1 Wakorintho 14

Karama Za Unabii Na Lugha

1Fuateni upendo na kutaka sana karama za Roho, hasa karama ya unabii. Kwa maana anayesema kwa lugha, hasemi na watu bali anasema na Mungu. Hakuna mtu anayemwelewa, kwani anasema siri katika Roho. Lakini anayetamka neno la Mungu anasema na watu akiwasaidia kupata nguvu, na kuwatia moyo na kuwafariji. Anayesema katika lugha anajijenga mwenyewe, lakini anayetoa neno la Mungu analijenga kanisa. Ningependa ninyi nyote mseme kwa lugha ngeni, lakini ningependa zaidi nyote muweze kutoa una bii kwa kuhubiri neno la Mungu. Kwa kuwa anayehubiri neno la Mungu ni mkuu kuliko anayesema kwa lugha, isipokuwa kama kuna mtu wa kutafsiri, ili kanisa zima liweze kusaidika.

Sasa ndugu zangu, kama nikija kwenu nikasema kwa lugha ngeni, nitapata faida gani kama sikuwaletea mafunuo au neno la maarifa au unabii au mafundisho? Hata vyombo vya muziki visivyo na uhai kama vile filimbi au kinubi, visipotumiwa kwa mpangilio wa sauti, ni nani atakayeweza kufahamu ni wimbo gani unaimbwa? Na kama baragumu ikitoa sauti isiyoeleweka, ni nani atakayej iandaa kwenda vitani? Hali kadhalika na ninyi. Kama mkisema kwa lugha isiyoeleweka, watu watafahamuje mnachosema? Kwa maana mta kuwa mnasema hewani.

10 Bila shaka ziko lugha nyingi ulimwenguni, na hakuna lugha isiyo na maana. 11 Lakini ikiwa sielewi maana ya lugha inayotu mika nitakuwa mgeni kwa yule anayezungumza, naye atakuwa mgeni kwangu. 12 Hali kadhalika na ninyi. Kwa kuwa mna hamu ya kuwa na karama za Roho, wekeni bidii katika karama zinazolijenga kanisa.

13 Kwa hiyo anayesema kwa lugha aombe kupewa kipawa cha kutafsiri lugha. 14 Kwa maana nikiomba kwa lugha roho yangu inaomba, lakini akili yangu haishiriki. 15 Nifanyeje basi? Nitaomba kwa roho na nitaomba kwa akili yangu pia. Nitaimba kwa roho na nitaimba kwa akili yangu pia. 16 Vinginevyo, kama mkim sifu Mungu katika roho, mtu mwingine ambaye anashiriki katika mkutano wenu na ambaye haelewi atawezaje kusema, ‘Amina 17 Mnaweza kuwa mnatoa shukrani kweli, lakini huyo mtu mwingine hajengeki. 18 Namshukuru Mungu kwamba mimi ninasema kwa lugha kuliko ninyi nyote. 19 Lakini hata hivyo, nikiwa kanisani, ni afadhali niseme maneno matano ya kueleweka ili niwafundishe wengine kuliko kusema maneno elfu kumi kwa lugha.

20 Ndugu zangu, msiwe kama watoto wadogo katika kufikiri kwenu. Kuhusu uovu muwe kama watoto wachanga, lakini katika kufi kiri, muwe watu wazima. 21 Imeandikwa katika sheria, “Kwa njia ya watu wenye lugha ngeni na kupitia midomo ya wageni, nitazun gumza na hawa watu, lakini hata hivyo hawatanisikiliza, asema Bwana.”

Bwana.”

22 Kwa hiyo lugha ngeni ni ishara kwa watu wasioamini, na si kwa ajili ya waamini. Lakini unabii ni kwa ajili ya waamini, na si kwa ajili ya wasioamini. 23 Kwa hiyo kama kanisa lote likiku tana na wote wakasema kwa lugha, kisha akaingia mgeni au asi yeamini, je, si atadhani wote mna kichaa? 24 Lakini ikiwa wote wanahubiri unabii wa neno la Mungu, na akaingia mtu asiyeamini au mgeni, atakuwa na uhakika kuwa yeye ni mwenye dhambi kutokana na yale yanayosemwa na wote, 25 na siri zote za moyo wake zitawekwa wazi. Kwa hiyo ataanguka chini na kumwabudu Mungu akisema, “Kweli Mungu yupo pamoja nanyi!”

Kumwabudu Mungu Kwa Mpango

26 Tuseme nini basi ndugu zangu? Mnapokutana pamoja, kila mtu ana wimbo, au neno la mafundisho, mafunuo, ujumbe katika lugha ngeni, au tafsiri ya lugha. Kila jambo lifanyike kwa sha baha ya kujengana. 27 Kama mtu akisema kwa lugha, basi waseme si zaidi ya wawili au watatu, mmoja baada ya mwingine; na lazima awepo mtu wa kutafsiri. 28 Lakini kama hakuna mtu wa kutafsiri, huyo mzungumzaji akae kimya kanisani na aseme na nafsi yake mwe nyewe na Mungu. 29 Watu wawili au watatu walio na unabii wa neno la Mungu waseme, na wengine wapime kwa makini yale yanayosemwa. 30 Kama mmoja wa wale waliokaa akipata mafunuo kutoka kwa Mungu, anayezungumza aache kusema. 31 Kwa maana wote mnaweza kutoa una bii, mtu mmoja mmoja, ili kila mtu anayesikiliza apate kufund ishwa na kutiwa moyo. 32 Roho za unabii ziko chini ya mamlaka ya manabii. 33 Kwa maana Mungu si Mungu wa machafuko bali ni Mungu wa amani. Kama ilivyo desturi katika mikutano ya watu wa Mungu,

34 wanawake wanapaswa kukaa kimya kanisani. Hawaruhusiwi kusema, bali wanyenyekee kama sheria inavyosema. 35 Kama wakitaka kuu liza kitu, wawaulize waume zao nyumbani. Kwa maana ni aibu kwa mwanamke kuzungumza kanisani. 36 Je, mnadhani neno la Mungu lil itoka kwenu? Au ni ninyi tu ambao neno la Mungu limewafikia?

37 Kama mtu anadhani yeye ni nabii, au ana karama za kiroho, basi akubali kwamba haya ninayoandika ni amri kutoka kwa Bwana. 38 Kama mtu asipotambua haya hatatambuliwa. 39 Kwa hiyo ndugu zangu, takeni sana kutoa unabii na msikataze watu kusema kwa lugha. 40 Lakini kila kitu kitendeke kwa utaratibu mzuri.