Yesu Alisha Watu Elfu Nne
1Muda si mrefu baadaye, umati mkubwa wa watu ulikusanyika tena. Kwa kuwa walikuwa hawana chakula, Yesu akawaita wanafunzi wake akawaambia, 2 “Ninawaonea huruma hawa watu. Wamekuwa nami kwa muda wa siku tatu sasa na hawana chakula. 3 Nikiwaruhusu waende bila kula, watazimia njiani na baadhi yao wametoka mbali.”
4 Wanafunzi wake wakamjibu, “Lakini hapa nyikani tutapata wapi chakula cha kutosha kuwalisha?”
5 Yesu akawauliza, “Mna mikate mingapi?” Wakajibu, “Saba.”
6 Akawaambia watu wakae chini. Kisha akaichukua ile mikate saba na baada ya kushukuru akaimega, akawapa wanafunzi wake wawa gawie watu. Wanafunzi wake wakafanya hivyo. 7 Walikuwa pia na visamaki vichache, Yesu akavibariki, akawaamuru wanafunzi wake wawagawie watu. 8 Watu walikula wakatosheka na baadaye wanafunzi wakakusanya vipande vilivyosalia wakajaza vikapu saba. 9 Na watu waliokula walikuwa wapata elfu nne. Baada ya kuwaaga, 10 aliin gia kwenye mashua pamoja na wanafunzi wake akaenda sehemu za Dal manutha.
11 Mafarisayo wakaja, wakaanza kumhoji Yesu. Ili kumtega, wakamwomba awaonyeshe ishara kutoka mbinguni. 12 Akahuzunika moyoni, akawaambia, “Kwa nini kizazi hiki kinataka ishara? Nawaambieni kweli, hakitapewa ishara yo yote.” 13 Kisha aka waacha, akarudi kwenye mashua, akavuka hadi ng’ambo ya pili.
Chachu Ya Mafarisayo Na Ya Herode
14 Wanafunzi walikuwa wamesahau kuleta mikate ya kutosha. Walikuwa na mkate mmoja tu kwenye mashua. 15 Yesu akawaonya: “Jihadharini na chachu ya Mafarisayo na ya Herode.”
16 Wakaanza kujadiliana wao kwa wao wakasema,“Anasema hivi kwa kuwa hatukuleta mikate.”
17 Yesu alifahamu majadiliano yao, akawauliza: “Mbona mna zungumzia kuhusu kutokuwa na mikate? Bado hamtambui wala kuelewa? Je, mbona mioyo yenu ni migumu kiasi hicho? 18 Mbona mna macho lakini mnashindwa kuona, na masikio lakini mnashindwa kusikia? Je hamkumbuki? 19 Nilipoimega mikate mitano kuwalisha watu elfu tano, mlikusanya mabaki vikapu vingapi?” Wakamjibu, “Kumi na viwili.” 20 “Na nilipomega mikate saba kuwalisha watu elfu nne mlikusanya mabaki vikapu vingapi?” Wakamjibu, “Saba.” 21 Aka wauliza, “Je, bado tu hamwelewi?”
Yesu Amponya Kipofu Huko Bethsaida
22 Wakafika Bethsaida na baadhi ya watu wakamleta kipofu mmoja wakamsihi Yesu amguse. 23 Yesu akamshika mkono huyo kipofu akampeleka nje ya kijiji. Baada ya kuyatemea mate macho ya yule kipofu na kumwekea mikono, Yesu akamwuliza, “Unaona cho chote?”
24 Yule kipofu akaangalia, akasema, “Ninaona watu; wanaonekana kama miti ikitembea.”
25 Yesu akamwekea tena mikono machoni. Ndipo akaona vizuri. Macho yake yakapona kabisa akaweza kuona kila kitu sawa sawa.
26 Yesu akamruhusu aende nyumbani kwake akisema, “Hata kijijini usipitie.”
27 Yesu na wanafunzi wake wakaondoka kwenda katika vijiji vya Kaisaria Filipi. Walipokuwa njiani Yesu akawauliza, “Watu husema mimi ni nani?”
28 Wakamjibu, “ Baadhi husema wewe ni Yohana Mbatizaji; wengine husema ni Eliya na wengine husema wewe ni mmojawapo wa manabii.”
29 Akawauliza, “Na ninyi je, mnasema mimi ni nani?” Petro akajibu, ‘ ‘Wewe ndiye Kristo.”
30 Akawaonya wasim wambie mtu ye yote habari zake.
Yesu Azungumza Juu Ya Kifo Chake
31 Akaanza kuwafundisha wanafunzi wake kuwa yeye, Mwana wa Adamu, atapata mateso mengi na kukataliwa na wazee, na makuhani wakuu na walimu wa sheria; na kwamba atauawa na baada ya siku tatu atafufuka. 32 Aliyasema haya wazi wazi. Ndipo Petro akam chukua kando akaanza kumkemea. 33 Lakini Yesu alipogeuka na kuwatazama wanafunzi wake alimkaripia Petro akamwambia, “Ondoka mbele yangu, shetani! Mawazo yako hayako upande wa Mungu bali upande wa wanadamu.”
34 Ndipo akawaita wale watu pamoja na wanafunzi wake aka waambia, “Mtu ye yote akitaka kunifuata, ni lazima ajikane mwe nyewe, auchukue msalaba wake, anifuate. 35 Kwa maana mtu ye yote aipotezaye nafsi yake kwa ajili yangu na kwa ajili ya kuitangaza Habari Njema, ataiokoa. 36 Mtu atafaidi nini kama atapata ulimwengu wote lakini akayaangamiza maisha yake? 37 Au mtu atatoa nini apate tena maisha yake? 38 Mtu ye yote atakayenionea aibu mimi na maneno yangu katika kizazi hiki kiovu na kisichomjali Mungu, na mimi, Mwana wa Adamu, nitamwonea aibu wakati nitakapokuja katika utu kufu wa Baba yangu na malaika watakatifu.”