Mariamu Ampaka Yesu Mafuta
1Siku sita kabla ya sikukuu ya Pasaka, Yesu alikwenda mpaka Bethania ambako Lazaro aliyemfufua alikuwa anaishi. 2 Wakamwan dalia karamu; na Martha akawahudumia. Lazaro alikuwa miongoni mwa wageni waliokaa mezani pamoja na Yesu. 3 Kisha Mariamu akachukua chupa yenye manukato ya thamani kubwa akayamimina miguuni mwa Yesu na kuipangusa kwa nywele zake. Nyumba nzima ikajaa harufu ya manukato. 4 Ndipo Yuda Iskariote, mmoja wa wanafunzi, ambaye baadaye alimsaliti Yesu, akasema, 5 “Kwa nini manukato haya hay akuuzwa zikapatikana fedha nyingi wapewe maskini?” 6 Yuda alisema hivi si kwa kuwa aliwajali sana maskini bali kwa kuwa alikuwa mwizi. Kama mtunza fedha, alikuwa mara kwa mara anaiba kutoka katika fedha alizokabidhiwa. 7 Yesu akajibu, “Msimsumbue! Mwacheni ayaweke manukato hayo kwa ajili ya siku ya kifo changu. 8 Maskini wapo pamoja nanyi siku zote ila hamtakuwa nami siku zote. ” 9 Umati mkubwa wa Wayahudi waliposikia kwamba Yesu ali kuwa Bethania, walikuja ili pia wamwone Lazaro ambaye alimfufua. 10 Kwa hiyo makuhani wakuu wakafanya mpango wa kumuua Lazaro pia, 11 kwa kuwa baada ya kufufuliwa kwake Wayahudi wengi wal iamua kuwakataa viongozi wao na kumwamini Yesu.
Yesu Aingia Yerusalemu Akishangiliwa
12 Kesho yake watu wengi waliokuja mjini kwa sikukuu waka pata habari kuwa Yesu angekuja Yerusalemu. 13 Basi wakachukua matawi ya mitende wakatoka kwenda kumpokea, huku wakiimba, “Hosana! Amebarikiwa anayekuja kwa jina la Bwana! Mungu ambar iki Mfalme wa Israeli!” 14 Yesu akampata mwanapunda akampanda, kama ilivyoandikwa katika Maandiko, 15 “Usiogope, wewe mwenyeji wa Sioni. Tazama, mfalme wako anakuja, amepanda mwanapunda!”
16 Wanafunzi wa Yesu hawakuelewa mambo haya wakati huo, lakini Yesu alipofufuka kwa utukufu walikumbuka kuwa mambo haya yalikuwa yametajwa katika Maandiko; na kwamba waliyatekeleza kwa ajili yake. 17 Wale waliokuwepo wakati Yesu alipomwita Lazaro kutoka kaburini na kumfufua, baadaye waliwasimulia wengine yaliy otokea. 18 Ndio sababu watu wengi walitoka kwenda kumpokea, kwa kuwa walikuwa wamesikia kwamba alikuwa ametenda muujiza huu. 19 Mafarisayo walipoona haya wakaambiana, “Mnaona? Hakuna tun aloweza kufanya; ulimwengu wote unamfuata!”
Yesu Anatabiri Kifo Chake
20 Kati ya watu waliokwenda Yerusalemu kuabudu wakati wa sikukuu walikuwepo Wagiriki kadhaa. 21 Hawa walimjia Filipo, ambaye alikuwa mwenyeji wa Bethsaida huko Galilaya, wakamwambia, “Tungependa kumwona Yesu.” 22 Filipo akaenda akamweleza Andrea, na wote wawili wakamwambia Yesu. 23 Yesu akawaambia, “Wakati umefika wa mimi Mwana wa Adamu kutukuzwa. 24 Ninawaha kikishia kuwa, mbegu ya ngano isipopandwa ardhini na kufa, huba kia peke yake. Lakini ikifa inazaa nafaka kwa wingi. 25 Mtu ye yote anayeishi kwa ajili ya nafsi yake tu, ataipoteza, lakini mtu anayeishi kwa ajili ya wengine, atasalimisha nafsi yake kwa maisha ya milele. 26 Mtu ye yote anayetaka kunitumikia lazima anifuate; ili mtumishi wangu awepo mahali nilipo; na mtu ye yote akinitumikia, Baba yangu atampa tuzo ya heshima.
27 “Moyo wangu unafadhaika sana. Niombeje? ‘Baba uniepushe na mambo yatakayotokea’? La, nilikuja ulimwenguni kwa sababu hii. 28 Baba, dhihirisha utukufu wa jina lako!” Kisha ikasikika sauti kutoka mbinguni, “Nimedhihirisha utukufu wa jina langu, na nitafanya hivyo tena.” 29 Umati wa watu uliposikia sauti hii, baadhi walidhani ilikuwa ni sauti ya radi, na wengine wakasema, “Malaika alikuwa anaongea naye.” 30 Yesu akawaambia, “Sauti hii imesikika, si kwa faida yangu, bali ni kwa faida yenu. 31 Wakati wa Mungu kutamka hukumu juu ya ulimwengu umetimia, huu ni wakati ambao shetani, mtawala wa dunia hii, atapinduliwa. 32 Nami nitakapoinuliwa kutoka ardhini, nitawavuta watu wote waje kwangu.” 33 Alisema haya ili kuonyesha jinsi atakavyokufa. 34 Wakamwambia, “Tumesoma katika Maandiko ya sheria kuwa Kristo anaishi milele na hatakufa. Mbona unasema lazima Mwana wa Adamu ainuliwe? Huyo Mwana wa Adamu ni nani? 35 Yesu akawajibu, “Nuru yangu itawaangazia kwa muda mfupi. Tembeeni wakati nuru bado ipo nanyi msije mkakumbwa na giza. Mtu anayetembea gizani hajui ana kokwenda. 36 Wakati mkiwa na nuru, muitegemee hiyo nuru ili mpate kuwa wana wa nuru.” Baada ya kusema haya, Yesu aliondoka akajificha.
Kutokuamini Kwa Wayahudi
37 Hata baada ya miujiza yote Yesu aliyofanya mbele yao hawakumwamini. 38 Ikawa kama alivyotabiri nabii Isaya aliposema, “Bwana, ni nani ameamini tuliyowaambia? Na ni nani ambaye ameona nguvu za Bwana?” 39 Kwa hiyo hawakuamini, kwa sababu kama Isaya alivyosema tena, 40 “Mungu amewafanya vipofu wasione na mioyo yao ameifanya migumu, ili wasije wakaona kwa macho yao na kuamini kwa mioyo yao, na kumgeukia Mungu awaponye.” 41 Isaya alisema haya kwa kuwa aliona katika maono utukufu wa Yesu na akatabiri juu yake. 42 Hata hivyo wapo wengi, pamoja na viongozi wa Way ahudi, ambao walimwamini, lakini hawakukiri wazi wazi kwa sababu waliwaogopa Mafarisayo, wasije wakafukuzwa kutoka katika masina gogi yao. 43 Wao walithamini zaidi sifa za watu kuliko sifa kutoka kwa Mungu.
Amwaminiye Yesu Hatabaki Gizani
44 Yesu akasema kwa sauti kuu, “Mtu anayeniamini mimi, anamwamini Mungu aliyenituma. 45 Na mtu anayeniona mimi, anam wona yeye ali yenituma. 46 Nimekuja kama nuru ulimwenguni, ili kila mtu anayeniamini asibaki gizani. 47 Mtu anayesikia maneno yangu asiyatii, simhukumu; kwa maana sikuja ulimwenguni kuhukumu bali kuokoa. 48 Mtu anayenikataa na kuyapuuza maneno yangu anaye hakimu; neno nililotamka litamhukumu siku ya mwisho. 49 Sikusema mambo haya kwa mamlaka yangu mwenyewe. Bali Baba yangu aliyeni tuma amenipa amri kuhusu mambo ninayosema na kutamka. 50 Ninafa hamu ya kuwa sheria yake ni uzima wa milele. Kwa hiyo ninayosema ni yale ambayo Baba yangu ameniagiza niyaseme.”