Marko 6

Watu Wa Nazareti Wamkataa Yesu

1 Yesu akaondoka mahali hapo, akaenda mji wa kwao, akifu atana na wanafunzi wake. Ilipofika siku ya sabato, alianza ku fundisha katika sinagogi na wengi waliomsikia walishangaa. Wakasema, “Mtu huyu ameyapata wapi mambo haya? Amepataje kuwa na hekima ya namna hii? Amepata wapi uwezo wa kutenda miujiza ya namna hii? Huyu si yule seremala mtoto wa Mariamu? Na ndugu zake si Yakobo, Yose, Yuda na Simoni? Dada zake si tuko nao hapa?” Basi hawakumwamini.

Yesu akawaambia, ‘ ‘Nabii huheshimiwa kila mahali isipokuwa katika mji wake na kati ya jamaa na ndugu zake.” Hakufanya miujiza yo yote huko isipokuwa kuwagusa wagonjwa wachache na kuwaponya. Alishangazwa sana na jinsi walivyokuwa hawana imani.

Yesu Awatuma Wanafunzi Wake Kumi Na Wawili

Akawaita wale wanafunzi kumi na wawili akaanza kuwatuma wawili wawili na akawapa mamlaka juu ya pepo wachafu.

Akawaagiza wasichukue cho chote safarini isipokuwa fimbo tu. Wasichukue mkate, wala mfuko, wala fedha. Ila wavae viatu lakini wasichukue nguo ya kubadili. 10 Pia akawaambia, “Mkiin gia nyumba yo yote, kaeni hapo hapo hadi mtakapoondoka katika mji huo. 11 Na mahali po pote ambapo hamtakaribishwa wala kusikili zwa, mtakapoondoka hapo, kung’uteni mavumbi yaliyoko miguuni mwenu, kama onyo lenu kwao.”

12 Kwa hiyo wakatoka, wakaenda wakihubiri kwamba watu wat ubu, waache dhambi. 13 Wakawatoa watu wengi pepo, wakawapaka mafuta wagonjwa wengi, wakawaponya.

Kifo Cha Yohana Mbatizaji

14 Mfalme Herode akapata habari hizi, kwa maana jina la Yesu lilikuwa limefahamika kila mahali. Watu wengine walikuwa wakisema, “Yohana Mbatizaji amefufuka kutoka kwa wafu ndiyo maana uwezo wa kutenda miujiza unafanya kazi ndani yake!” 15 Wengine walisema, “Huyo ni Eliya!” Na wengine wakasema, “Ni nabii kama wale manabii wa zamani.” 16 Lakini Herode ali posikia habari hizi alisema, “Huyo ni Yohana Mbatizaji niliyem kata kichwa; amefufuka!” 17 Kwa maana Herode alikuwa ameagiza kwamba Yohana Mbatizaji akamatwe, awekwe gerezani. Alifanya hivi kwa sababu ya Herodia, mke wa kaka yake, Filipo, ambaye alikuwa amemwoa. 18 Yohana alikuwa amemwambia Herode, “Si halali wewe kumwoa mke wa kaka yako.” 19 Kwa hiyo Herodia alikuwa amemwe kea kinyongo Yohana akataka kumwua. Lakini hakupata nafasi, 20 kwa sababu Herode alimwogopa Yohana ambaye alifahamu kuwa ni mtu mwenye haki na mtakatifu, akawa anamlinda. Ingawa Herode alifadhaika sana kila alipomsikiliza Yohana, bado alipenda kumsi kiliza.

21 Baadaye Herodia alipata nafasi aliyokuwa akiitafuta. Wakati wa sikukuu ya kuzaliwa kwa mfalme Herode, mfalme alifanya sherehe kubwa, akawaalika viongozi wakuu wa ikulu, makamanda wa jeshi na watu mashuhuri wa Galilaya. 22 Binti yake Herodia akaja akacheza, akamfurahisha Herode pamoja na wageni wake. Mfalme Her ode akamwambia yule binti, “Niombe kitu cho chote utakacho, nami nitakupa.” 23 Akala kiapo akamwambia, “Cho chote utakachoomba, hata ikiwa ni nusu ya ufalme wangu, nitakupa.”

24 Yule binti akaenda akamwuliza mama yake, “Niombe nini?” Mama yake akajibu, “Mwombe kichwa cha Yohana Mbati zaji.” 25 Yule binti akarudi haraka kwa mfalme akamwambia, “Nataka unipe sasa hivi kichwa cha Yohana Mbatizaji kwenye sinia .” 26 Mfalme akajuta sana, lakini hakuweza kumkatalia kwa kuwa alikuwa ameapa mbele ya wageni wake, na hakupenda kuvunja ahadi yake. 27 Kwa hiyo Herode akamtuma mmojawapo wa walinzi wake mara moja akamwagiza alete kichwa cha Yohana. 28 Yule mlinzi akaenda gerezani akamkata Yohana kichwa kisha akakileta kwenye sinia akampa yule binti; naye akampatia mama yake.

29 Wanafunzi wa Yohana walipopata habari hizi, walikuja wakauchukua mwili wake, wakauzika kaburini.

Yesu Awalisha Watu Elfu Tano

30 Wale wanafunzi kumi na wawili waliporudi, walimweleza Yesu mambo yote waliyofanya na kufundisha. 31 Kwa kuwa watu wengi mno walikuwa wakija na kutoka, hata wakakosa nafasi ya kula, Yesu aliwaambia wanafunzi wake, “Twendeni peke yetu mahali pa faragha, mpate kupumzika.” 32 Basi wakaondoka kwa mashua peke yao wakaenda mahali pasipo na watu.

33 Lakini watu waliowaona wakiondoka, wakawatambua. Wakawa tangulia mbio kwa miguu kutoka miji yote wakielekea kule waliko kuwa wakienda. Wakawahi kufika.

34 Yesu alipofika nchi kavu na kuuona huo umati wa watu, aliwaonea huruma kwa maana walikuwa kama kondoo wasiokuwa na mchungaji. Kwa hiyo akaanza kuwafundisha mambo mengi.

35 Hata saa za mchana zilipoanza kupita, wanafunzi wake wakamwendea wakamwambia, “Mahali hapa ni nyikani, na saa zimek wenda. 36 Waruhusu watu waondoke wakajinunulie chakula kwenye mashamba na vijiji vya jirani.”

37 Lakini Yesu akawajibu, “Wapeni ninyi chakula.” Wakam wambia, “Tunahitaji fedha nyingi sana, kununulia mikate ya kutosha kulisha watu wote hawa.”

38 Akawauliza, “Mna mikate mingapi? Nendeni mkaangalie.” Waliporudi wakamwambia, “Ipo mikate mitano na samaki wawili.”

39 Kisha Yesu akawaamuru wawaketishe watu makundi makundi kwenye nyasi, 40 nao wakaketi kwenye makundi ya watu mia mia na hamsini hamsini. 41 Yesu akaichukua ile mikate mitano na wale samaki wawili akatazama mbinguni, akashukuru, kisha akaimega ile mikate akawapa wanafunzi wake wawagawie wale watu. Pia akawagawia wote wale samaki wawili. 42 Watu wote wakala, wakashiba. 43 Wanafunzi wakakusanya vipande vilivyosalia wakajaza vikapu kumi na viwili. 44 Idadi ya wanaume waliokula walikuwa elfu tano.

Yesu Atembea Juu Ya Maji

45 Wakati huo huo Yesu akawaamuru wanafunzi wake waingie kwenye mashua watangulie kwenda Bethsaida, wakati yeye anawaaga watu. 46 Baada ya kuwaaga wale watu, akaenda mlimani kusali. 47 Ilipofika jioni, ile mashua ilikuwa imeshafika katikati ya ziwa na Yesu alikuwa peke yake nchi kavu. 48 Aliwaona wanafunzi wake wakihangaika na kuvuta makasia kwa nguvu kwa sababu upepo ulikuwa ukielekea walikotoka. Karibu na mapambazuko, Yesu aka waendea wanafunzi wake akitembea juu ya maji. Alikuwa karibu kuwapita, 49 lakini walipomwona akitembea juu ya maji, walid hani ni mzimu, wakapiga yowe, 50 kwa maana wote walimwona wakaogopa. Lakini mara Yesu akasema nao, “Tulieni! Ni mimi, msi ogope!” 51 Akapanda kwenye mashua yao na ule upepo ukakoma! Wakashangaa kabisa. 52 Walikuwa bado hawajaelewa hata maana ya u le muujiza wa mikate. Walikuwa bado hawajafunuliwa akilini mwao.

53 Walipokwisha kuvuka, walifika katika wilaya ya Gene zareti, wakatia nanga. 54 Waliposhuka kutoka katika mashua yao, watu walimtambua Yesu mara moja, 55 wakapita vijiji vyote haraka haraka, wakawabeba wagonjwa kwenye machela wakamfuata mahali po pote waliposikia kuwa yupo. 56 Na kila mahali Yesu alipokwenda, ikiwa ni vijijini, mijini na mashambani, watu waliwaweka wagonjwa wao masokoni wakamwomba awaruhusu hao wagonjwa angalao waguse pindo la vazi lake. Na wote waliomgusa, waliponywa.