Mchungaji Mwema
1“Ninawaambia hakika, mtu asiyeingia katika zizi la kondoo kwa kupitia mlangoni, bali hupenya ndani kwa kupitia njia nyin gine, ni mwizi na mnyang’anyi. 2 Anayepitia mlangoni ndiye mchun gaji wa kondoo. 3 Mlinzi humfungulia mlango na kondoo hutambua sauti yake. Yeye huwaita kondoo wake kwa majina yao na kuwaongoza nje ya zizi. 4 Akiisha watoa wote nje, hutangulia mbele yao na kondoo humfuata kwa kuwa wanaifahamu sauti yake. 5 Kondoo hawam fuati mtu wasiyemfahamu bali humkimbia, kwa sababu hawatambui sauti ya mgeni.” 6 Yesu alitumia mfano huu lakini wao hawakuel ewa maana yake.
7 Kwa hiyo Yesu akasema nao tena akawaambia, “Mimi ni mlango wa kupitia kondoo. 8 Wote walionitangulia ni wezi na wany ang’anyi. Hata hivyo kondoo hawakuwafuata. 9 Mimi ni mlango; mtu ye yote anayeingia zizini kwa kupitia kwangu atakuwa salama, naye ataingia na kutoka na kupata malisho. 10 Mwizi huja kwa nia ya kuiba, kuua na kuharibu. Nimekuja ili watu wapate uzima; uzima ulio kamili. 11 Mimi ni Mchungaji Mwema. Mchungaji Mwema hutoa maisha yake kwa ajili ya kondoo. 12 Mtu wa kuajiriwa anapoona mbwa mwitu akija, hukimbia na kuwaacha kondoo hatarini kwa kuwa kondoo si wake, naye si mchungaji wao; na hivyo mbwa mwitu huwar ukia kondoo na kuwatawanya. 13 Yeye hukimbia kwa sababu ameaji riwa tu na hawajali kondoo.
14 Mimi ni Mchungaji Mwema: ninawafahamu kondoo wangu nao wananifahamu, 15 kama vile Baba yangu anavyonifahamu na mimi ninamfahamu. Nami nautoa uhai wangu kwa ajili ya kondoo. 16 Ninao kondoo wengine ambao si wa zizi hili; nao pia itanibidi niwalete, nao wataisikia sauti yangu. Hivyo patakuwa na kundi moja na mchungaji mmoja. 17 Baba yangu ananipenda kwa kuwa ninautoa uhai wangu ili niupate tena. 18 Hakuna mtu atakayeondoa uhai wangu, bali ninautoa mwenyewe. Ninao uwezo wa kuutoa uhai wangu na pia ninao uwezo wa kuuchukua tena. Hii ni amri niliyopo kea kutoka kwa Baba yangu.”
19 Maneno haya yalisababisha mafarakano tena kati ya Way ahudi. 20 Wengi wao walisema, “Huyu amepagawa na shetani, kwa nini tuendelee kumsikiliza?” 21 Wengine wakasema, “Haya si maneno ya mtu aliyepagawa na shetani. Je, shetani anaweza kumpo nya kipofu?”
Yesu Anajitambulisha
22 Ilikuwa sikukuu ya Utakaso wa Hekalu wakati wa majira ya baridi, 23 na Yesu alikuwa akitembea ndani ya Hekalu katika ukumbi wa Sulemani. 24 Wayahudi wakamzunguka wakamwuliza, “Utatuweka katika hali ya mashaka mpaka lini? Kama wewe ndiye Kristo utuambie wazi wazi.” 25 Yesu akawajibu, “Nimewaambia lakini hamuamini. Mambo ninayoyatenda kwa jina la Baba yangu yan anishuhudia. 26 Lakini hamuamini kwa sababu ninyi si wa kundi la kondoo wangu. 27 Kondoo wangu husikia sauti yangu nami nawajua, nao hunifuata; 28 nami ninawapa uzima wa milele. Hawataangamia kamwe wala hakuna mtu atakayewapokonya kutoka katika mikono yangu. 29 Baba yangu ambaye amenipa hawa ni mkuu kuliko wote na hakuna awezaye kuwatoa hawa kutoka katika mikono yake. 30 Mimi na Baba yangu tu mmoja.”
31 Kwa mara nyingine wale Wayahudi wakainua mawe ili wampige nayo. 32 Yesu akawauliza, “Nimewaonyesha mambo mengi mazuri kutoka kwa Baba yangu. Kati ya hayo ni lipi linalosababisha mtake kunipiga mawe?” 33 Wao wakamjibu, “Tunataka kukupiga mawe si kwa sababu ya mambo mema uliyotenda bali ni kwa kuwa umekufuru. Wewe ni mtu tu lakini unajiita Mungu.”
Wewe ni mtu tu lakini unajiita Mungu.”
34 Yesu akawauliza, “Je, haikuandikwa katika Maandiko yenu ya sheria, ‘Nimesema, ninyi ni miungu’? 35 Ikiwa Maandiko, ambayo ni kweli daima, yanawataja wale waliyoyapokea kuwa ni ‘miungu 36 itakuwaje mseme ninakufuru ninaposema ‘mimi ni Mwana wa Mungu,’ ambapo mimi Baba ameniteua niwe wake na akani tuma ulimwenguni? 37 Ikiwa sifanyi kazi za Baba yangu, basi msi niamini; 38 lakini ikiwa nafanya kazi za Mungu, mziamini hizo; hata kama hamniamini mimi. Mkifanya hivyo, mtaelewa na kutambua kuwa Baba yangu yuko ndani yangu na mimi ni ndani yake.”
39 Kwa mara nyingine Wayahudi wakajaribu kumkamata, lakini yeye aka waponyoka.
40 Kisha akaenda ng’ambo ya mto Yordani mpaka pale mahali ambapo Yohana alianzia kubatiza, akakaa huko. 41 Watu wengi wakamfuata, nao wakawa wakiambiana, “Yohana hakufanya muujiza wo wote, lakini kila jambo alilosema kumhusu huyu mtu ni kweli.” 42 Na wengi wakamwamini Yesu.