Luka 16

1Akawaambia wanafunzi wake, “Palikuwa na tajiri mmoja na meneja wake. Ilisemekana kwamba huyo meneja alikuwa anatumia vibaya mali ya tajiri yake. Basi huyo tajiri akamwita meneja wake akamwuliza, ‘Ni mambo gani haya ninayosikia kukuhusu? Nitay arishie hesabu ya mapato na matumizi ya mali yangu kwa maana hutaendelea kuwa meneja tena.’

“Yule meneja akawaza moyoni mwake, ‘Nitafanya nini sasa? Bwana wangu anataka kuniondoa katika kazi yangu. Sina nguvu za kulima, na ninaona aibu kuombaomba! Najua nitakalofanya ili nikipoteza kazi yangu hapa, watu wanikaribishe nyumbani kwao.’

“Kwa hiyo akawaita wadeni wote wa tajiri wake, mmoja mmoja. Akamwuliza wa kwanza, ‘Deni lako kwa bwana wangu ni kiasi gani?’ Akajibu, ‘Galoni mia nane za mafuta ya alizeti.’ Meneja akamwambia, ‘Chukua hati hii ya deni lako, ibadilishe upesi, uan dike mia nne.’ Kisha akamwuliza wa pili, ‘Na wewe deni lako ni kiasi gani?’ Akajibu, ‘Vipimo elfu moja vya ngano.’ Yule meneja akamwambia, ‘ Chukua hati yako, uandike mia nane.’

“Yule tajiri akamsifu yule meneja mjanja kwa jinsi alivy otumia busara. Kwa maana watu wanaojishughulisha na mambo ya dunia hii hutumia busara zaidi kuliko watu wa nuru kukamilisha mambo yao. Nami nawaambieni, tumieni mali ya dunia hii kujipa tia marafiki, ili itakapokwisha mkaribishwe katika makao ya milele.

10 “Mtu ambaye ni mwaminifu katika mambo madogo, atakuwa mwaminifu hata katika mambo makubwa; na mtu ambaye si mwaminifu katika mambo madogo hatakuwa mwaminifu katika mambo makubwa. 11 Na ikiwa hamkuwa waaminifu katika kutunza mali ya dunia hii, ni nani atakayewaamini awakabidhi mali ya kweli? 12 Na kama ham kuwa waaminifu na mali ya mtu mwingine, ni nani atakayewapa mali yenu wenyewe? 13 Hakuna mtumishi awezaye kuwatumikia mabwana wawili. Ama atamchukia mmoja na kumpenda mwingine; au atamheshimu mmoja na kumdharau mwingine. Hamwezi kumtumikia Mungu pamoja na mali.”

14 Basi Mafarisayo, ambao wenyewe walipenda fedha, waliyasi kia hayo yote wakamcheka. 15 Yesu akawaambia, “Ninyi mnajifa nya kuwa wenye haki mbele za wanadamu, lakini Mungu anaijua mioyo yenu. Kwa maana vile vitu ambavyo wanadamu wanavithamini sana, kwa Mungu havina thamani yo yote.”

Sheria Na Ufalme Wa Mungu

16 “Sheria ya Musa na Maandiko ya manabii yalitumiwa mpaka wakati wa Yohana Mbatizaji. Tangu wakati huo Habari Njema za Ufalme wa Mungu zinahubiriwa na kila mtu anafanya bidii kuingia huko. 17 Lakini ni rahisi zaidi kwa mbingu na nchi kutoweka kuliko hata herufi moja katika sheria kufutwa.

18 Mtu ye yote anayempa mke wake talaka na kumwoa mke mwin gine anazini, na mwanamume amwoaye mwanamke aliyeachwa na mumewe, ewe, anazini.”

Mfano Wa Tajiri Na Maskini Lazaro

19 Akasema, “Palikuwa na tajiri mmoja aliyevaa nguo za rangi ya zambarau na kitani safi, nguo za gharama kubwa, kila siku. 20 Na maskini mmoja, jina lake Lazaro, mwenye vidonda mwili mzima, alikuwa akiletwa mlangoni kwa huyo tajiri kila siku. 21 Lazaro alikuwa akitamani kula makombo yaliyodondoka mezani kwa tajiri. Hata mbwa walikuwa wakiramba vidonda vyake.

22 “Hatimaye, yule maskini alikufa. Malaika wakamchukua akakae pamoja na Ibrahimu mbinguni. Yule tajiri naye pia akafa, akazikwa. 23 Alipokuwa kuzimuni ambapo alikuwa akiteseka, alita zama juu, akamwona Ibrahimu kwa mbali na Lazaro karibu yake. 24 Akaita, ‘Baba Ibrahimu, nionee huruma umtume Lazaro achovye japo ncha ya kidole chake katika maji aupoze ulimi wangu maana ninateseka kwenye moto huu.’ 25 Lakini Ibrahimu akamjibu, ‘Mwa nangu, kumbuka kwamba ulipokuwa hai ulipata kila kitu kizuri uli chotaka, ambapo Lazaro alipokea mabaya. Lakini sasa anafarijika hapa na wewe unateseka. 26 Isitoshe, kati yetu na ninyi huko, kumewekwa bonde kubwa lisilopitika ili wale wanaotaka kutoka huku kuja huko au kutoka huko kuja huku wasiweze.’ 27 Akasema, ‘Basi, baba, tafadhali umtume Lazaro aende nyumbani kwa baba yangu, 28 awaonye ndugu zangu, wasije wao pia wakaletwa mahali hapa pa mateso watakapokufa.’ 29 Ibrahimu akamjibu, ‘Ndugu zako wanazo sheria za Musa na maandiko ya Manabii. Itawapasa watii hayo.’ Lakini yule tajiri akazidi kumsihi, 30 ‘Hapana baba Ibrahimu, ndugu zangu hawatashawishiwa na hayo. Lakini mtu kutoka kuzimu akitumwa kwao watatubu na kuziacha dhambi zao.’

31 “Ibrahimu akamwambia, ‘Wasiposikiliza na kutii sheria za Musa na Maandiko ya manabii, hawatashawishika kutubu hata kama mtu akifufuka kutoka kuzimu.”’