Wagalatia 5

1Kristo alituweka sisi huru ili tuwe na uhuru. Kwa hiyo simameni imara wala msikubali tena kulemewa na minyororo ya utumwa. 2Sikilizeni! Mimi Paulo nawaambieni kwamba kama mkiku bali kutahiriwa, basi Kristo hatawafaidia cho chote. 3Tena, napenda kumshuhudia kila mmoja wenu anayekubali kutahiriwa kwamba inampasa kushika sheria zote. 4Ninyi mnaotafuta kuhesabiwa haki kwa njia ya sheria fahamuni kwamba mmetengwa na Kristo, mko mbali na neema ya Mungu. 5Kwa maana, kwa msaada wa Roho wa Mungu, sisi tunangojea kwa matumaini kupata haki kwa njia ya imani. 6Kwa maana tukiwa ndani ya Kristo, kutahiriwa au kutotahiriwa hakuleti faida yo yote, bali jambo la msingi ni kuwa na imani inayofanya kazi kwa upendo.

7Mlikuwa mkienenda vizuri, sasa ni nani aliyewazuia msiitii kweli? 8Kushawishiwa huku hakutokani na yule anayewaita. 9Hamira kidogo sana inaweza kuchachusha donge zima. 10Nina hakika katika Bwana kwamba mtakubaliana na msimamo wangu. Huyo anayewasumbueni atapata hukumu anayostahili hata akiwa nani. 11Lakini ndugu zangu, kama mimi ninahubiri kwamba kutahiriwa ni lazima, kwa nini bado nateswa? Ingekuwa hivyo, mahubiri yangu juu ya msalaba wa Kristo yasingekuwa kikwazo tena. 12Laiti hao wanaowavurugeni wangejikatakata wenyewe!

13Ndugu zangu, ninyi mliitwa ili muwe watu huru. Hata hivyo msitumie uhuru wenu kuendelea kufuata tamaa za mwili, bali tumi kianeni ninyi kwa ninyi kwa upendo. 14Kwa maana sheria yote hukamilika katika amri moja: “Mpende jirani yako kama nafsi yako.” 15Lakini ikiwa mtaumana na kutafunana, basi jihadhar ini, msije mkaangamizana wenyewe kwa wenyewe.

Maisha Ya Kiroho

16Kwa hiyo nasema, mruhusuni Roho atawale maisha yenu na msitafute kutimiza tamaa za mwili. 17Kwa maana tamaa za mwili hushindana na Roho; na Roho hushindana na tamaa za mwili. Roho na mwili hupingana, na kwa sababu hiyo ninyi hamwezi kufanya yale mnayotaka. 18Lakini kama mkiongozwa na Roho, hamko tena chini ya sheria.

19Basi matendo ya mwili ni dhahiri nayo ni haya: uasherati, uchafu, ufisadi, 20kuabudu sanamu, uchawi, uadui, ugomvi, wivu, hasira, fitina, mafarakano, uzushi, 21husuda, ulevi, ulafi na mambo mengine yanayofanana na hayo. Nawaonya, kama nilivyokwisha waonya kabla, kwamba watu watendao mambo kama haya, hawataurithi Ufalme wa Mungu. 22Lakini tunda la Roho ni upendo, furaha, amani, uvumili vu, wema, fadhili, uaminifu, 23upole, kiasi. Hakuna sheria inayopinga mambo kama haya.

24Wote walio wa Kristo Yesu wameusulubisha mwili pamoja na tamaa zake. 25Kwa kuwa tunaishi kwa kuongozwa na Roho wa Mungu, basi tufuate uongozi wake. 26Tusiwe watu wenye maji vuno, tusichokozane na wala tusioneane wivu. Kuchukuliana Mizigo