1Kulipopambazuka, makuhani wakuu walifanya mkutano pamoja na wazee na walimu wa sheria, na Baraza zima likafanya mashauri. Wakamfunga Yesu, wakamchukua na kumkabidhi kwa Pilato. 2Pilato akamwuliza, “Wewe ndiye Mfalme wa Wayahudi?” Yesu akajibu, “Wewe ndiye uliyesema maneno hayo.” 3Makuhani wakuu wakamsh taki kwa mambo mengi. 4Pilato akamwuliza tena, “Huna la kujibu?
Unasikia mashtaka yao!”
5Yesu hakusema neno. Pilato akashangaa.
Yesu Ahukumiwa Kifo
6Ilikuwa desturi wakati wa sherehe za Pasaka kumfungulia mfungwa ye yote ambaye watu walimtaka . 7Wakati huo, mtu mmoja aitwaye Baraba alikuwa amefungwa gerezani pamoja na wahalifu wen gine kwa makosa ya kusababisha uasi ambapo mauaji yalitokea. 8Basi watu waliokusanyika walimjia Pilato wakamwomba awafanyie kama ilivyokuwa desturi wakati wa Pasaka. 9Pilato akawauliza, “Mnataka nimfungue huyu mfalme wa Wayahudi?” 10Alikuwa ana fahamu kwamba wakuu wa makuhani walikuwa wanamwonea Yesu wivu ndio sababu wakamshtaki kwake. 11Lakini makuhani wakuu wakawa chochea watu wamwombe awafungulie Baraba.
12Pilato akawauliza tena watu, “Nimfanye nini huyu mtu mnayemwita mfalme wa Wayahudi?” 13Wakapiga kelele, “Msulub ishe!” 14Akawauliza, “Kwa nini? Amefanya kosa gani?” Lakini wao wakapiga kelele kwa nguvu zaidi, “Msulubishe!”
15Pilato alitaka kuwaridhisha watu, kwa hiyo akamfungulia Baraba; na baada ya kuamuru Yesu apigwe mijeledi, akamtoa asulub ishwe.
Maaskari Wamdhihaki Yesu
16Maaskari wakampeleka Yesu hadi kwenye ukumbi wa ndani ya Ikulu iliyoitwa Praitoria, wakakusanya kikosi kizima cha askari. 17Wakamvika Yesu vazi la zambarau, wakatengeneza taji ya miiba, wakamvika. 18Wakaanza kumsalimu kwa dhihaka, “Salamu, Mfalme wa Wayahudi!” 19Wakampiga kwa fimbo kichwani, wakamte mea mate. Wakamdhihaki kwa kupiga magoti kama vile wanamheshimu mfalme. 20Walipokwisha kumdhihaki, walimvua lile vazi la zam barau, wakamvika nguo zake. Kisha wakamtoa nje wakamsulubishe.
Yesu Asulubishwa
21Walipokuwa wakienda kumsulubisha, njiani walikutana na mtu mmoja aitwaye Simoni, raia wa Kirene. Yeye alikuwa baba yao Aleksanda na Rufas. Alikuwa anakuja mjini kutoka shamba. Wakamla zimisha abebe msalaba wa Yesu. 22Kisha wakampeleka Yesu mpaka mahali palipoitwa Golgota, -yaani Mahali pa Fuvu la Kichwa.
23Wakampa divai iliyochanganywa na manemane, lakini akaikataa. 24Basi wakamsulubisha, wakagawana nguo zake kwa kuzipigia kura kuamua kila mtu achukue nini.
25Ilikuwa yapata saa tatu asubuhi walipomsulubisha. 26Tangazo la mashtaka yake liliandikwa maneno haya: “MFALME WA WAYAHUDI.” 27Majambazi wawili walisulubiwa pamoja naye, mmoja upande wake wa kulia na mwingine upande wa kushoto. [ 28Na kwa njia hii yale Maandiko yasemayo, “Alihesabiwa pamoja na wenye hatia,” yalitimia.] 29Watu waliokuwa wakipita, walimtukana na kutikisa vichwa vyao kwa mzaha wakasema, “Si ulikuwa ukisema kwamba unaweza kulivunja Hekalu na kulijenga kwa siku tatu? 30Shuka msalabani basi, ujiokoe mwenyewe!” 31Hali kadhalika makuhani wakuu na walimu wa sheria walimdhihaki wakisema, “Ali waokoa wengine lakini anashindwa kujiokoa mwenyewe. 32Kristo mfalme wa Wayahudi ashuke basi msalabani ili tupate kuona na kuamini!” Na wale waliosulubiwa pamoja naye pia walimtukana.
Kifo Cha Yesu Msalabani
33Ilipofika saa sita, giza lilikumba nchi nzima kwa muda wa saa tatu. 34Ilipofika saa tisa, Yesu akalia kwa sauti kuu “Eloi, Eloi lama Sabaktani?” Yaani, “Mungu wangu, Mungu wangu, mbona umeniacha?” 35Baadhi ya watu waliokuwa wanasimama karibu waliposikia maneno hayo, walisema, “Mnamsikia? Anamwita
Eliya!”
36Mtu mmoja akaenda mbio, akachovya sponji kwenye divai na siki, akaiweka kwenye ufito akamwinulia Yesu ili anywe huku akisema, “Hebu tuone kama Eliya atakuja kumshusha kutoka msala bani!”
37Yesu akatoa sauti kuu, akakata roho. 38Pazia la hekalu likapasuka vipande viwili kuanzia juu hadi chini.
39Yule askari aliyekuwa amesimama mbele ya msalaba alipoona jinsi alivyokata roho, akasema, “Hakika mtu huyu alikuwa Mwana wa Mungu!”
40Walikuwapo pia wanawake walio kuwa wakiangalia mambo haya kwa mbali. Kati yao walikuwapo Mariamu Magdalena, na Mariamu mama yao Yakobo mdogo na Yose, na pia Salome . 41Hawa walifuatana na Yesu alipokuwa Galilaya na kumhudumia. Pia walikuwapo wanawake wengine wengi waliokuwa wamekuja naye Yerusalemu.
Mazishi Ya Yesu
42Ilipofika jioni, kwa kuwa ilikuwa siku ya Maandalizi, siku moja kabla ya Pasaka, 43Yusufu wa Arimathea alijikaza akamwendea Pilato akamwomba auchukue mwili wa Yesu. Yeye alikuwa ni mjumbe wa Baraza aliyeheshimika, ambaye alikuwa anatazamia kuja kwa Ufalme wa Mungu. 44Pilato alishangaa kusikia kwamba Yesu amekwisha kufa. Kwa hiyo akamwita askari amhakikishie kuwa kweli amekufa. 45Baada ya kuhakikishiwa na yule askari kwamba kweli amekufa, Pilato alimpa Yusufu ruhusa ya kuuchukua mwili wa Yesu. 46Basi Yusufu alinunua sanda ya kitani, akautoa mwili wa Yesu msalabani; akamzungushia sanda, akamweka ndani ya kaburi lililochongwa kwenye mwamba. Kisha akaviringisha jiwe akaufunika mlango wa kaburi. 47Mariamu Magdalena na Mariamu mama wa Yose walipaona mahali alipozikwa Yesu.