Kuzaliwa Kwa Yesu
1Siku zile Kaisari Augusto, mtawala wa milki ya Kirumi, aliamuru ya kwamba watu wote wa milki yake waandikishwe. 2 Hii ilikuwa ni sensa ya kwanza kufanyika nayo ilitokea wakati Kirenio alipokuwa liwali wa Siria. 3 Watu wote walikwenda katika sehemu walikozaliwa ili waandikishwe huko. 4 Yusufu alitoka mji wa Nazareti uliopo Galilaya akaenda mpaka Bethlehemu mji wa Daudi kwa sababu yeye alikuwa wa ukoo wa Daudi. 5 Alikwenda huko kujiandikisha pamoja na mchumba wake Mariamu ambaye kwa wakati huu alikuwa mja mzito.
6 Walipokuwa Bethlehemu, wakati wa Mariamu kujifungua uli fika, 7 naye akamzaa mtoto wa kiume, kifungua mimba. Akamfunika kwa vinguo na kumlaza horini, kwa sababu hapakuwa na nafasi katika nyumba ya wageni.
Wachungaji Wapata Habari
8 Usiku ule walikuwako wachungaji wakilinda kondoo zao nje ya mji. 9 Ghafla malaika wa Bwana akawatokea, na utukufu wa Mungu ukawang’azia pande zote. Wakajawa na hofu kuu. 10 Lakini malaika akawatuliza akisema: “Msiogope! Nawaletea habari njema ya furaha kubwa, na habari hii ni kwa faida ya watu wote! 11 Kwa maana leo katika mji wa Bethlehemu, amezaliwa Mwokozi ambaye ndiye Kristo Bwana. 12 Na hivi ndivyo mtakavyomtambua: mtamkuta mtoto mchanga amefunikwa vinguo na kulazwa horini.”
13 Mara jeshi kubwa la malaika wa mbinguni likatokea na pamoja wakamsifu Mungu wakiimba: 14 “Atukuzwe Mungu juu mbin guni, na duniani iwepo amani kwa watu ambao amependezwa nao.”
15 Malaika hao waliporudi mbinguni wale wachungaji walish auriana: “Jamani, twendeni Bethlehemu tukaone mambo haya ya ajabu yaliyotokea, ambayo Bwana ametufahamisha.”
16 Kwa hiyo wakaenda haraka Bethlehemu, wakawakuta Mariamu na Yusufu; na yule mtoto mchanga alikuwa amelala mahali pa kulia ng’ombe. 17 Walipomwona mtoto, wakawaeleza yale waliyokuwa wameambiwa. 18 Na wote waliosikia habari hizi wakastaajabia yale waliyoambiwa na wachungaji. 19 Lakini Mariamu akayaweka mambo haya yote moyoni mwake, akayafikiria mara kwa mara.
20 Wale wachungaji wakarudi, huku wakimtukuza Mungu na kum sifu kwa yale waliyoyasikia na kuyaona.
21 Hata baada ya siku nane, ilipotimia siku ya kumtahiri mtoto, aliitwa Yesu; jina alilopewa na malaika kabla hata haja chukuliwa mimba.
Yesu Apelekwa Hekaluni
22 Baada ya kutimia kwa muda wa utakaso wa Yusufu na Mar iamu, kwa mujibu wa sheria ya Musa, walimpeleka mtoto Yerusalemu, wakamtoa kwa Bwana 23 kama ilivyotakiwa na sheria ya Bwana -“Kila mtoto wa kiume wa kwanza atakabidhiwa kwa Bwana.” 24 Pia walitoa sadaka, kama ilivyotakiwa na sheria ya Bwana: “Hua wawili au makinda ya njiwa wawili.” 25 Na alikuwepo huko Yerusalemu mzee mmoja jina lake Simeoni ambaye alikuwa mwenye haki na mcha Mungu. Siku zote alikuwa akitarajia ukombozi wa Israeli na Roho Mtakatifu alikuwa juu yake. 26 Pia Roho Mtaka tifu alikuwa amemhakikishia kuwa hangekufa kabla ya kumwona Kristo wa Bwana. 27 Kwa hiyo, akiwa ameongozwa na Roho Mtaka tifu, Simeoni alikwenda Hekaluni. Wazazi walipomleta mtoto Yesu ili wamfanyie kama ilivyokuwa desturi ya sheria, 28 Simeoni alimpokea mtoto mikononi mwake akamshukuru Mungu akisema: 29 “Sasa Bwana, niruhusu mimi mtumishi wako niende kwa amani kama ulivyoniahidi, 30 kwa sababu macho yangu yameuona wokovu 31 ulioandaa mbele ya watu wote, 32 nuru itakayowaangazia watu wa mataifa na kuleta utukufu kwa watu wako Israeli.” 33 Wazazi wa mtoto walistaajabu kwa yale yaliyokuwa yakisemwa kumhusu mtoto wao. 34 Simeoni akawabariki. Kisha akamwambia Mariamu, mama yake, “Mtoto huyu amechaguliwa na Mungu kwa makusudi ya kuanga mizwa na kuokolewa kwa wengi katika Israeli. Atakuwa ishara ya onyo kutoka kwa Mungu ambayo watu wengi wataikataa 35 ili kudhi hirisha mawazo yao ya ndani. Na uchungu kama kisu kikali utaku choma moyoni.” 36-37 ,Tena, alikuwepo Hekaluni nabii mmoja mwanamke, mzee sana, jina lake Ana, binti wa Fanueli, wa kabila la Asheri. Nabii Ana alikuwa mjane wa miaka themanini na minne naye alikuwa ameolewa kwa miaka saba tu mumewe akafariki. Yeye aliishi humo Hekaluni daima, akimwabudu Mungu na kuomba na kufunga.
38 Wakati huo huo, Ana alikuja mbele akamshukuru Mungu na kueleza habari za huyo mtoto kwa watu wote waliokuwa wakitarajia ukombozi wa Yerusalemu. 39 Yusufu na Mariamu walipokamilisha mambo yote yaliyotakiwa na sheria ya Mungu, walirudi nyumbani kwao Nazareti katika Wilaya ya Galilaya. 40 Yesu aliendelea kukua, akawa kijana mwenye nguvu na hekima, akijaa baraka za
Mtoto Yesu Adhihirisha Hekima Yake
41 kila mwaka wazazi wake walikwenda Yerusalemu kushiriki katika siku kuu ya Pasaka. 42 Yesu alipokuwa na umri wa miaka kumi na miwili wote walikwenda kwenye sikukuu hiyo kama desturi ilivyokuwa. 43 Sikukuu ilipokwisha walianza safari ya kurudi nyumbani. Yesu akabaki Yerusalemu pasipo wazazi wake kujua. 44 Wao walidhani yupo nao kwenye msafara kwa hiyo wakaenda mwendo wa siku nzima. Walipotambua kwamba hawakuwa naye, walianza kumtafuta kati ya jamaa na marafiki. 45 Hawakumpata, kwa hiyo wakarudi Yerusalemu wakimtafuta. 46 Siku ya tatu wakamkuta Hek aluni ameketi kati ya walimu wa sheria, akiwasikiliza na kuwau liza maswali. 47 Wote waliomsikia walistaajabishwa na uwezo wake mkubwa wa kuelewa na majibu aliyoyatoa.
48 Wazazi wake walipomwona walishangaa. Mama yake akamwul iza: “Mwanangu, mbona umetufanyia hivi? Baba yako na mimi tume hangaika kukutafuta kila mahali kwa wasiwasi mkubwa.” 49 Lakini yeye akajibu: “Kwa nini mlihangaika kunitafuta? Hamkujua ninge kuwa hapa Hekaluni kwenye nyumba ya Baba yangu? 50 Lakini wao hawakuelewa maana ya jibu lake.
51 Akarudi pamoja na wazazi wake hadi Nazareti. Akawa aki watii, na mama yake akayaweka moyoni mambo haya yote. 52 Basi Yesu akaendelea kuongezeka katika kimo na hekima, akipendwa na