1Yesu alipomaliza kuwaambia watu mambo haya alikwenda Kaper naumu. 2 Huko mtumishi wa jemadari mmoja wa Kirumi ambaye bwana wake alimpenda, alikuwa mgonjwa sana, karibu ya kufa. 3 Jemadari huyo aliposikia habari za Yesu aliwatuma wazee wa Kiyahudi wakam wombe aje kumponya mtumishi wake. 4 Wale wazee walipofika kwa Yesu walimsihi sana amsaidie yule jemadari wakisema, “Mtu huyu anastahili msaada wako kwani 5 yeye analipenda taifa letu, tena ametujengea sinagogi.”
6 Hivyo Yesu akaongozana nao. Hata alipoikaribia nyumba yake, yule jemadari aliwatuma rafiki zake, kumwambia Yesu, “Bwana, usijisumbue kuingia nyumbani kwangu. Sistahili heshima kubwa kiasi hicho, 7 wala sikuona ninastahili mimi kuja kukuona binafsi. Sema neno moja tu na mtumishi wangu atapona. 8 Katika nafasi yangu ya kazi nina wakubwa wangu na wapo askari wengine chini ya mamlaka yangu. Nikitoa amri kwa askari, ‘Nenda!’ huenda; nikimwambia mwingine, ‘Njoo!’ huja; na nikimwambia mtumishi wangu, ‘Fanya hiki,’ hufanya.” 9 Yesu aliposikia maneno haya alishangaa sana. Akawageukia wale watu walioongozana naye aka waambia, “Hata katika Israeli yote sijakutana na mtu mwenye imani kama hii.” 10 Na wale waliotumwa kwa Yesu waliporudi nyumbani kwa yule jemadari walikuta yule mtumishi amepona kabisa.
Yesu Amfufua Mtoto Wa Mjane
11 Baada ya siku hiyo, Yesu alikwenda mji mmoja uitwao Naini. Wanafunzi wake na umati wa watu waliongozana naye. 12 Alipokaribia njia ya kuingia mjini alikutana na watu wal iobeba maiti wakitoka nje ya mji. Marehemu alikuwa mtoto wa kiume wa pekee wa mama mmoja mjane na umati wa watu wa mji ule ulikuwa pamoja na huyo mama. 13 Bwana Yesu alipomwona yule mjane moyo wake ulijaa huruma, akamwambia, “Usilie.” 14 Kisha akalisoge lea lile jeneza akaligusa na wale waliolibeba wakasimama. Ndipo akasema: “Kijana nakuambia, amka!” 15 Yule aliyekuwa marehemu akaamka, akakaa na akaanza kusema! Yesu akamkabidhi kwa mama yake.
16 Watu wote wakajawa na hofu. Wakamtukuza Mungu wakisema, “Nabii mkuu ametokea kati yetu. Mungu amekuja kutuokoa sisi watu wake.” 17 Habari hizi za mambo aliyofanya Yesu zikaenea Uyahudi nzima na sehemu za jirani.
Hakuna Aliye Mkuu Kuliko Yohana
18 Wanafunzi wa Yohana Mbatizaji walipomweleza Yohana habari hizi zote aliwaita wawili kati yao 19 akawatuma wakamwulize Bwana Yesu, “Wewe ndiye yule ajaye, au tumtazamie mwingine?”
201 Walipofika kwa Yesu wakamwambia, “Yohana Mbatizaji ametutuma tukuulize, ‘Wewe ndiye yule ajaye au tumtazamie mwin gine?”’
21 Wakati huo huo, Yesu aliwaponya wengi waliokuwa na magonjwa, maumivu na pepo wachafu. Pia akawawezesha vipofu wengi kuona. 22 Ndipo akawajibu wale wanafunzi waliotumwa, “Nendeni mkamwambie Yohana yote mliyoyaona na kusikia: vipofu wanapata kuona, vilema wanatembea, wenye ukoma wanapona, viziwi wanasikia, wafu wanafufuliwa na maskini wanasikia Habari Njema. 23 Amebari kiwa mtu asiyepoteza imani yake kwangu.” 24 Wanafunzi wa Yohana walipoondoka, Yesu akaanza kuwaeleza watu juu ya Yohana: “Hivi mlipokwenda nyikani mlikwenda kuona nini? Nyasi zikipeperushwa na upepo? 25 Kama sivyo, mlikwenda kuona nini basi? Mtu aliyevaa nguo za fahari? Sidhani! Watu wanaovaa nguo za fahari na kuishi maisha ya anasa hukaa katika majumba makubwa. 26 Sasa mlikwenda kuona nini? Mlikwenda kuona nabii? Naam! Tena aliye mkuu kuliko nabii. 27 Huyu Yohana ndiye anayezungumzwa katika Maandiko yase mayo: ‘Tazama, namtuma mjumbe wangu akutangulie, ili akuandalie njia.’ 28 Nawaambia, kati ya binadamu wote, hakuna aliye mkuu kumzidi Yohana. Hata hivyo aliye mdogo kabisa katika Ufalme wa Mungu ni mkuu kuliko Yohana. 29 Watu wote waliosikia maneno hayo, ikiwa ni pamoja na watoza ushuru, walimtukuza Mungu kwa kuwa wao waliukubali ubatizo wa Yohana. 30 Bali Mafarisayo na wanasheria walikataa mpango wa Mungu kwao kwa kutokukubali kubatizwa na Yohana. 31 Yesu akawau liza, “Niseme nini juu ya watu wa kizazi hiki? Niwafananishe na nini? 32 Wao wamefanana na watoto waliokaa sokoni wakijibizana na wenzao wakisema: ‘Tuliwaimbia nyimbo za shangwe, hamkucheza. Tuliwaimbia nyimbo za msiba, hamkuomboleza.’ 33 Yohana Mbatizaji alikuwa akifunga na hakuonja divai maishani mwake, ninyi mkasema, ‘Ana wazimu!’ 34 Lakini mimi nakula na kunywa, nanyi mnasema: ‘Mtazameni mlafi na mlevi! Rafiki wa watoza kodi na wenye dhambi.’ 35 Lakini hekima ya Mungu inadhihirishwa kuwa kweli na wote wanaoipokea.”
Mwanamke Aliyempaka Yesu Manukato
36 Farisayo mmoja alimwalika Yesu nyumbani kwake kwa chak ula. Naye akaenda akakaa ale chakula. 37 Katika mji ule palikuwa na mwanamke mmoja kahaba. Naye aliposikia kuwa Yesu atakula nyum bani kwa yule Farisayo, alichukua chupa ya alabasta iliyojaa man ukato 38 akaenda, akakaa nyuma ya Yesu, karibu na miguu yake. Kisha akaanza kulia, machozi yake yakidondokea miguuni mwa Yesu, akayafuta kwa nywele zake. Huku akimbusu miguu na kuimiminia yale manukato.
39 Yule Farisayo aliyemwalika Yesu alipoona yanayotendeka, akawaza moyoni mwake, “Huyu mtu hawezi kuwa ni nabii. Kama ange kuwa nabii angetambua kuwa huyu mwanamke ni kahaba.” 40 Kisha Yesu akijua mawazo ya yule Farisayo akamwambia, “Simoni, kuna jambo nataka kukuambia.” Simoni akajibu “Sema, mwalimu.” 41 “Palikuwa na mtu mmoja aliyewakopesha watu wawili fedha: mmoja shillingi elfu tano na mwingine shillingi mia tano. 42 Wote wawili wakashindwa kulipa madeni yao, kwa hiyo akaamua kuwasamehe. Unadhani kati yao, ni yupi aliyempenda zaidi yule aliyewasamehe?” 43 Simoni akajibu, “Nadhani ni yule aliyesame hewa deni kubwa zaidi.” Yesu akamwambia, “Umejibu sawa.” 44 Ndipo akamgeukia yule mwanamke akamwambia Simoni, “Unamwona mwanamke huyu? Niliingia nyumbani kwako hukunipa maji ya kunawa miguu, lakini huyu ameniosha miguu kwa machozi yake na kunifuta kwa nywele zake. 45 Hukunisalimu kwa busu, lakini huyu mwanamke amekuwa akiibusu miguu yangu tangu niingie hapa. 46 Hukunipaka mafuta kichwani kama ilivyo desturi lakini huyu mwanamke ameipaka miguu yangu manukato. 47 Kwa hiyo nakuambia, upendo mkubwa aliouonyesha huyu mama unathibitisha kuwa dhambi zake ambazo ni nyingi zimesamehewa. Lakini ye yote asamehewaye kidogo, huonyesha upendo kidogo.”
48 Akamwambia yule mwanamke, “Dhambi zako zimesamehewa.” 49 Ndipo wale wageni wengine waliokuwepo wakaanza kuulizana, “Hivi huyu ni nani, hata aweze kusamehe dhambi?” 50 Yesu akam wambia yule mwanamke, “Imani yako imekuokoa; nenda kwa amani.”