Marko 11

Yesu Aingia Yerusalemu

1Walipokaribia Yerusalemu, wakiwa katika miji ya Bethfage na Bethania katika mlima wa Mizeituni, Yesu aliwatuma wanafunzi wake wawili watangulie. Akawaagiza, “Nendeni kwenye kijiji kile kilichoko mbele yenu. Mtakapokuwa mnaingia kijijini, mtam wona mwana punda amefungwa, ambaye hajawahi kupandwa na mtu ye yote. Mfungueni mumlete hapa. Kama mtu atawauliza, ‘Mbona mnam fungua?’ Mwambieni, ‘Bwana anamhitaji na atamrudisha mara moja.’ ” 4-5 Wakaenda, wakamkuta mwana punda mmoja kando ya barabara, akiwa amefungwa kwenye mlango wa nyumba. Walipokuwa wakimfungua, watu waliokuwa wamesimama karibu wakauliza, “Mbona mnamfungua huyo mwanapunda?” Wakawajibu kama Yesu alivyokuwa amewaagiza, na wale watu wakawaruhusu.

Wakamleta huyo mwana punda kwa Yesu wakamtandikia mavazi yao, akaketi juu yake. 8-10 Watu wengi wakatandaza nguo zao barabarani na wengine wakatandaza matawi waliyokata mashambani. Na wote waliotangulia na wale waliofuata wakapaza sauti zao wakasema: “Hosana! Mungu apewe sifa! Mungu ambariki yeye anayekuja kwa jina la Bwana! Ubarikiwe Ufalme unaokuja wa baba yetu Daudi! Mungu asifiwe!”

11 Yesu akaingia Yerusalemu, akaenda Hekaluni akaangalia kila kitu. Lakini kwa kuwa ilikuwa jioni, akaenda Bethania na wale wanafunzi kumi na wawili.

Yesu Alaani Mtini Usiozaa

12 Kesho yake walipokuwa wanaondoka Bethania, Yesu alikuwa na njaa. 13 Alipouona mtini kwa mbali, alikwenda kuangalia kama ulikuwa na matunda. Alipoufikia, alikuta una majani tu kwa kuwa hayakuwa majira ya tini. 14 Yesu akauambia ule mti, “Hakuna mtu atakayekula tini kutoka kwako tena.” Wanafunzi wake walimsikia akisema hayo.

Yesu Afukuza Wafanya Biashara Hekaluni

15 Walipofika Yerusalemu, Yesu aliingia Hekaluni akaanza kuwafukuza watu waliokuwa wakifanya biashara humo. Akapindua meza za waliokuwa wakibadilisha fedha na viti vya watu waliokuwa wakiuza njiwa. 16 Hakuruhusu mtu ye yote kuchukua bidhaa kupi tia ukumbi wa Hekalu. 17 Akawafundisha akisema, “Je, haikuan dikwa katika Maandiko kuwa: ‘Nyumba yangu itaitwa nyumba ya sala kwa watu wote’? Mbona ninyi mmeigeuza kuwa pango la wany ang’anyi?”

18 Makuhani wakuu na walimu wa sheria wakapata habari. Wakatafuta njia ya kumwangamiza. Walimwogopa kwa sababu watu wal ikuwa wamevutiwa sana na mafundisho yake.

19 Ilipofika jioni, Yesu na wanafunzi wake walikwenda nje ya mji.

Fundisho Kuhusu Ule Mtini Uliolaaniwa

20 Asubuhi yake walipokuwa wakipita, wakauona ule mtini ume nyauka kutoka juu hadi kwenye mizizi yake. 21 Petro alikumbuka, akamwambia Yesu, “Mwalimu, tazama! Ule mtini ulioulaani umeny auka!”

22 Yesu akamjibu, “Mwamini Mungu. 23 Nawaambieni hakika, mtu akiuambia mlima huu, ‘Ondoka hapo nenda kajitupe baharini,’ akiamini pasipo kuwa na mashaka yo yote kwamba anayosema yata tendeka, atatimiziwa maombi yake. 24 Kwa hiyo nawaambieni, lo lote mnaloomba katika sala, aminini kwamba mmekwisha kulipokea nanyi mtapewa. 25 Nanyi mnaposimama kusali, sameheni kila mtu aliyewakosea ili Baba yenu wa mbinguni apate kuwasamehe ninyi makosa yenu.” [ 26 Lakini msipowasamehe wengine, basi makosa mliyofanya ninyi hayatasamehewa na Baba yenu wa mbinguni.]

Yesu Aulizwa Kuhusu Mamlaka Yake

27 Wakafika tena Yerusalemu. Wakati Yesu alipokuwa akitem bea Hekaluni, makuhani wakuu, walimu wa sheria pamoja na wazee wakamjia 28 wakamwuliza, “Unafanya mambo haya kwa mamlaka gani?

Na ni nani aliyekupa mamlaka hayo?”

29 Yesu akawajibu, “Nitawauliza swali mmoja. Mkinijibu, mimi pia nitawaeleza ni kwa mamlaka gani ninafanya mambo haya. 30 Niambieni, mamlaka aliyotumia Yohana kubatiza watu, yalitoka kwa Mungu au kwa watu?”

31 Wakaanza kubishana, “Tukisema, ‘Yalitoka kwa Mungu’ atatuuliza, ‘Mbona hamkumwamini?’ 32 Je, tunaweza kusema ‘Yali toka kwa watu’? - Waliogopa watu kwa sababu kila mtu aliamini kwamba Yohana Mbatizaji alikuwa nabii. 33 Kwa hiyo wakamjibu, “Hatujui.” Na Yesu akawaambia, “Mimi pia sitawaambia ni kwa mamlaka gani ninafanya mambo haya.”