Yesu Anatabiri Kubomolewa Kwa Hekalu
1Alipokuwa akitoka nje ya Hekalu, mmojawapo wa wanafunzi wake akamwambia, “Mwalimu, ona jinsi mawe haya na majengo haya yalivyo maridadi!”
2Yesu akamjibu, “Unayaona majengo haya yalivyo makubwa? Hakuna hata jiwe moja litakalobaki juu ya jingine, yote yatabomo lewa.”
Yesu Anawaambia Wafuasi Wake Wajiandae Kwa Mateso
3Alipokuwa ameketi kwenye mlima wa Mizeituni akiliangalia Hekalu, Petro, Yakobo na Yohana walimwuliza faraghani, 4“Tafadhali tuambie, mambo haya yatatokea lini, na ni ishara gani zitaonyesha kuwa karibu yatatimia?” 5Yesu akaanza kuwaeleza: “Jihadharini mtu asije akawadanganya. 6Wengi wata kuja wakilitumia jina langu na kusema, ‘Mimi ndiye’ na wata wadanganya wengi. 7Na mkisikia habari za vita na uvumi juu ya vita, msishtuke. Mambo haya hayana budi kutokea, lakini mwisho utakuwa bado. 8Mataifa yatapigana na falme kushambuliana. Matetemeko ya ardhi yatatokea sehemu mbalimbali na kutakuwa na njaa. Lakini huu utakuwa kama maumivu ya mwanzo tu ya uchungu wa uzazi. 9Lakini ninyi jihadharini. Kwa maana watu watawapeleka mahakamani na mtapigwa mijeledi katika masinagogi. Mtashtakiwa mbele ya watawala na wafalme kwa ajili yangu, ndipo mtaweza kutoa ushuhuda kuhusu Habari Njema. 10Lakini kabla mwisho kufika, Habari Njema itahubiriwa kwa mataifa yote. 11“Mtakapokamatwa na kupelekwa mahakamani, msihangaike kuhusu mtakalosema. Semeni lo lote litakalowajia wakati huo, kwa sababu maneno mtakayosema si yenu bali yatatoka kwa Roho Mtaka tifu.
12“Ndugu atamsaliti ndugu yake auawe; baba atamsaliti mwanae. Watoto watawaasi wazazi wao na kusababisha wauawe. 13Kila mtu atawachukia kwa ajili yangu; lakini atakayevumilia mpaka mwisho, ataokolewa.
14“Mtakapoona ile ‘sanamu ya chukizo’ imesimama mahali isipostahili - msomaji na aelewe maana yake -basi wale walioko Yudea wakimbilie milimani. 15Mtu aliyeko juu ya nyumba asiter emke kuingia ndani kuchukua cho chote. 16Aliyeko shambani asi rudi nyumbani kuchukua koti lake. 17Ole wao akina mama waja wazito na watakaokuwa wakinyonyesha siku hizo! 18Ombeni mambo haya yasitokee wakati wa masika. 19Kwa maana siku hizo itaku wapo dhiki kuu ambayo haijapata kutokea tangu dunia ilipoumbwa, wala haitatokea tena. 20Na kama Bwana hakuufupisha muda huo wa dhiki, hakuna mtu ambaye angesalimika; lakini kwa ajili ya watu wake aliowachagua, ameufupisha muda huo.
21“Na wakati huo mtu akiwaambia, ‘Tazama, Kristo huyu hapa’ au , ‘Tazama, yule pale,’ msiamini. 22Kwa maana watatokea makristo wa uongo na manabii wa uongo nao watafanya ishara na miujiza ili kuwadanganya hata wale waliochaguliwa na Mungu, kama ikiwezekana. 23Kwa hiyo jihadharini kwa maana nimewaambia mambo haya kabla hayajatokea.”
Kuja Kwa Mwana Wa Adamu
24“Siku hizo, baada ya hiyo dhiki, jua litatiwa giza na mwezi hautatoa mwanga wake. 25Nyota zitaanguka kutoka mbinguni na nguvu za anga zitatikisika. 26Ndipo watu wote wataniona mimi Mwana wa Adamu nikija katika mawingu kwa nguvu nyingi na utu kufu. 27Nami nitawatuma malaika wawakusanye watu wangu kutoka pande zote nne za dunia, kutoka mwisho wa nchi hadi mwisho wa mbi ngu.
28“Sasa jifunzeni jambo hili kutoka kwa mtini: mwonapo matawi ya mtini yakianza kulainika na kutoa majani, mnatambua kwamba wakati wa kiangazi umekaribia. 29Hali kadhalika mtaka poyaona mambo haya yanatokea, tambueni kwamba mimi Mwana wa Adamu, ni karibu kuja. 30Ninawaambieni hakika, kizazi hiki hakitapita kabla ya mambo haya kutokea. 31Mbingu na nchi zita toweka, lakini maneno yangu hayatapita kamwe.”
Hakuna Ajuaye Siku Wala Saa
32“Hakuna ajuaye siku hiyo itakuwa lini au saa ngapi; hata malaika mbinguni hawajui wala mimi Mwana sijui, isipokuwa Mungu Baba peke yake. 33“Jiandaeni, muwe macho. Kwa maana hamjui wakati mambo haya yatakapotokea. 34Ni kama mtu anayesafiri na kuwaachia wat umishi wake madaraka, kila mtu na wajibu wake; kisha akamwambia mlinzi wa mlango awe macho. 35Kesheni basi, kwa sababu hamjui ni lini bwana mwenye nyumba atarudi. Anaweza akaja jioni, au usiku wa manane au alfajiri au mapambazuko. 36Kama akija gha fla, pasipo ninyi kumtazamia, asije awakute mmelala. 37Na haya ninayowaambia ninyi nawaambia watu wote: Kesheni!”