Mfano Wa Shamba La Mizabibu Na Wakulima Waovu
1Yesu alianza kusema nao kwa kutumia mifano: “Mtu mmoja alipanda shamba la mizabibu; akalizungushia uzio, akachimba kisima cha kutengenezea divai na akajenga mnara. Akalikodisha shamba hilo kwa wakulima fulani kisha akasafiri kwenda nchi nyingine. 2Wakati wa mavuno ulipofika, mwenye shamba alimtuma mtumishi wake kwa hao wakulima kuchukua sehemu yake ya mavuno. 3Lakini wale wakulima walimkamata yule mtumishi, wakampiga, wakamfukuza mikono mitupu. 4Yule mwenye shamba akamtuma mtum ishi mwingine. Wale wakulima wakampiga kichwani, na kumfanyia mambo ya aibu. 5Akapeleka mtumishi mwingine tena. Huyu, wakam wua. Akapeleka wengine zaidi, baadhi yao wakawapiga na wengine wakawaua. 6Mwenye shamba akawa amebakiwa na mtu mmoja tu ambaye angeweza kumtuma. Huyu alikuwa mwanae aliyempenda sana. Hatimaye akaamua kumtuma akisema, ‘Bila shaka watamheshimu mwanangu.’ 7Lakini wale wakulima wakashauriana, ‘Huyu mwanae ndiye mrithi. Tumwue na urithi utakuwa wetu.’ 8Wakamchukua, wakamwua, wakam tupa nje ya shamba. 9Mnadhani yule mwenye shamba atafanya nini? Atakuja, awaue hao wakulima kisha alikodishe shamba lake kwa wak ulima wengine. 10Hamjasoma Maandiko haya? ‘Lile jiwe waliloli kataa wajenzi limekuwa jiwe kuu la msingi. 11Jambo hili limefa nywa na Bwana, nalo ni la ajabu kwetu.’ ”
12Viongozi wa Wayahudi wakatafuta njia ya kumkamata Yesu kwa sababu walifahamu kuwa mfano huo uliwasema wao. Lakini wali waogopa watu. Kwa hiyo walimwacha wakaondoka, wakaenda zao. Kuhusu Kulipa Kodi
13Mafarisayo kadhaa na Maherode walitumwa kuja kumtega Yesu katika maneno yake. 14Wakamjia, wakamwambia, “Mwalimu, tunafahamu kuwa wewe huwaambia watu ukweli pasipo kujali watu watasema nini. Wala hujali cheo cha mtu bali unafundisha njia ya Mungu kwa kweli. Je, ni halali au si halali kulipa kodi kwa Kais ari? 15Tulipe kodi hiyo au tusilipe?” Lakini Yesu alitambua hila yao. Akawaambia, “Mbona mnajaribu kunitega? Nileteeni sar afu niione.” 16Wakamletea. Akawauliza, “Hii ni picha ya nani na hii ni sahihi ya nani?” Wakamjibu, “Ni ya Kaisari.”
17Basi Yesu akawaambia, “Mpeni Kaisari vilivyo vya Kais ari na vya Mungu mpeni Mungu.” Jibu hili liliwastaajabisha sana.
Kuhusu Ufufuo wa Wafu
18Kisha Masadukayo, ambao wanaamini kuwa hakuna ufufuo wa wafu, walimjia Yesu wakamwuliza swali wakisema, 19“Mwalimu, Musa alituandikia agizo kuwa kama mtu akifariki akamwacha mkewe bila mtoto, basi ndugu yake hana budi kumwoa mjane huyo ili amzalie ndugu yake watoto. 20Sasa walikuwapo ndugu saba. Yule wa kwanza akaoa akafariki pasipo kupata mtoto. 21Wapili akam woa yule mjane, naye akafariki bila kuacha mtoto. Ikawa hivyo hata kwa yule wa tatu. 22Kwa kifupi, ndugu wote saba walimwoa huyo mjane lakini wote hawakuzaa naye. Hatimaye yule mama naye akafariki. 23Sasa tuambie, wakati wa ufufuo, watakapofufuka wote, huyo mama aliyeolewa na ndugu wote saba, atakuwa mke wa nani?”
24Yesu akawajibu, “Mmekosea kabisa kwa maana hamfahamu Maandiko wala uweza wa Mungu.” 25Wafu watakapofufuka, hawataoa wala kuolewa; watakuwa kama malaika wa mbinguni . 26Na kuhusu ufufuo wa wafu: hamjasoma katika kitabu cha Musa, sehemu ile inayoelezea jinsi Mungu alivyozungumza na Musa kutoka katika kichaka akisema, ‘Mimi, ni Mungu wa Ibrahimu na Mungu wa Isaka na Mungu wa Yakobo’? 27Mungu si Mungu wa wafu bali ni Mungu wa walio hai. Kwa hiyo mmekosea kabisa.”
Amri Iliyo Kuu
28Mwalimu mmoja wa sheria aliwasikiliza wakijadiliana. Alipoona kwamba Yesu amewajibu vizuri, naye akamwuliza, “Katika amri zote, ni ipi iliyo kuu?” 29Yesu akamjibu, “Iliyo kuu ni hii, ‘Sikiliza Israeli, Bwana Mungu wetu ndiye Bwana pekee. 30Nawe mpende Bwana Mungu wako kwa moyo wako wote, kwa roho yako yote, kwa akili zako zote na kwa nguvu zako zote.’ 31Na sheria ya pili kwa ukuu ndio hii: ‘Mpende jirani yako kama nafsi yako.’ Hakuna amri nyingine iliyo kuu kuliko hizi.”
32Yule mwalimu wa sheria akamwambia Yesu, “Mwalimu, ume jibu vyema. Ulivyosema ni kweli kabisa, Mungu ni mmoja wala hakuna mwingine ila yeye. 33Na kumpenda Mungu kwa moyo wote na kwa akili zote na kwa nguvu zote; na kumpenda jirani kama mtu anavyojipenda ni bora zaidi kuliko kutoa sadaka ya kuteketezwa.”
34Yesu alipoona jinsi alivyojibu kwa busara, akamwambia, “Wewe hauko mbali na Ufalme wa Mungu.” Tangu wakati huo, hakuna mtu aliyethubutu kumwuliza maswali zaidi.
Kuhusu Mwana Wa Daudi
35Yesu alipokuwa akifundisha Hekaluni, aliuliza, “Mbona walimu wa sheria wanasema kwamba Kristo ni Mwana wa Daudi? 36Kwa maana Daudi akiongozwa na Roho Mtakatifu alisema, ‘Bwana alimwambia Bwana wangu: keti mkono wangu wa kulia mpaka niwashi nde na kuwafedhehesha maadui zako chini ya miguu yako.’ 37Ikiwa Daudi mwenyewe anamwita Bwana, yawezekanaje tena Kristo akawa mwanawe?” Watu wote wakamsikiliza kwa furaha.
Yesu Awatahadharisha Watu Kuhusu Walimu Wa Shera
38Katika mafundisho yake, Yesu alisema, “Jihadharini na walimu wa sheria. Wao hupenda kutembea wakiwa wamevaa mavazi yao rasmi na kusalimiwa kwa heshima masokoni. 39Pia wao hupenda kukaa viti vya mbele katika masinagogi na kupewa nafasi za heshi ma katika sherehe. 40Hao hao ndio huwadhulumu wajane nyumba zao na ili waonekane kuwa wema wanasali sala ndefu. Mungu ata waadhibu vikali zaidi.”
Sadaka Ya Mjane
41Kisha Yesu akaketi karibu na sehemu ya kutolea sadaka Hekaluni akawaangalia watu walivyokuwa wakiweka sadaka zao kwenye chombo cha sadaka. Matajiri wengi waliweka humo kiasi kikubwa cha fedha. 42Lakini mjane mmoja fukara, alikuja akaweka sarafu mbili zenye thamani ya senti kumi.
43Yesu akawaita wanafunzi wake akawaambia, “Ninawaambia hakika, huyu mjane ametoa zaidi kuliko wote! 44Wengine wote wametoa kutokana na ziada ya mali zao; lakini huyu mama ingawa ni fukara, ameweka kila kitu alichokuwa nacho, hata na kile alicho hitaji kwa ajili ya riziki yake.”