Kuhesabiwa Haki Kwa Njia Ya Imani
1Ninyi Wagalatia wajinga! Nani aliyewaloga? Yesu Kristo alielezwa wazi wazi mbele yenu kwamba alisulubiwa. 2Nataka mni jibu swali moja: je, mlipokea Roho wa Mungu kwa kutimiza sheria au kwa kuamini mliyosikia? 3Je, ninyi ni wajinga kiasi hiki? Baada ya kuanza na Roho wa Mungu, sasa mnataka kuwa wakamilifu kwa uwezo wenu wenyewe? 4Je, mateso yote yaliyowapata hayakuwa faa kitu? Kweli yalikuwa bure? 5Je, Mungu anawapa Roho wake na kufanya miujiza kati yenu kwa sababu mnatii sheria au kwa sababu mnaamini Injili mliyosikia?
6Tazameni mfano wa Abrahamu: “Yeye alimwamini Mungu, na Mungu alimhesabu kuwa mtu mwenye haki.” 7Kwa hiyo mnaona kwamba watu wanaomwamini Mungu ndio watoto halisi wa Abrahamu. 8Na Maandiko yalitabiri mambo ya baadaye, kwamba Mungu angewahesabia haki watu wa mataifa mengine kwa njia ya imani. Kwa hiyo Maandiko yalitangulia kumtangazia Abrahamu kwa kutamka, “Kwa ajili yako mataifa yote yatabarikiwa.” 9Hivyo basi, walio na imani wana barikiwa pamoja na Abrahamu, ambaye alikuwa mtu wa imani.
Sheria Na Laana
10Wote wanaotegemea kutimiza sheria, wako chini ya laana. Kwa sababu Maandiko yanasema, “Mtu ye yote asiyeshika na kufu ata mambo yote yaliyoandikwa katika kitabu cha sheria, amelaani wa.” 11Ni wazi kwamba hakuna mtu anayehesabiwa haki mbele za Mungu kwa kutimiza sheria, kwa maana, “Mwenye haki ataishi kwa imani.” 12Lakini sheria haitegemei imani kwa maana, “Atimizaye maagizo ya sheria ataishi kwa sheria.” 13Kristo alitukomboa kutoka katika laana ya sheria kwa kuchukua laana hiyo kwa ajili yetu, kwa maana imeandikwa, “Mtu anayetundikwa msalabani amelaaniwa.” 14Lakini alitukomboa ili baraka aliyo pewa Abrahamu iwafikie na watu wa mataifa mengine kwa njia ya Yesu Kristo. Na kwa kutegemea imani, sisi tupate kupokea Roho wa
Sheria Na Ahadi
15Ndugu zangu, napenda nitoe mfano kutoka katika maisha ya kila siku. Hakuna mtu anayetengua wasia wa mtu au kuuongezea ukishatiwa sahihi. 16Abrahamu alipewa ahadi yeye pamoja na mzawa wake. Lakini Maandiko hayasemi, “Na wazao wake,” Kwa maana ya wengi, bali yanasema, “Na mzawa wake,” yaani mmoja, ambaye ndiye Kristo. 17Ninachotaka kusema ni kwamba, sheria, ambayo ilitolewa miaka mia nne na thelathini baadaye, haiwezi kutangua agano lililothibitishwa na Mungu na kulifanya duni. 18Kwa maana, kama urithi wetu unategemea sheria, basi hauwezi tena kutegemea ahadi ya Mungu. Lakini Mungu kwa neema yake alimpa Abrahamu urithi kwa njia ya ahadi. 19Kwa nini basi ipo sheria? Sheria iliwekwa kwa ajili ya uhalifu hadi atakapokuja yule wa uzao wa Abrahamu, ambaye ali tajwa katika ahadi hiyo. Sheria ililetwa na malaika kwa mkono wa mjumbe. 20Lakini mjumbe huwakilisha zaidi ya mtu mmoja; bali
Lengo La Sheria
21Je, sheria inapingana na ahadi za Mungu? La, sivyo! Kama ingetolewa sheria ambayo ingeweza kuwapa watu uzima, basi haki mbele za Mungu ingepatikana kwa kutimiza sheria. 22Lakini Maan diko yanasema kwamba ulimwengu wote upo chini ya utawala wa dhambi, kwa sababu hiyo, ile ahadi inatolewa tu kwa njia ya imani katika Yesu Kristo na wanaoipokea ni wale wenye imani.
23Kabla imani haijakuwepo tulikuwa tumefungwa chini ya sheria, mpaka imani ifunuliwe. 24Kwa hiyo, sheria ilikuwa kama kiongozi wa kutufikisha kwa Kristo, ili tuhesabiwe haki kwa imani. 25Lakini sasa kwa kuwa imani imekuja hatusimamiwi tena na sheria. 26Ninyi nyote mmekuwa wana wa Mungu kwa kumwamini Kristo. 27Kwa maana nyote mliobatizwa katika Kristo, mmemvaa Kristo. 28Hakuna tena tofauti kati ya Myahudi na Mgiriki, mtumwa na mtu huru, mwanaume na mwanamke. Wote mmekuwa kitu kimoja kwa kuungana na Kristo Yesu. 29Ikiwa ninyi ni wa Kristo, basi ni wa uzao wa Ibrahimu na ni warithi wa ahadi aliyopewa na