Kuhusu Ndoa
1Na sasa kuhusu mambo mliyoniandikia. Ni vizuri mtu asioe. 2Lakini kwa kuwa dhambi ya zinaa imeenea, kila mwanamume awe na mke wake mwenyewe, na kila mwanamke awe na mume wake mwenyewe.
3Mume atimize wajibu wake wa ndoa kwa mkewe; na hali kadhal ika mke kwa mumewe. 4Kwa maana mke hatawali mwili wake mwe nyewe, bali mume wake ndiye autawalaye. Vivyo hivyo, mume hata wali mwili wake mwenyewe, bali mkewe ndiye anayeutawala. 5Msiny imane, isipokuwa kama mmekubaliana kufanya hivyo kwa muda mfupi ili muwe na nafasi nzuri ya maombi. Lakini baada ya muda huo rudianeni tena shetani asije akapata nafasi ya kuwajaribu kwa sababu ya kushindwa kujizuia. 6Nasema haya kama ushauri, na si sheria. 7Ningalipenda wote wawe kama mimi nilivyo. Lakini kila mtu amepewa karama yake kutoka kwa Mungu, mmoja ana karama hii na mwingine ana karama ile.
8Na sasa nasema kwa wale wasioolewa na kwa wajane. Ingekuwa vizuri kama wangeendelea kuishi bila kuoa au kuolewa kama mimi. 9Lakini kama hawawezi kujizuia, basi waoe. Ni afadhali kuoa kuliko kuwaka kwa tamaa.
10Kwa wale waliooana ninayo amri, si amri yangu ila ni ya Bwana. Mke asimwache mumewe. 11Lakini kama akimwacha, ni lazima akae bila kuolewa, ama sivyo apatane tena na mumewe. Na mume asimpe mkewe talaka.
12Lakini kwa wengine nasema, si Bwana ila ni mimi: kama ndugu ana mke asiyeamini, na huyo mke amekubali kuishi pamoja naye, basi asimpe talaka. 13Na kama mwanamke mwamini ameolewa na mwanaume asiyeamini, na huyo mwanaume amekubali kuishi naye, basi huyo mwanamke asimpe talaka. 14Kwa maana huyo mwanaume asiyeamini anatakaswa kwa ajili ya mkewe naye mwanamke asiyeamini anatakaswa kwa ajili ya mumewe anayeamini. Kama isingalikuwa hivyo watoto wao wangalikuwa si safi, lakini ilivyo sasa wao ni watakatifu. 15Lakini kama yule asiyeamini akitaka kuachana na mwenzake anayeamini, basi na iwe hivyo. Katika hali hiyo mke au mume ambaye ni mwamini hafungwi. Kwa sababu Mungu ametuita tuishi kwa amani. 16Wewe mke, unajuaje kama hutamwokoa mumeo? Wewe mume unajuaje kama hutamwokoa mkeo?
Kuishi Kama Mlivyoitwa
17Kila mtu aishi maisha aliyopangiwa na Bwana, na ambayo ameitiwa na Mungu. Hii ndio amri ninayotoa kwa makanisa yote.
18Kama mtu alikuwa ametahiriwa alipoitwa, basi asijaribu kuondoa alama za kutahiriwa kwake. Na kama mtu alikuwa hajatahi riwa alipoitwa, basi, asitafute kutahiriwa. 19Kwa kuwa kutahi riwa au kutotahiriwa si kitu. Jambo lililo muhimu ni kutii amri za Mungu . 20Kila mtu abaki katika nafasi ambayo alikuwa nayo alipoitwa kuamini. 21Je, wewe ulipoitwa ulikuwa mtumwa? Jambo hilo lisikusumbue. Lakini kama unaweza kuwa huru, utumie nafasi hiyo. 22Kwa maana aliyeitwa kwa Bwana akiwa mtumwa ni mtu huru wa Bwana. Hali kadhalika mtu aliyekuwa huru alipoitwa ni mtumwa wa Kristo. 23Mmenunuliwa kwa gharama; msikubali kuwa watumwa wa watu. 24Kwa hiyo ndugu zangu, kila mmoja wenu akae na Mungu katika nafasi aliyokuwa nayo alipoitwa.
Kwa Hali Ya Sasa, Afadhali Kutokuoa
25Sasa, kuhusu wale walio bikira. Sina amri yo yote kutoka kwa Bwana, lakini mimi natoa ushauri kama mtu aliyemwaminifu kwa rehema ya Bwana.
26Kwa sababu ya dhiki iliyopo, nadhani itakuwa vyema mki baki kama mlivyo. 27Je, umeoa? Basi usitake talaka. Kama hujaoa usitafute mke. 28Lakini kama ukioa, hujatenda dhambi; na kama bikira akiolewa hajatenda dhambi. Lakini wanaooa watakabil iana na matatizo mengi katika maisha haya, nami ningependa myaep uke kwa kubaki mlivyo.
29Nikisema hivyo ndugu zangu, nina maana kwamba muda uliobaki ni mfupi. Tangu sasa waliooa waishi kama hawakuoa; 30na wana oomboleza kama hawaoombolezi; wenye furaha kama hawana furaha; wanaonunua kama walivyonunua si mali yao; 31na wanaoshughulika na vitu vya dunia hii, kama hawahusiki navyo. Kwa maana dunia hii kama tunavyoiona sasa inatoweka.
32Ningependa msiwe na wasiwasi. Mwanamume ambaye hajaoa anajishughulisha na mambo ya Bwana, jinsi ya kumpendeza. 33Lakini mwanamume aliyeoa anajishughulisha na mambo ya dunia hii, jinsi ya kumfurahisha mke wake. 34Kwa sababu hiyo, ana vutwa huku na huko. Mwanamke asiyeolewa au msichana bikira anaj ishughulisha na kazi ya Bwana, jinsi ya kuwa mtakatifu kimwili na kiroho. Lakini mwanamke aliyeolewa anajishughulisha na mambo ya dunia, jinsi ya kumfurahisha mume wake. 35Ninasema haya kwa faida yenu na sio kuwawekea vikwazo. Napenda muishi sawa na kumpa Bwana maisha yenu yote. 36Kama mtu anafikiri kwamba mwenendo wake kwa mchumba wake si sawa, na hasa kama mchumba wake anaanza kuzeeka, na anaona anawajibika kumuoa, basi afanye anavyoona vyema; waoane, si dhambi. 37Lakini kama mwanamume ameshaamua moyoni mwake kuto kuoa bila kulazimishwa na mtu; kama anaweza kujitawala kabisa, basi anafanya vyema kutokumuoa mchumba wake. 38Kwa hiyo mwana mume anayeamua kumuoa mchumba wake anafanya vizuri, lakini yule anayeamua kutokumuoa anafanya vizuri zaidi.
39Mwanamke aliyeolewa amefungwa kwa mume wake maadamu anaishi. Kama mumewe akifa, basi mwanamke huyo yuko huru kuolewa na mume mwingine ampendaye, ila iwe katika Bwana. 40Lakini kwa upande wangu naona kuwa angekuwa na furaha zaidi akibaki alivyo.