa miaka arobaini. 10Kwa hiyo kizazi kile kilinikasirisha, nikasema, ‘Mioyo ya watu hao imepotoka; hawajapata kujua njia zangu.’ 11Katika hasira yangu nikaapa, ‘Hawataingia kwenye pumziko langu kamwe.’
12Angalieni, ndugu zangu, asiwepo miongoni mwenu mtu ye yote mwenye moyo wa dhambi, usioamini, unaomfanya ajitenge na Mungu wa uzima. 13Bali muonyane kila siku maadamu bado ni ‘ ‘leo” ili asiwepo mtu kati yenu anayefanywa mkaidi na udangany ifu wa dhambi. 14Kwa maana sisi ni washiriki pamoja na Kristo iwapo tutashikilia tumaini letu la kwanza kwa uaminifu mpaka mwisho. 15Kama Maandiko yalivyosema: “Leo mkiisikia sauti yake, msiifanye mioyo yenu kuwa migumu. Kama mlivyofanya wakati wa uasi.” 16Ni nani hao waliosikia lakini wakaasi? Si wale wote waliotoka Misri wakiongozwa na Musa? 17Na ni nani waliom kasirisha Mungu kwa miaka arobaini? Si wale waliofanya dhambi wakafa jangwani? 18Na ni nani ambao Mungu aliapa kuwa hawatain gia kwenye pumziko lake, isipokuwa wale waliokataa kutii? 19Kwa hiyo tunaona kwamba walishindwa kuingia kwa sababu ya kutokuamini kwao. Pumziko La Sabato