Mfano Wa Shamba La Mizabibu Na Wakulima Waovu
1Yesu alianza kusema nao kwa kutumia mifano: “Mtu mmoja alipanda shamba la mizabibu; akalizungushia uzio, akachimba kisima cha kutengenezea divai na akajenga mnara. Akalikodisha shamba hilo kwa wakulima fulani kisha akasafiri kwenda nchi nyingine. 2 Wakati wa mavuno ulipofika, mwenye shamba alimtuma mtumishi wake kwa hao wakulima kuchukua sehemu yake ya mavuno. 3 Lakini wale wakulima walimkamata yule mtumishi, wakampiga, wakamfukuza mikono mitupu. 4 Yule mwenye shamba akamtuma mtum ishi mwingine. Wale wakulima wakampiga kichwani, na kumfanyia mambo ya aibu. 5 Akapeleka mtumishi mwingine tena. Huyu, wakam wua. Akapeleka wengine zaidi, baadhi yao wakawapiga na wengine wakawaua. 6 Mwenye shamba akawa amebakiwa na mtu mmoja tu ambaye angeweza kumtuma. Huyu alikuwa mwanae aliyempenda sana. Hatimaye akaamua kumtuma akisema, ‘Bila shaka watamheshimu mwanangu.’ 7 Lakini wale wakulima wakashauriana, ‘Huyu mwanae ndiye mrithi. Tumwue na urithi utakuwa wetu.’ 8 Wakamchukua, wakamwua, wakam tupa nje ya shamba. 9 Mnadhani yule mwenye shamba atafanya nini? Atakuja, awaue hao wakulima kisha alikodishe shamba lake kwa wak ulima wengine. 10 Hamjasoma Maandiko haya? ‘Lile jiwe waliloli kataa wajenzi limekuwa jiwe kuu la msingi. 11 Jambo hili limefa nywa na Bwana, nalo ni la ajabu kwetu.’ ”
12 Viongozi wa Wayahudi wakatafuta njia ya kumkamata Yesu kwa sababu walifahamu kuwa mfano huo uliwasema wao. Lakini wali waogopa watu. Kwa hiyo walimwacha wakaondoka, wakaenda zao. Kuhusu Kulipa Kodi
13 Mafarisayo kadhaa na Maherode walitumwa kuja kumtega Yesu katika maneno yake. 14 Wakamjia, wakamwambia, “Mwalimu, tunafahamu kuwa wewe huwaambia watu ukweli pasipo kujali watu watasema nini. Wala hujali cheo cha mtu bali unafundisha njia ya Mungu kwa kweli. Je, ni halali au si halali kulipa kodi kwa Kais ari? 15 Tulipe kodi hiyo au tusilipe?” Lakini Yesu alitambua hila yao. Akawaambia, “Mbona mnajaribu kunitega? Nileteeni sar afu niione.” 16 Wakamletea. Akawauliza, “Hii ni picha ya nani na hii ni sahihi ya nani?” Wakamjibu, “Ni ya Kaisari.”
17 Basi Yesu akawaambia, “Mpeni Kaisari vilivyo vya Kais ari na vya Mungu mpeni Mungu.” Jibu hili liliwastaajabisha sana.
Kuhusu Ufufuo wa Wafu
18 Kisha Masadukayo, ambao wanaamini kuwa hakuna ufufuo wa wafu, walimjia Yesu wakamwuliza swali wakisema, 19 “Mwalimu, Musa alituandikia agizo kuwa kama mtu akifariki akamwacha mkewe bila mtoto, basi ndugu yake hana budi kumwoa mjane huyo ili amzalie ndugu yake watoto. 20 Sasa walikuwapo ndugu saba. Yule wa kwanza akaoa akafariki pasipo kupata mtoto. 21 Wapili akam woa yule mjane, naye akafariki bila kuacha mtoto. Ikawa hivyo hata kwa yule wa tatu. 22 Kwa kifupi, ndugu wote saba walimwoa huyo mjane lakini wote hawakuzaa naye. Hatimaye yule mama naye akafariki. 23 Sasa tuambie, wakati wa ufufuo, watakapofufuka wote, huyo mama aliyeolewa na ndugu wote saba, atakuwa mke wa nani?”
24 Yesu akawajibu, “Mmekosea kabisa kwa maana hamfahamu Maandiko wala uweza wa Mungu.” 25 Wafu watakapofufuka, hawataoa wala kuolewa; watakuwa kama malaika wa mbinguni . 26 Na kuhusu ufufuo wa wafu: hamjasoma katika kitabu cha Musa, sehemu ile inayoelezea jinsi Mungu alivyozungumza na Musa kutoka katika kichaka akisema, ‘Mimi, ni Mungu wa Ibrahimu na Mungu wa Isaka na Mungu wa Yakobo’? 27 Mungu si Mungu wa wafu bali ni Mungu wa walio hai. Kwa hiyo mmekosea kabisa.”
Amri Iliyo Kuu
28 Mwalimu mmoja wa sheria aliwasikiliza wakijadiliana. Alipoona kwamba Yesu amewajibu vizuri, naye akamwuliza, “Katika amri zote, ni ipi iliyo kuu?” 29 Yesu akamjibu, “Iliyo kuu ni hii, ‘Sikiliza Israeli, Bwana Mungu wetu ndiye Bwana pekee. 30 Nawe mpende Bwana Mungu wako kwa moyo wako wote, kwa roho yako yote, kwa akili zako zote na kwa nguvu zako zote.’ 31 Na sheria ya pili kwa ukuu ndio hii: ‘Mpende jirani yako kama nafsi yako.’ Hakuna amri nyingine iliyo kuu kuliko hizi.”
32 Yule mwalimu wa sheria akamwambia Yesu, “Mwalimu, ume jibu vyema. Ulivyosema ni kweli kabisa, Mungu ni mmoja wala hakuna mwingine ila yeye. 33 Na kumpenda Mungu kwa moyo wote na kwa akili zote na kwa nguvu zote; na kumpenda jirani kama mtu anavyojipenda ni bora zaidi kuliko kutoa sadaka ya kuteketezwa.”
34 Yesu alipoona jinsi alivyojibu kwa busara, akamwambia, “Wewe hauko mbali na Ufalme wa Mungu.” Tangu wakati huo, hakuna mtu aliyethubutu kumwuliza maswali zaidi.
Kuhusu Mwana Wa Daudi
35 Yesu alipokuwa akifundisha Hekaluni, aliuliza, “Mbona walimu wa sheria wanasema kwamba Kristo ni Mwana wa Daudi? 36 Kwa maana Daudi akiongozwa na Roho Mtakatifu alisema, ‘Bwana alimwambia Bwana wangu: keti mkono wangu wa kulia mpaka niwashi nde na kuwafedhehesha maadui zako chini ya miguu yako.’ 37 Ikiwa Daudi mwenyewe anamwita Bwana, yawezekanaje tena Kristo akawa mwanawe?” Watu wote wakamsikiliza kwa furaha.
Yesu Awatahadharisha Watu Kuhusu Walimu Wa Shera
38 Katika mafundisho yake, Yesu alisema, “Jihadharini na walimu wa sheria. Wao hupenda kutembea wakiwa wamevaa mavazi yao rasmi na kusalimiwa kwa heshima masokoni. 39 Pia wao hupenda kukaa viti vya mbele katika masinagogi na kupewa nafasi za heshi ma katika sherehe. 40 Hao hao ndio huwadhulumu wajane nyumba zao na ili waonekane kuwa wema wanasali sala ndefu. Mungu ata waadhibu vikali zaidi.”
Sadaka Ya Mjane
41 Kisha Yesu akaketi karibu na sehemu ya kutolea sadaka Hekaluni akawaangalia watu walivyokuwa wakiweka sadaka zao kwenye chombo cha sadaka. Matajiri wengi waliweka humo kiasi kikubwa cha fedha. 42 Lakini mjane mmoja fukara, alikuja akaweka sarafu mbili zenye thamani ya senti kumi.
43 Yesu akawaita wanafunzi wake akawaambia, “Ninawaambia hakika, huyu mjane ametoa zaidi kuliko wote! 44 Wengine wote wametoa kutokana na ziada ya mali zao; lakini huyu mama ingawa ni fukara, ameweka kila kitu alichokuwa nacho, hata na kile alicho hitaji kwa ajili ya riziki yake.”