Yesu Ahudhuria Harusi Mjini Kana
1Siku ya tatu kulikuwa na harusi katika mji wa Kana ulioko Galilaya. Mama yake Yesu alikuwapo 2 na Yesu pamoja na wanafunzi wake walikuwa wamealikwa pia. 3 Divai ilipowaishia, mama yake Yesu alimwambia, “Hawana divai.” 4 Yesu akamjibu, “Mama, mbona unanihusisha kwenye jambo hili? Wakati wangu bado haujafika.” 5 Mama yake akawaambia watumishi, “Lo lote atakalowaambia, fanyeni. ” 6 Basi ilikuwapo hapo mitungi sita ya kuwekea maji ya kunawa, kufuatana na desturi ya Wayahudi ya kutawadha. Kila mtungi ungeweza kujazwa kwa madebe sita au saba ya maji. 7 Yesu akawaambia wale watumishi, “Ijazeni mitungi hiyo maji.” Wakaijaza mpaka juu. 8 Kisha akawaambia, “Sasa choteni maji kidogo mumpelekee mkuu wa sherehe.” Wakachota, wakampelekea. 9 Yule mkuu wa sherehe akayaonja yale maji ambayo yalikuwa yame geuka kuwa divai. Hakujua divai hiyo imetoka wapi ingawa wale watumishi waliochota yale maji walifahamu. Basi akamwita bwana harusi kando 10 akamwambia, “Watu wote huwapa wageni divai nzuri kwanza kisha wakianza kutosheka huwaletea divai hafifu.
Imekuwaje wewe ukaiweka divai nzuri mpaka sasa?”
11 Hii ilikuwa ishara ya kwanza aliyofanya Yesu. Muujiza huu ulifanyika katika mji wa Kana huko Galilaya, ambako Yesu alidhi hirisha utukufu wake, na wanafunzi wake wakamwamini. 12 Baada ya haya, Yesu pamoja na mama yake, ndugu zake na wanafunzi wake, walikwenda Kapernaumu ambapo alikaa kwa siku chache.
Yesu Alitakasa Hekalu
13 Ilipokaribia sikukuu ya Wayahudi iitwayo Pasaka, Yesu alikwenda Yerusalemu. 14 Alipoingia Hekaluni aliwakuta watu wakiuza ng’ombe, kondoo na njiwa, na wengine wamekaa kwenye meza zao wakifanya biashara ya kubadilishana fedha. 15 Akatengeneza mjeledi wa kamba akawafukuza wote kutoka Hekaluni pamoja na kon doo na ng’ombe; akazipindua meza za wale waliokuwa wakibadilish ana fedha na kuzimwaga fedha zao. 16 Akawaambia wale waliokuwa wakiuza njiwa, “Watoeni hapa! Mnathubutuje kuifanya nyumba ya Baba yangu kuwa soko?” 17 Wanafunzi wake wakakumbuka kuwa Maan diko yalisema: “Upendo wangu kwa nyumba yako utaniangamiza.”
18 Viongozi wa Wayahudi wakamwuliza, “Unaweza kutuonyesha ishara gani kuthibitisha una mamlaka ya kufanya mambo haya?”
19 Yesu akawajibu, “Livunjeni hili Hekalu, nami nitalijenga tena kwa siku tatu!”
20 Wale Wayahudi wakamjibu, “Hekalu hili lilijengwa kwa muda wa miaka arobaini na sita. Wewe unasema unaweza kulijenga kwa siku tatu?”
21 Lakini yeye aliposema ‘Hekalu’ alikuwa anazungumzia mwili wake. 22 Kwa hiyo alipofufuliwa kutoka kwa wafu, wanafunzi wake walikumbuka maneno haya; wakayaamini Maandiko na yale maneno ali yosema Yesu.
23 Yesu alipokuwa Yerusalemu kwenye sikukuu ya Pasaka, watu wengi waliona ishara za ajabu alizokuwa akifanya, wakamwamini. 24 Lakini Yesu hakuwa na imani nao kwa sababu aliwajua binadamu wote. 25 Hakuhitaji mtu ye yote amwambie lo lote kuhusu bina damu. Alijua yote yaliyokuwa mioyoni mwao.