Marko 3

Yesu Amponya Mtu Aliyelemaa Mkono

1Yesu aliingia tena katika sinagogi na mtu mmoja aliyelemaa mkono alikuwapo pia. 2Baadhi ya watu waliokuwa wakimtega, ili wapate sababu ya kumshtaki, walimtazama kwa makini waone kama atamponya huyo kilema siku ya sabato. 3Yesu akamwambia yule mwe nye mkono uliolemaa, “Njoo hapa mbele.”

4Yesu akawauliza, “Ni lipi lililo halali siku ya sabato? Kufanya jema, au baya? Kusalimisha maisha au kuua?” Wakakaa kimya.

5Yesu akawatazama kwa hasira, akahuzunishwa na ugumu wa mioyo yao. Akamwambia yule mtu, “Nyoosha mkono wako.” Akauny oosha, nao ukapona kabisa! 6Kisha Mafarisayo wakatoka nje, wakaenda kushauriana na kundi la wafuasi wa Herode mbinu za kum wua Yesu.

Umati Wa Watu Wamfuata Yesu

7Yesu pamoja na wanafunzi wake waliondoka mahali hapo wakaenda ziwani wakifuatwa na umati mkubwa wa watu kutoka Gali laya na Yudea. 8Na watu kutoka Yerusalemu, Idumaya, na eneo lote la ng’ambo ya Yordani, sehemu za Tiro na Sidoni, waliposi kia mambo aliyokuwa akitenda, wakamwendea. 9Akawaomba wanafunzi wake wamwandalie mashua ili asisongwe na kubanwa sana na watu. 10Kwa kuwa alikuwa amewaponya wagonjwa wengi, wote wenye mar adhi walikuwa wakisukumana wapate kumgusa. 11Na kila mara pepo wachafu walipomwona, walianguka chini mbele yake na kulia kwa sauti kuu, “Wewe ni Mwana wa Mungu.” 12Lakini aliwaamuru wasimtambulishe kwa watu.

Yesu Achagua Mitume Kumi Na Wawili

13Yesu alipanda mlimani akawaita wale aliowataka, nao wakaja. 14Akawachagua kumi na wawili wafuatane naye na awatume kuhubiri na 15wawe na mamlaka ya kufukuza pepo. 16Hawa ndio aliowachagua: Simoni, ambaye alimwita Petro, 17Yakobo na Yohana, wana wa Zebedayo ambao aliwaita Boanerge, yaani wana wa ngurumo; 18Andrea; Filipo; Bartholomayo; Mathayo; Tomaso; Yakobo, mwana wa Alfayo; Thadayo; Simoni, Mkanaani; na 19Yuda

Yesu Na Beelzebuli

20Yesu akarudi nyumbani. Umati wa watu ukamfuata tena, hata yeye na wanafunzi wake wakashindwa kula chakula. 21Ndugu zake walipopata habari walikuja kumchukua kwa maana watu walikuwa wakisema, “Amerukwa na akili.”

22Walimu wa sheria waliotoka Yerusalemu walikuwa wakisema, “Amepagawa na Beelzebuli, mkuu wa mashetani; na ni kwa uwezo wa Beelzebuli anawafukuza mashetani.”

Beelzebuli anawafukuza mashetani.”

23Basi Yesu akawaita akazungumza nao kwa mifano: “Shetani awezaje kufukuza shetani? 24Ikiwa utawala wa nchi umegawanyika wenyewe, hauwezi kudumu. 25Hali kadhalika kama jamaa moja ime gawanyika yenyewe kwa yenyewe, jamaa hiyo haiwezi kudumu. 26Na kama shetani akijipiga vita yeye mwenyewe hatatimiza cho chote ila mwisho wake umekaribia. 27Pia hakuna mtu awezaye kuivamia nyumba ya mtu mwenye nguvu na kumwibia vitu vyake vyote pasipo kwanza kumfunga huyo mwenye nyumba mwenye nguvu. Akisha mfunga, ndipo anaweza kumwibia kila kitu.

28“Nawaambieni kweli, dhambi zote watendazo wanadamu na maneno yote ya kufuru wasemayo, watasamehewa. 29Lakini ye yote anayemtukana Roho Mtakatifu hatasamehewa kamwe, atakuwa na hatia ya dhambi ya milele.” 30Yesu alisema hivi kwa sababu walikuwa wanasema ana pepo mchafu.

Mama Na Ndugu Wa Yesu

31Mama yake Yesu na ndugu zake wakafika wakasimama nje wakamtuma mtu amwite. 32Umati wa watu waliokuwa wameketi kum zunguka wakamwambia, “Mama yako na ndugu zako wako nje, wana kutafuta.”

33Akawauliza, “Mama yangu na ndugu zangu ni akina nani?”

34Akawatazama wale watu waliokuwa wameketi kumzunguka, akasema, “Hawa ndio mama zangu na ndugu zangu. 35Mtu ye yote anayetenda mapenzi ya Mungu ndiye ndugu yangu na dada yangu na mama yangu.”