Yesu Azungumzia Tena Juu Ya Kifo Chake
1Yesu akawachukua wale wanafunzi wake kumi na wawili kando akawaambia, “Sikilizeni! Tunakwenda Yerusalemu, na yote yaliy oandikwa na manabii kunihusu mimi Mwana wa Adamu yatatimia. 2 Akawaambia, “Katika mji mmoja alikuwapo hakimu ambaye hakumwogopa Mungu wala kumjali mtu. 3 Na alikuwapo mjane mmoja katika mji huo ambaye alikuwa akija kwake mara kwa mara akimwomba, ‘Tafadhali niamulie haki kati yangu na adui yangu.’ 4 Kwa muda mrefu yule hakimu hakufanya lo lote. Lakini hatimaye akasema moyoni mwake, ‘Simwogopi Mungu wala simjali mtu 5 lakini kwa kuwa huyu mjane ananisumbua na kesi yake, nitamwamulia haki asije akanichosha kwa kuja kwake mara kwa mara.”’ 6 Bwana akasema, “Mnasikia asemavyo huyu hakimu dhalimu. 7 Na Mungu je, hatawatendea haki watu wake wanaomlilia mchana na usiku? Je, atakawia kuwapa msaada? 8 Nina waambieni atahakikisha amewatendea haki upesi. Lakini je, mimi Mwana wa Adamu nitakaporudi duniani nitakuta watu wanadumu katika imani?”
Mfano Wa Farisayo Na Mtoza Ushuru
9 Yesu alitoa mfano huu kwa ajili ya wale waliojiona kuwa wao ni wenye haki na kuwadharau wengine. 10 Watu wawili walikwenda hekaluni kusali, mmoja wao alikuwa Farisayo na mwingine alikuwa mtoza ushuru. 11 yule Farisayo alisimama akasali kimoyomoyo. ‘Ninakushukuru Mungu kwa sababu mimi si kama watu wengine: wany ang’anyi, wadhalimu, wazinzi, au kama huyu mtoza ushuru. 12 Mimi nafunga mara mbili kwa juma na kutoa sehemu ya kumi ya mapato yangu.’ 13 Lakini yule mtoza ushuru alisimama mbali. Hakuthubutu hata kuinua uso wake kutazama mbinguni; bali alijipiga kifuani kwa majuto akasema, ‘Mungu, nihurumie, mimi mwenye dhambi.’
14 Nawaambieni, huyu mtoza ushuru alirudi nyumbani akiwa amehesabiwa haki mbele za Mungu na wala si yule Farisayo. Kwa maana ye yote ajikwezaye atashushwa na ye yote ajinyenyekezaye, atainuliwa.”
Yesu Awabariki Watoto Wadogo
15 Watu wakamletea Yesu watoto wao wachanga ili awaguse. Wanafunzi walipowaona, wakawakemea. 16 Lakini Yesu akawaita wale watoto waje kwake, akasema, “Waacheni watoto wadogo waje kwangu, msiwazuie, kwa maana Ufalme wa Mungu ni wa watu walio kama hawa watoto. 17 Nawaambia hakika, ye yote ambaye hataupokea Ufalme wa Mungu kama mtoto mdogo, hatauingia kamwe.”
18 Kiongozi mmoja akamwuliza Yesu, “Mwalimu mwema, nifanye nini ili niurithi uzima wa milele?”
19 Yesu akamjibu, “Mbona unaniita mwema? Hakuna mtu aliye mwema ila Mungu peke yake. 20 Unazifahamu amri: ‘Usizini, usiue, usiibe, usishuhudie uongo, waheshimu baba yako na mama yako?”’ 21 Akajibu, “Amri zote hizi nimezishika tangu utoto wangu.”
22 Yesu aliposikia haya, akamwambia, “Bado unahitaji kufa nya jambo moja. Nenda ukauze vitu vyote ulivyo navyo, uwagawie maskini, nawe utakuwa na hazina mbinguni. Kisha njoo, unifuate.” 23 Aliposikia hayo alisikitika, kwa maana alikuwa tajiri sana.
24 Yesu alipoona yule kiongozi amesikitika, akasema, “Jinsi gani ilivyo vigumu kwa tajiri kuingia katika Ufalme wa Mungu! 25 Ni rahisi zaidi kwa ngamia kupita katika tundu la sindano kuliko tajiri kuingia katika Ufalme wa Mungu.” 26 Wale waliosi kia hayo wakauliza, “Kama ni hivyo, ni nani basi awezaye kuoko lewa?” 27 Yesu akajibu, “Yasiyowezekana kwa binadamu yaweze kana kwa Mungu.” 28 Ndipo Petro akasema, “Sisi je? Tumeacha vyote tulivyokuwanavyo tukakufuata!” 29 Yesu akajibu, “Nawaam bia hakika, hakuna hata mmoja aliyeacha nyumba yake, au mke, ndugu, wazazi au watoto kwa ajili ya Ufalme wa Mungu, 30 ambaye hatapewa na Mungu mara nyingi zaidi ya hivyo katika maisha haya na kupata uzima wa milele katika maisha yajayo.” 32 Nitatiwa mikononi mwa watawala wa Kirumi. Watu watanizomea, watanitukana na kunitemea mate. 33 Watanipiga na kuniua, lakini siku ya tatu nitafufuka.”
34 Wanafunzi wake hawakuelewa mambo haya. Maana ya maneno haya ilikuwa imefichika kwao, nao hawakujua Yesu alikuwa anazun gumzia nini.
Yesu Amponya Kipofu
35 Yesu na wafuasi wake walipokaribia Yeriko, walimpita kipofu mmoja aliyekuwa amekaa kando ya njia, akiomba fedha. 36 Kipofu huyo aliposikia umati wa watu ukipita aliuliza, “Kuna nini?” 37 Wakamwambia, “Yesu Mnazareti anapita.” 38 Akaita kwa sauti kuu, “Yesu, Mwana wa Daudi! Nionee huruma!” 39 Wale waliokuwa wakiongoza msafara wakamkemea wakamwambia akae kimya. Lakini yeye akapiga kelele zaidi, “Mwana wa Daudi! Nionee huruma!”
40 Yesu akasimama, akaagiza huyo mtu aletwe kwake. Alipo karibia, Yesu akamwuliza, 41 “Unataka nikufanyie nini?” Aka jibu, “Bwana, nataka kuona.”
42 Yesu akamwambia, “Basi upate kuona; imani yako imekupo nya.” 43 Akaweza kuona mara hiyo hiyo akamfuata Yesu, huku akimsifu Mungu. Watu wote walioshuhudia mambo hayo, nao wakamsifu Mungu.