Utaratibu Wa Kuabudu
1Niigeni mimi, kama mimi ninavyomuiga Kristo. 2 Ninawasifu kwa sababu mnanikumbuka katika kila jambo na kwa kuwa mnashika mafundisho niliyowakabidhi. 3 Lakini napenda muelewe kwamba Kristo ni kichwa cha kila mwanamume, kama vile mume alivyo kichwa cha mkewe, na Mungu ni kichwa cha Kristo. 4 Kwa hiyo mwanamume anayeomba au kutoa unabii akiwa amefunika kichwa chake, anaaib isha kichwa chake. 5 Na mwanamke anayeomba au kutoa unabii pasipo kufunika kichwa chake, anaaibisha kichwa chake, ni sawa kama ame nyoa nywele zote kichwani. 6 Kama mwanamke hataki kufunika kichwa chake, nywele zake zinyolewe; na kama ni aibu kwa mwanamke kunyoa kichwa chake, au kukata nywele zake, basi afunike kichwa chake. 7 Mwanamume asifunike kichwa chake kwa sababu yeye ni mfano na utukufu wa Mungu. Lakini mwanamke ni utukufu wa mwanamume. 8 Kwa maana mwanamume hakuumbwa kutoka kwa mwanamke, bali mwanamke ame toka kwa mwanamume. 9 Wala mwanamume hakuumbwa kwa ajili ya mwa namke, bali mwanamke aliumbwa kwa ajili ya mwanamume. 10 Hii ndio sababu inampasa mwanamke afunike kichwa chake na kwa ajili ya malaika. 11 Lakini katika Bwana mwanamke hawezi kufanya lo lote pasipo mwanamume, wala mwanamume hawezi kufanya lo lote pasipo mwanamke. 12 Kwa maana kama vile mwanamke alivyoumbwa kutoka kwa mwanamume, vivyo hivyo sasa mwanamume anazaliwa na mwanamke. Lakini vitu vyote vinatoka kwa Mungu.
13 Amueni wenyewe, je, ni sawa kwa mwanamke kumwomba Mungu akiwa hakufunika kichwa chake? 14 Je, maumbile ya asili hayatu fundishi kuwa ni aibu kwa mwanamume kuwa na nywele ndefu? 15 Lakini mwanamke akiwa na nywele ndefu ni sifa kwake. Kwa maana mwanamke amepewa nywele ndefu za kumfunika. 16 Kama mtu anataka kubishana juu ya jambo hili, sisi wala makanisa ya Mungu hatutambui desturi nyingine.
Chakula Cha Bwana
17 Kuhusu maagizo yafuatayo, siwezi kuwasifu kwa sababu mikutano yenu inaleta madhara zaidi kuliko mema. 18 Kwanza, mna pokutana kama kanisa nasikia kwamba kuna mgawanyiko kati yenu, na kwa kiasi fulani naamini ndivyo ilivyo. 19 Bila shaka lazima pawe na tofauti miongoni mwenu ili wale walio wa kweli waweze kuonekana.
20 Mnapokutana pamoja hamli chakula cha Bwana. 21 Kwa kuwa mnapokula, kila mmoja wenu anaendelea na chakula chake bila kun goja wengine, na mmoja anabaki na njaa wakati mwingine analewa. 22 Je, hamwezi mkala na kunywa kwenye nyumba zenu? Au mnadharau kanisa la Mungu na kuwafedhehesha wasio na kitu? Niwaambie nini?
Je, niwasifu juu ya jambo hili? La, sitawasifu!
23 Kwa maana mimi nilipokea kutoka kwa Bwana yale maagizo niliyowapa ninyi, kwamba Bwana Yesu, usiku ule aliposalitiwa, alitwaa mkate, 24 naye akiisha kushukuru , akaumega, akasema, “Huu ndio mwili wangu, ambao ni kwa ajili yenu. Fanyeni hivi kwa ukumbusho wangu.” 25 Na vivi hivi baada ya kula akakitwaa kikombe, akisema, “Hiki kikombe ni agano jipya katika damu yangu. Fanyeni hivi kila mnywapo kwa ukumbusho wangu.” 26 Maana kila mlapo mkate huu na kunywa katika kikombe hiki, mnatangaza kifo cha Bwana mpaka atakapokuja.
27 Kwa hiyo mtu ye yote anayekula mkate huo au kukinywea kikombe hicho isivyostahili, atakuwa na hatia juu ya mwili na damu ya Bwana. 28 Kila mtu ajichunguze mwenyewe, na ndipo aule mkate na kukinywea kikombe. 29 Kwa maana mtu ye yote alaye na kunywa pasipo kutambua mwili wa Bwana, anajiletea hukumu juu yake mwenyewe. 30 Na hii ndio sababu wengi wenu ni wagonjwa na dhaifu, na wengine wamekufa. 31 Lakini kama tungejichunguza wenyewe tusingalihukumiwa. 32 Tunapohukumiwa na Bwana, anaturudi ili tusije tukahukumiwa pamoja na ulimwengu. 33 Kwa hiyo, ndugu zangu, mnapokutana pamoja kula, ngojaneni. 34 Kama mtu akiwa na njaa, ale nyumbani ili mnapokutana pamoja msije mkahukumiwa. Na nitakapokuja nitawapa maagizo zaidi.