1 Wakorintho 13

Upendo

1Kama ningekuwa na uwezo wa kusema kwa lugha za wanadamu na za malaika, kama sina upendo, nimekuwa kama kelele ya kengele au toazi. Na kama nina uwezo wa unabii, na kuelewa siri zote na maarifa yote; na hata kama nina imani kiasi cha kuweza kuhamisha milima, kama sina upendo, mimi si kitu. Kama nikitoa mali yote niliyo nayo, na kama nikitoa mwili wangu uchomwe moto, kama sina upendo, hainifaidii kitu.

Upendo huvumilia, upendo hufadhili; upendo hauna wivu au majivuno.

Upendo hauna kiburi na haukosi kuwa na adabu. Upendo hau tafuti kujipendeza nafsi; haukasiriki upesi, hauweki orodha ya mabaya. Upendo haufurahii mabaya, bali hufurahia kweli. Upendo huvumilia yote, huamini yote, hutumaini yote, hustahim ili yote.

Upendo hauna mwisho. Lakini penye unabii, utakoma; zikiwepo lugha zitakoma; yakiwepo maarifa yatakwisha. Kwa maana tunafa hamu kwa sehemu na tunafanya unabii kwa sehemu. 10 Lakini uka milifu utakapokuja, yale yasiyo kamili yatakwisha. 11 Nilipokuwa mtoto mdogo, nilisema kama mtoto mdogo, niliwaza kama mtoto mdogo, nilifikiri kama mtoto mdogo. Nilipokuwa mtu mzima niliacha mambo ya kitoto. 12 Kwa maana sasa tunaona sura kama ya kwenye kioo, lakini wakati huo tutaona uso kwa uso. Sasa nafahamu kwa sehemu, wakati huo nitafahamu kikamilifu, kama vile ninavyo faha mika kikamilifu.

13 Basi sasa, mambo matatu yanadumu: imani, tumaini na upendo. Lakini lililo kuu kati ya haya ni upendo.