Paulo Akubaliwa Na Mitume
1Kisha, baada ya miaka kumi na minne, nilikwenda tena Yeru salemu pamoja na Barnaba, nikamchukua na Tito ili awe pamoja nami. 2 Nilikwenda kwa sababu nilikuwa nimefunuliwa na Mungu, kwamba nikawaeleze kwa faragha wale waliokuwa viongozi, Injili ninayohubiri kwa watu wa mataifa mengine. Nilifanya hivyo ili kazi yangu niliyokwisha fanya na hii ninayofanya sasa isije ikawa bure. 3 Hata hivyo Tito ambaye alikuwa ni Mgiriki, hakulazimika kutahiriwa. 4 Lakini walikuwepo ndugu wengine wa uongo ambao walikuja kwa siri kupeleleza uhuru tulio nao katika Kristo Yesu, ili waturudishe kwenye utumwa wa sheria. 5 Sisi hatukukubaliana nao hata kidogo ili ukweli wa Injili uendelee kutunzwa kwa ajili yenu. 6 Lakini wale ambao walionekana kuwa viongozi wao, mimi sijui wala sijali kama walikuwa na vyeo gani, kwa sababu Mungu haangalii cheo cha mtu; nasema kwamba hao watu hawakuongezea cho chote katika ujumbe wangu. 7 Badala yake walitambua kwamba Mungu alikuwa amenipa kazi ya kuhubiri Injili kwa watu wa mataifa mengi ne kama vile Petro naye alivyotumwa kuhubiri Injili kwa Wayahudi. 8 Kwa maana ilikuwa dhahiri kwamba Mungu aliyemwezesha Petro kuwa mtume kwa Wayahudi ndiye aliyekuwa akifanya kazi katika huduma yangu kama mtume kwa watu wa mataifa mengine. 9 Basi, Yakobo, Kefa na Yohana, ambao walikuwa nguzo za kanisa, walipotambua kwamba Mungu alikuwa amenijalia neema yake, walitushika mikono, mimi na Barnaba, kama ishara ya ushirikiano wetu. Walikubaliana kwamba sisi twende kwa watu wa mataifa mengine na wao waende kwa Wayahudi. 10 Walichotuomba ni kwamba katika huduma yetu tuende lee kuwasaidia maskini; jambo ambalo nimekuwa nikijitahidi kufa nya.
Paulo Anampinga Petro
11 Lakini Petro alipofika Antiokia, mimi nilimpinga hadhar ani kwa kuwa alikuwa amekosea. 12 Kwa sababu kabla ya watu kadhaa waliotoka kwa Yakobo hawajafika, alikuwa akila pamoja na watu wa mataifa mengine. Lakini baada ya hao watu kufika ali ji tenga, akaacha kula pamoja na watu wa mataifa mengine, kwa kuwaogopa wale wa kundi la tohara. 13 Pia Wayahudi wengine wal iungana naye katika unafiki huu, hata Barnaba naye akashawishika kuwaunga mkono.
14 Nilipoona kwamba msimamo wao kuhusu ukweli wa Injili hau kuwa wazi, nilimwambia Petro mbele za watu wote, “Ikiwa wewe uliye Myahudi unaishi kama watu wa mataifa, na huishi kama Myahudi, unawezaje kuwalazimisha watu wa mataifa mengine waishi kama Wayahudi?” Habari Njema Aliyohubiri Paulo
15 Sisi tulio Wayahudi wa kuzaliwa na sio watu wa mataifa ‘wenye dhambi,’ 16 tunafahamu kwamba mtu hawezi kuhesabiwa haki kwa kutii sheria bali kwa kumwamini Yesu Kristo. Kwa hiyo sisi pia tumemwamini Yesu Kristo ili tupate kuhesabiwa haki kwa kumwa mini Kristo, na wala si kwa kuitii sheria. Maana hakuna mtu ata kayehesabiwa haki kwa kutii sheria. 17 Lakini ikiwa sisi katika jitihada ya kuhesabiwa haki katika Kristo, bado tunaonekana tun gali wenye dhambi, je, hii ina maana kwamba Kristo amekuwa mwene zaji wa dhambi? La hasha! 18 Lakini ikiwa mimi nina jenga tena kile ambacho nimekwisha bomoa, basi ninadhihirisha kwamba mimi ni mvunja sheria. 19 Kwa maana mimi kwa njia ya sheria, nimeifia sheria, ili nipate kuishi kwa ajili ya Mungu. 20 Nimesulubiwa pamoja na Kristo; si mimi tena ninayeishi bali ni Kristo anayeishi ndani yangu. Maisha ninayoishi sasa naishi kwa kumwa mini Mwana wa Mungu, aliyenipenda hata akatoa maisha yake kwa ajili yangu. 21 Siwezi nikadharau neema ya Mungu; kwa maana kama haki ingeweza kupatikana kwa kutimiza sheria, basi Kristo alikufa bure.