Wana Wa Mungu
1Nataka muelewe kwamba mrithi akiwa bado ni mtoto mdogo hana tofauti na mtumwa, ingawa mali yote ni yake. 2 Kwa sababu anakuwa yuko chini ya uangalizi wa walezi na wadhamini mpaka ufike wakati uliowekwa na baba yake. 3 Hali kadhalika na sisi, tulipokuwa bado watoto wadogo, tulikuwa tunatawaliwa na kanuni za mazingira. 4 Lakini wakati ulipotimia, Mungu alimtuma Mwana we, ambaye alizaliwa na mwanamke chini ya sheria, 5 ili kusudi awakomboe wale waliokuwa chini ya sheria, tupate kibali cha kuwa wana wa Mungu. 6 Na kwa kuwa ninyi sasa ni wana wa Mungu, Mungu amemtuma Roho wa Mwanae akae ndani ya mioyo yenu, akiita, “Abba! Baba.” 7 Kwa hiyo, wewe sio mtumwa tena, bali ni mwana wa Mungu, na ikiwa wewe ni mwana wa Mungu, basi wewe pia ni mrithi.
Paulo Alivyowajali Wagalatia
8 Zamani, wakati hamkumjua Mungu, mlikuwa mkitumikia ‘miu ngu’ ambayo kwa asili si miungu. 9 Lakini sasa kwa kuwa mmemfa hamu Mungu, au tuseme, sasa Mungu anawafahamu ninyi, mnawezaje kurudia tena upungufu na umaskini wa nguvu za pepo muwe watumwa wake? 10 Bado mnaadhimisha siku maalumu, miezi, nyakati na miaka! 11 Nina hofu juu yenu; inaelekea kazi niliyofanya kwa ajili yenu imepotea bure.
12 Ndugu zangu, nawasihi muwe kama mimi, kwa sababu na mimi nimekuwa kama ninyi. Hamkunitendea ubaya wo wote. 13 Ninyi mnafahamu kwamba ugonjwa wangu ndio ulionipatia nafasi ya kuwa hubiria Habari Njema kwa mara ya kwanza. 14 Lakini ninyi hamku nidharau wala kunikataa ingawa udhaifu wa mwili wangu ulikuwa mzigo kwenu. Bali mlinipokea vizuri kama malaika wa Mungu, na kama Kristo Yesu. 15 Ile furaha mliyokuwa nayo iko wapi sasa? Naweza kushuhudia kwamba wakati ule mlikuwa tayari hata kung’oa macho yenu mnipe. 16 Je, sasa nimekuwa adui yenu kwa sababu nawaambieni ukweli?
17 Hao watu wanaoshughulika ili muwe upande wao nia yao si nzuri. Wanataka kuwatenganisha na sisi ili muwajali wao zaidi. 18 Ni vema watu wanapowahangaikia kwa bidii kama shabaha ya kufanya hivyo ni nzuri, na kama wanafanya hivyo wakati wote, isiwe tu wakati nikiwa nanyi. 19 Watoto wangu wadogo, najisikia kwa mara nyingine kama mama mwenye uchungu wa kuzaa, nikitamani kwamba Kristo aumbike ndani yenu. 20 Natamani ningekuwa pamoja nanyi sasa, pengine ningebadilisha msemo wangu. Kwa maana nata tanishwa na hali yenu.
21 Niambieni, ninyi mnaotaka kutawaliwa na sheria, je, hamu elewi sheria inavyosema? 22 Kwa maana imeandikwa katika Maandi ko kwamba Abrahamu alikuwa na watoto wawili: mtoto mmoja alizal iwa na mwanamke mtumwa, na wa pili alizaliwa na mwanamke huru. 23 Lakini, mtoto wa mwanamke mtumwa alizaliwa kwa mapenzi ya mwili na yule wa mwanamke huru alizaliwa kutokana na ahadi ya Mungu. 24 Mambo haya yanaweza kueleweka kama mfano. Kwa maana hao mama wawili ni mfano wa maagano mawili: agano la kwanza, ni lile lililofanyika katika mlima wa Sinai, wakazaliwa watoto wa utumwa; huyo ni Hajiri. 25 Hajiri sasa anawakilisha mlima Sinai ulioko Arabuni, na ni mfano wa Yerusalemu ya sasa ambayo iko utumwani pamoja na watoto wake. 26 Lakini Yerusalemu ya mbinguni ni huru, nayo ndio mama yetu. 27 Kwa maana imeandikwa: “Furahi wewe uliyetasa usiyeweza kuzaa; piga kelele, ulie kwa furaha wewe usiyepatwa na maumivu ya uzazi; kwa maana watoto wa yule ali yeachwa ni wengi kuliko watoto wa yule aliye na mume.”
28 Sasa ndugu zangu, sisi kama Isaki, tu watoto wa ahadi. 29 Lakini, kama vile siku zile yule aliyezaliwa kwa mwili alivy omtesa yule aliyezaliwa kwa Roho, ndivyo ilivyo hata sasa. 30 Lakini Maandiko yanasemaje? “Mfukuze mwanamke mtumwa pamoja na mwanae; kwa sababu mtoto wa mtumwa hawezi kurithi pamoja na mtoto wa mwanamke huru.” 31 Kwa hiyo ndugu zangu, sisi si watoto wa mtumwa bali wa mwanamke huru. Uhuru Ndani Ya Kristo