Marko 8

Yesu Alisha Watu Elfu Nne

1Muda si mrefu baadaye, umati mkubwa wa watu ulikusanyika tena. Kwa kuwa walikuwa hawana chakula, Yesu akawaita wanafunzi wake akawaambia, 2“Ninawaonea huruma hawa watu. Wamekuwa nami kwa muda wa siku tatu sasa na hawana chakula. 3Nikiwaruhusu waende bila kula, watazimia njiani na baadhi yao wametoka mbali.”

4Wanafunzi wake wakamjibu, “Lakini hapa nyikani tutapata wapi chakula cha kutosha kuwalisha?”

5Yesu akawauliza, “Mna mikate mingapi?” Wakajibu, “Saba.”

6Akawaambia watu wakae chini. Kisha akaichukua ile mikate saba na baada ya kushukuru akaimega, akawapa wanafunzi wake wawa gawie watu. Wanafunzi wake wakafanya hivyo. 7Walikuwa pia na visamaki vichache, Yesu akavibariki, akawaamuru wanafunzi wake wawagawie watu. 8Watu walikula wakatosheka na baadaye wanafunzi wakakusanya vipande vilivyosalia wakajaza vikapu saba. 9Na watu waliokula walikuwa wapata elfu nne. Baada ya kuwaaga, 10aliin gia kwenye mashua pamoja na wanafunzi wake akaenda sehemu za Dal manutha.

11Mafarisayo wakaja, wakaanza kumhoji Yesu. Ili kumtega, wakamwomba awaonyeshe ishara kutoka mbinguni. 12Akahuzunika moyoni, akawaambia, “Kwa nini kizazi hiki kinataka ishara? Nawaambieni kweli, hakitapewa ishara yo yote.” 13Kisha aka waacha, akarudi kwenye mashua, akavuka hadi ng’ambo ya pili.

Chachu Ya Mafarisayo Na Ya Herode

14Wanafunzi walikuwa wamesahau kuleta mikate ya kutosha. Walikuwa na mkate mmoja tu kwenye mashua. 15Yesu akawaonya: “Jihadharini na chachu ya Mafarisayo na ya Herode.”

16Wakaanza kujadiliana wao kwa wao wakasema,“Anasema hivi kwa kuwa hatukuleta mikate.”

17Yesu alifahamu majadiliano yao, akawauliza: “Mbona mna zungumzia kuhusu kutokuwa na mikate? Bado hamtambui wala kuelewa? Je, mbona mioyo yenu ni migumu kiasi hicho? 18Mbona mna macho lakini mnashindwa kuona, na masikio lakini mnashindwa kusikia? Je hamkumbuki? 19Nilipoimega mikate mitano kuwalisha watu elfu tano, mlikusanya mabaki vikapu vingapi?” Wakamjibu, “Kumi na viwili.” 20“Na nilipomega mikate saba kuwalisha watu elfu nne mlikusanya mabaki vikapu vingapi?” Wakamjibu, “Saba.” 21Aka wauliza, “Je, bado tu hamwelewi?”

Yesu Amponya Kipofu Huko Bethsaida

22Wakafika Bethsaida na baadhi ya watu wakamleta kipofu mmoja wakamsihi Yesu amguse. 23Yesu akamshika mkono huyo kipofu akampeleka nje ya kijiji. Baada ya kuyatemea mate macho ya yule kipofu na kumwekea mikono, Yesu akamwuliza, “Unaona cho chote?”

24Yule kipofu akaangalia, akasema, “Ninaona watu; wanaonekana kama miti ikitembea.”

25Yesu akamwekea tena mikono machoni. Ndipo akaona vizuri. Macho yake yakapona kabisa akaweza kuona kila kitu sawa sawa.

26Yesu akamruhusu aende nyumbani kwake akisema, “Hata kijijini usipitie.”

27Yesu na wanafunzi wake wakaondoka kwenda katika vijiji vya Kaisaria Filipi. Walipokuwa njiani Yesu akawauliza, “Watu husema mimi ni nani?”

28Wakamjibu, “ Baadhi husema wewe ni Yohana Mbatizaji; wengine husema ni Eliya na wengine husema wewe ni mmojawapo wa manabii.”

29Akawauliza, “Na ninyi je, mnasema mimi ni nani?” Petro akajibu, ‘ ‘Wewe ndiye Kristo.”

30Akawaonya wasim wambie mtu ye yote habari zake.

Yesu Azungumza Juu Ya Kifo Chake

31Akaanza kuwafundisha wanafunzi wake kuwa yeye, Mwana wa Adamu, atapata mateso mengi na kukataliwa na wazee, na makuhani wakuu na walimu wa sheria; na kwamba atauawa na baada ya siku tatu atafufuka. 32Aliyasema haya wazi wazi. Ndipo Petro akam chukua kando akaanza kumkemea. 33Lakini Yesu alipogeuka na kuwatazama wanafunzi wake alimkaripia Petro akamwambia, “Ondoka mbele yangu, shetani! Mawazo yako hayako upande wa Mungu bali upande wa wanadamu.”

34Ndipo akawaita wale watu pamoja na wanafunzi wake aka waambia, “Mtu ye yote akitaka kunifuata, ni lazima ajikane mwe nyewe, auchukue msalaba wake, anifuate. 35Kwa maana mtu ye yote aipotezaye nafsi yake kwa ajili yangu na kwa ajili ya kuitangaza Habari Njema, ataiokoa. 36Mtu atafaidi nini kama atapata ulimwengu wote lakini akayaangamiza maisha yake? 37Au mtu atatoa nini apate tena maisha yake? 38Mtu ye yote atakayenionea aibu mimi na maneno yangu katika kizazi hiki kiovu na kisichomjali Mungu, na mimi, Mwana wa Adamu, nitamwonea aibu wakati nitakapokuja katika utu kufu wa Baba yangu na malaika watakatifu.”