1Basi watoza kodi na wenye dhambi wakaja kwa Yesu ili wapate kumsikiliza. 2 Mafarisayo na walimu wa sheria wakaanza kunung’unika, “Huyu mtu anawakaribisha wenye dhambi na kula nao!” 3 Ndipo Yesu akawaambia mfano huu: 4 “Tuseme mmoja wenu ana kondoo mia moja halafu mmoja wao apotee. Si ana waacha wale tisini na tisa malishoni aende kumtafuta huyo aliyepotea mpaka ampate? 5 Akisha kumpata atambeba mabegani mwake na kwenda nyum bani. 6 Kisha atawaita marafiki na majirani na kuwaambia, ‘Fura hini pamoja nami; nimempata kondoo wangu aliyepotea.’ 7 Nawaam bieni, vivyo hivyo kutakuwa na furaha zaidi mbinguni kwa sababu ya mwenye dhambi mmoja atubuye na kuacha dhambi zake, kuliko ilivyo kwa wenye haki tisini na tisa ambao hawana haja ya kutubu.”
Shilingi Iliyopotea
8 “Au tuseme mwanamke ana shilingi kumi halafu apoteze moja. Si atawasha taa afagie nyumba na kutafuta kwa uangalifu mpaka aipate? 9 Na akisha kuipata atawaita marafiki zake na majirani na kuwaambia, ‘Furahini pamoja nami; nimeipata ile shilingi yangu iliyopotea!’ 10 Vivyo hivyo nawaambia, kuna furaha mbele ya mal aika wa Mungu kwa sababu ya mwenye dhambi mmoja atubuye na kuacha dhambi.”
Mwana Mpotevu
11 Yesu akaendelea kusema, “Kulikuwa na mtu aliyekuwa na watoto wawili wa kiume. 12 Yule mdogo akamwambia baba yake, ‘Baba, nipe urithi wangu.’ Basi huyo baba akagawanya mali yake kati yao.
13 “Baada ya muda mfupi yule mdogo akakusanya vitu vyote alivyokuwa navyo akaenda nchi ya mbali akaitapanya mali yake kwa maisha ya anasa. 14 Baada ya kutumia kila kitu alichokuwa nacho, kukawa na njaa kali katika nchi ile yote naye akawa hana cho chote. 15 Kwa hiyo akaomba kibarua kwa raia mmoja wa nchi hiyo aliyemtuma shambani kwake kulisha nguruwe. 16 Akatamani kujish ibisha kwa maganda waliyokuwa wanakula nguruwe, wala hakuna mtu aliyempa cho chote cha kula.
17 “Hatimaye akili zikamrudia, akasema, ‘Ni watumishi wan gapi walioajiriwa na baba yangu ambao wana chakula cha kuwatosha na kusaza nami hapa nakufa kwa njaa! 18 Nitaondoka nirudi kwa baba yangu nikamwambie, ‘Baba, nimetenda dhambi mbele ya Mungu na mbele yako. 19 Sistahili kuitwa mwanao tena; nifanye kama mmoja wa watumishi wako.’ 20 Basi akaondoka, akaenda kwa baba yake. Lakini alipokuwa bado yuko mbali, baba yake akamwona, moyo wake ukajawa na huruma. Akamkimbilia mwanae, akamkumbatia na kumbusu. 21 Yule mtoto akasema, ‘Baba, nimekosa mbele ya Mungu na mbele yako. Sistahili kuitwa mwanao tena.’ 22 Lakini baba yake aka waambia watumishi, ‘Leteni upesi kanzu iliyo bora mumvalishe. Pia mvalisheni pete na viatu. 23 Kisha mleteni yule ndama aliyenona mkamchinje; ili tule tusherehekee. 24 Kwa maana huyu mwanangu alikuwa amekufa, na sasa yu hai tena; alikuwa amepotea na sasa amepatikana.’ Basi wakaanza sherehe.
25 “Wakati huo kaka yake alikuwa shambani. Alipokuwa ana karibia nyumbani akasikia sauti ya nyimbo na ngoma. 26 Akamwita mmoja wa watumishi akamwuliza, ‘Kuna nini?’ 27 Akamwambia, ‘Mdogo wako amekuja, na baba yako amemchinja yule ndama aliyenona kwa sababu amempata mwanawe akiwa mzima.’ 28 Yule kaka akakasi rika, akakataa kuingia ndani. Basi baba yake akaenda nje akaanza kumbembeleza. 29 Lakini yeye akamjibu baba yake, ‘Angalia, miaka yote hii nimekutumikia na hata siku moja sijaacha kutii amri zako, lakini hujanipa hata mwana mbuzi ili nisherehekee na mara fiki zangu. 30 1Lakini huyu mwanao ambaye ametapanya mali yako kwa makahaba amerudi nyumbani nawe umemchinjia ndama aliyenona!’
31 “Baba yake akamwambia, ‘Mwanangu, umekuwa nami siku zote na vyote nilivyo navyo ni vyako. 32 Lakini ilitubidi tufurahi na kusherehekea kwa sababu mdogo wako alikuwa amekufa na sasa yu hai tena, alikuwa amepotea naye amepatikana.”’ Mfano Wa Meneja Mjanja