1Wakati huo, watu fulani walimwambia Yesu habari za Wagali laya ambao Pilato aliwaua na damu yao akaichanganya na damu ya sadaka waliyokuwa wakimtolea Mungu. 2 Yesu akawajibu, “Mnadhani Wagalilaya hao walikufa kifo cha namna hiyo kwa kuwa walikuwa na dhambi kuwazidi Wagalilaya wengine wote? 3 Sivyo hata kidogo. Ninyi pia msipoacha dhambi zenu mtaangamia vivyo hivyo. 4 Au wale watu kumi na wanane ambao walikufa walipoangukiwa na mnara huko Siloamu, mnadhani wao walikuwa waovu kuliko watu wote waliokuwa wanaishi Yerusalemu? 5 Nawaambieni, sivyo! Ninyi pia msipoacha dhambi zenu, mtaangamia vivyo hivyo.”
Mfano Wa Mti Usiozaa Matunda
6 Kisha Yesu akatoa mfano huu: “Mtu mmoja alikuwa na mtini uliopandwa katika shamba lake la mizabibu, akaenda kutafuta tini kwenye mti huo asipate hata moja. 7 Kisha akamwambia mtunza shamba:, ‘Kwa muda wa miaka mitatu sasa nimekuwa nikija kutafuta matunda kwenye mtini huu, sijawahi kupata hata moja. Ukate, sioni kwa nini uendelee kutumia ardhi bure!’ 8 Yule mtunza shamba akam jibu, ‘Bwana, tuuache tena kwa mwaka mmoja zaidi, niulimie, niuwekee mbolea. 9 Ukizaa matunda, vema; na usipozaa baada ya hapo, utaukata.”’ Yesu Amponya Mwanamke Siku Ya Sabato
10 Siku moja ya sabato, Yesu alikuwa akifundisha katika sinagogi mojawapo. 11 Na hapo alikuwapo mwanamke mmoja alikuwa ameugua kwa muda wa miaka kumi na minane kutokana na pepo ali yekuwa amemwingia. Hali hiyo ilimfanya mwanamke huyo apindike hata asiweze kusimama wima. 12 Yesu alipomwona, akamwita akam wambia, “Mama, uwe huru, umepona ugonjwa wako.” 13 Yesu akamwekea mikono, na mara akasimama wima, akamtukuza Mungu. 14 Mkuu wa sinagogi akakasirika kwa kuwa Yesu alikuwa ameponya mtu siku ya sabato. Kwa hiyo akawaambia watu, “Kuna siku sita ambazo watu wanapaswa kufanya kazi, katika siku hizo, njooni mpo nywe; msije kuponywa siku ya sabato!”
15 Lakini Bwana akamjibu, “Ninyi ni wanafiki! Kila mmoja wenu humfungulia ng’ombe wake au punda wake kutoka zizini akampeleka kumnywesha maji siku ya sabato. 16 Je, huyu mama, ambaye ni binti wa Ibrahimu aliyefungwa na shetani kwa miaka yote hii kumi na minane, hastahili kufunguliwa kutoka katika kifungo hicho siku ya sabato?” 17 Aliposema haya, wapinzani wake wakaona aibu lakini watu wakafurahi kwa ajili ya mambo ya ajabu aliyoyafanya. Mfano Wa Punje Ya Haradali
18 Kisha Yesu akauliza, “Ufalme wa Mungu ukoje? Nitaufanan isha na nini? 19 Umefanana na punje ndogo sana ya haradali ambayo mtu aliichukua akaipanda katika shamba lake, ikamea, ikawa mti na ndege wa angani wakatengeneza viota vyao kwenye matawi yake.”
Mfano Wa Hamira
20 Yesu akauliza tena, “Nitaufananisha na nini Ufalme wa Mungu? 21 Uko kama hamira ambayo mwanamke aliichukua na kuichan ganya kwenye vipimo vitatu vya unga wa ngano na wote ukaumuka.”
Mlango Mwembamba
22 Yesu akapita katika miji na vijiji akifundisha wakati akisafiri kwenda Yerusalemu. 23 Mtu mmoja akamwuliza, “Bwana, ni watu wachache tu watakaookolewa?” 24 Akajibu, “Jitahidini kuingia kwa kupitia mlango mwembamba; kwa maana, nawaambia, wengi watataka kuingia na hawataweza. 25 Wakati mwenye nyumba ataka poamka na kufunga mlango, mtasimama nje mkigonga mlango na kusema, ‘Bwana utufungulie!’ Atawajibu, ‘Sijui mtokako!’ 26 Nanyi mtamjibu, ‘Tulikula na kunywa pamoja nawe, ulifundisha katika mitaa yetu!’ 27 Lakini yeye atawajibu, ‘Sijui mtokako. Ondokeni kwangu ninyi watenda maovu!’ 28 Ndipo kutakuwapo na kilio na kusaga meno mtakapomwona Ibrahimu, Isaka na Yakobo na manabii wote wakiwa katika Ufalme wa Mungu, wakati ninyi mkiwa mmetupwa nje. 29 Watu watakuja kutoka mashariki na magharibi na kaskazini na kusini na wataketi kwenye sehemu walizoandaliwa kar amuni katika Ufalme wa Mungu. 30 Hakika wapo watu ambao sasa wako mwisho watakaokuwa wa kwanza, na wengine walio wa kwanza sasa watakaokuwa wa mwisho.” Yesu Aomboleza Juu Ya Yerusalemu
31 Wakati huo huo baadhi ya Mafarisayo wakamwendea Yesu wakamwambia, “Ondoka hapa uende mahali pengine kwa maana Herode anataka kukuua.” 32 Yesu akawajibu, “Nendeni mkamwambie yule mbweha: ninafukuza pepo na kuponya wagonjwa leo na kesho, na siku ya tatu nitakamilisha kazi yangu. 33 Sina budi kuendelea na safari yangu leo, kesho na kesho kutwa, kwa maana haiwezekani nabii kufa mahali pengine isipokuwa Yerusalemu.
34 “Ewe Yerusalemu, Yerusalemu, wewe uwauaye manabii na kuwapiga mawe wale waliotumwa kwako! Mara ngapi nimetamani kuwa kusanya watoto wako pamoja kama kuku akusanyavyo vifaranga vyake chini ya mbawa zake, lakini hukuniruhusu! 35 Sasa nyumba yako inaachwa tupu. Ninakuambia, hutaniona tena mpaka wakati ule uta kaposema, ‘Amebarikiwa yeye ajaye katika jina la Bwana.”’