Kufufuka Kwa Kristo
1Na sasa napenda kuwakumbusha ndugu zangu kuhusu Injili niliyowahubiria, mkaipokea na ambayo ndio msimamo wenu. 2 Mnaoko lewa kwa Injili hii ikiwa mnashikilia imara neno nililowahubiria. Vinginevyo mtakuwa mmeamini bure. 3 Kwa maana niliyopokea ndio niliyowapa ninyi, nayo ni muhimu sana: kwamba Kristo alikufa kwa ajili ya dhambi zetu, kama ilivy oandikwa katika Maandiko. 4 Na kwamba alizikwa na kufufuka siku ya tatu, kama ilivyoandikwa katika Maandiko. 5 Na kwamba alimto kea Kefa, kisha akawatokea wale kumi na wawili. 6 Baadaye akawa tokea ndugu waamini zaidi ya mia tano kwa pamoja, na wengi wao wangali hai, ingawa wengine wameshakufa. 7 Kisha akamtokea Yakobo, na ndipo akawatokea mitume wote. 8 Na mwisho wa wote, akanitokea na mimi, ambaye ni kama nilizaliwa kwa hali isiyo ya kawaida.
9 Kwa maana mimi ni mdogo kuliko mitume wote, nisiyestahili kuitwa mtume kwa sababu nililitesa kanisa la Mungu. 10 Lakini kwa neema ya Mungu nimekuwa hivi nilivyo, na neema yake kwangu haikuwa bure. Badala yake, nilifanya kazi kuliko mitume wote, ingawaje haikuwa mimi bali ni neema ya Mungu iliyokuwa pamoja nami. 11 Hivyo basi, kama ilikuwa ni mimi au ni wao, haya ndio tuliyohubiri, na haya ndio mliyoamini.
Kufufuka Kwa Wafu
12 Basi kama tumehubiri ya kwamba Kristo alifufuliwa kutoka kwa wafu, inakuwaje baadhi yenu mnasema hakuna ufufuo wa wafu? 13 Lakini kama hakuna ufufuo wa wafu, basi Kristo hakufufuliwa. 14 Na ikiwa Kristo hakufufuliwa kutoka kwa wafu, mahubiri yetu ni bure na imani yenu ni bure. 15 Na zaidi ya hayo, tunaonekana kuwa tunamshuhudia Mungu uongo, kwa sababu tumeshuhudia kumhusu Mungu ya kuwa alimfufua Kristo kutoka kwa wafu. Na kumbe hakumfu fua, kama kweli wafu hawafufuliwi. 16 Kwa kuwa kama wafu hawa fufuliwi, basi hata Kristo hajafufuliwa. 17 Na ikiwa Kristo hajafufuliwa, imani yenu ni bure; nanyi bado mngali katika dhambi zenu. 18 Pia waamini wote waliokufa wakimwamini Yesu wamepotea. 19 Na kama imani yetu ndani ya Kristo ni kwa ajili ya maisha haya tu, basi sisi tunastahili kuhurumiwa kuliko watu wengine wo wote duniani. 20 Lakini ukweli ni kwamba Kristo amefufuliwa kutoka kwa wafu, matunda ya kwanza ya wote waliolala. 21 Kwa maana kama vile kifo kilivyokuja kwa njia ya mtu mmoja, vivyo hivyo, ufufuo wa wafu umekuja kwa njia ya mtu mmoja. 22 Kwa kuwa katika Adamu watu wote hufa, vivyo hivyo katika Kristo wote wata fanywa kuwa hai. 23 Lakini kila mmoja kwa mpango: Kristo ni mat unda ya kwanza ya ufufuo; kisha wale walio wake wakati atakapo kuja watafufuliwa. 24 Ndipo mwisho utafika, wakati ambao ataka bidhi Ufalme kwa Mungu Baba, akiisha angamiza kila mamlaka na uwezo na nguvu. 25 Kwa maana Kristo atamiliki mpaka Mungu ataka powaweka adui zake chini ya miguu yake. 26 Adui wa mwisho kuan gamizwa ni kifo. 27 “Kwa maana Mungu ameweka kila kitu chini ya utawala wake, chini ya miguu yake.” Ni wazi kwamba maneno haya, “Kila kitu kimewekwa chini ya utawala wake,” hayamjumlishi na Mungu ambaye ameweka vitu vyote chini ya Kristo. 28 Vitu vyote vikishawekwa chini ya utawala wake, ndipo naye Mwana atakuwa chini ya Mungu ambaye ameviweka vitu vyote chini yake, ili Mungu awe yote katika yote.
29 Vinginevyo, kwa nini watu wanabatizwa kwa niaba ya wafu? Kama wafu hawafufuliwi kamwe, mbona watu wanabatizwa kwa niaba yao? 30 Na kwa upande wetu kwa nini tunajitia hatarini kila wakati? 31 Nakufa kila siku, nasema kweli ndugu zangu, kama ninavyojivuna kwa ajili yenu katika Kristo Yesu, Bwana wetu. 32 Kama nilipigana na wanyama wakali huko Efeso kwa sababu za kibinadamu, nimepata faida gani? Kama wafu hawafufuliwi, basi, “Tule na kunywa, kwa maana kesho tutakufa.” 33 Mtu asiwadanga nye, “Ushirika na watu wabaya huharibu tabia njema.” 34 Pateni tena fahamu, muache kutenda dhambi. Kwa maana baadhi yenu hawam jui Mungu; nasema mambo haya ili muone aibu.
Ufufuo Wa Mwili
35 Lakini mtu anaweza kuuliza, “Wafu wanafufuliwaje? Wata kuwa na mwili wa namna gani?” 36 Wapumbavu ninyi! Mnachopanda hakiwi hai tena kama hakikufa. 37 Unapopanda, hupandi mwili unaoutegemea, bali unapanda mbegu, pengine mbegu ya ngano au ya nafaka nyingine. 38 Lakini Mungu huipa hiyo mbegu umbo kama alivyochagua mwenyewe, na kila aina ya mbegu ina umbo lake. 39 Kwa maana nyama zote si za aina moja. Binadamu wana nyama ya aina moja, wanyama wana aina nyingine na hali kadhalika ndege na samaki wana nyama tofauti. 40 Pia kuna miili ya mbinguni na miili ya duniani; lakini uzuri wa miili ya mbinguni ni wa aina moja na uzuri wa miili ya duniani ni wa aina nyingine. 41 Jua lina uzuri wa aina moja, mwezi nao una uzuri wake na nyota pia; na nyota hutofautiana na nyota nyingine kwa uzuri.
42 Ndivyo itakavyokuwa wakati wa ufufuo wa wafu. Mwili uliopandwa ni wakuharibika; utafufuliwa usioharibika; 43 unapandwa katika aibu, unafufuliwa katika utukufu; unapandwa katika udhaifu, unafufuliwa katika nguvu. 44 Unapandwa ukiwa mwili wa asili, unafufuliwa ukiwa mwili wa kiroho. Kama kuna mwili wa asili, basi kuna mwili wa kiroho pia. 45 Kwa hiyo imeandikwa, “Adamu wa kwanza akawa kiumbe hai,” Adamu wa mwisho akawa roho inayohuisha. 46 Lakini si yule wa kiroho aliyekuja kwanza; bali ni yule wa mwili, na kisha yule wa kiroho. 47 Mtu wa kwanza alitokana na mavumbi ya ardhini, mtu wa pili alitoka mbinguni. 48 Na kama alivyokuwa yule wa ardhini, ndivyo walivyo wale walio wa ardhini; na alivyo mtu wa mbinguni, ndivyo walivyo wale walio wa mbinguni. 49 Na kama tulivyochukua umbile la mtu wa ardhini, ndivyo tutakavyochukua umbile la yule mtu kutoka mbinguni. 50 Nawatangazia ndugu zangu kwamba nyama na damu haviwezi kurithi Ufalme wa Mungu, wala uharibifu hauwezi kurithi kutokuharibika.
51 Sikilizeni, nawaambia siri: sote hatutalala, lakini sote tutabadilishwa 52 ghafla, kufumba na kufumbua, tarumbeta ya mwisho itakapolia. Kwa kuwa tarumbeta italia, wafu watafufuliwa na miili isiyoharibika, nasi tutabadilishwa. 53 Kwa maana hali hii ya kuharibika lazima ivae kutokuharibika, na hali hii ya kufa lazima ivae hali ya kutokufa. 54 Kwa hiyo, wakati kuharibika kutakapovaa kutokuharibika, na mwili wa kufa utakapovaa hali ya kutokufa, ndipo lile neno lililoandikwa litakapotimia, “Kifo kimemezwa na ushindi .” 55 “Mauti, ushindi wako uko wapi? Na uchungu wako uko wapi?” 56 Uchungu wa kifo ni dhambi, na nguvu ya dhambi ni sheria. 57 Lakini, Mungu ashukuriwe! Yeye anatupa tia ushindi kwa njia ya Bwana wetu Yesu Kristo.
58 Kwa hiyo ndugu zangu, simameni imara. Msitikisike. Mzidi sana kujitoa kwa ajili ya kazi ya Bwana, kwa maana mnajua ya kuwa, juhudi yenu si bure katika Bwana.