Mitume Wa Kristo
1Basi, mtuhesabu sisi kuwa watumishi wa Kristo na mawakili wa siri za Mungu. 2Zaidi ya hayo, mawakili wanatakiwa wawe waaminifu. 3Mimi sijali kama ninyi mkinihukumu au nikihukumiwa na mahakama ya wanadamu; kwa kweli hata mimi mwenyewe sijihukumu 4Dhamiri yangu hainishitaki; lakini hilo halinifanyi nisiwe na hatia. Bwana ndiye anayenihukumu. 5Kwa hiyo msitoe hukumu kabla ya wakati wake, kabla Bwana hajaja. Yeye atafichua mambo yaliyof ichwa gizani na kwa kuweka wazi nia za mioyo ya watu. Ndipo kila mtu atapokea sifa anayostahili kutoka kwa Mungu.
6Basi ndugu zangu nimetumia mfano wa Apolo na mimi kwa faida yenu ili muweze kujifunza kutoka kwetu maana ya usemi, “Usivuke mpaka wa yale yaliyoandikwa.” Na hivyo hamtajivunia mtu fulani na kumdharau mwingine. 7Ni nani aliyewafanya kuwa tofauti na watu wengine wote? Mna kitu gani ambacho hamkupokea? Basi ikiwa mmepokea, mbona mnajivuna kana kwamba hayo mliyonayo si zawadi?
8Mmekwisha pata kila kitu mnachohitaji! Mmekuwa matajiri! Mmekuwa wafalme pasipo msaada wetu! Lakini laiti kama mngekuwa wafalme kweli ili na sisi tuwe wafalme pamoja nanyi! 9Kwa sababu inaonekana kwamba Mungu ametuweka sisi mitume katika nafasi ya mwisho kabisa katika msafara wa maonyesho kama watu waliohukumiwa kufa hadharani, kwa sababu tumekuwa maonyesho kwa ulimwengu wote, kwa malaika na kwa wanadamu pia.
10Kwa ajili ya Kristo sisi ni wajinga, lakini ninyi mna hekima ndani ya Kristo. Sisi ni dhaifu, lakini ninyi mna nguvu. Tunadharauliwa, lakini ninyi mnaheshimiwa. 11Mpaka wakati huu tuna njaa na kiu, tumevaa matambara, tumeteswa, hatuna makao. 12Tunafanya kazi ngumu kwa mikono yetu. Tunapolaaniwa, tunabar iki; tunapoteswa tunavumilia. 13Tunaposingiziwa tunajibu kwa maneno ya upole. Tumekuwa kama takataka ya dunia hii, na uchafu wa ulimwengu mpaka leo hii.
14Nawaandikia mambo haya, si kwa sababu nataka muone aibu, bali nataka niwaonye kama wanangu wapendwa. 15Ingawa mnao viongozi wasiohesabika katika Kristo, lakini hamna baba wengi. Mimi nilikuwa baba yenu katika Kristo Yesu kwa kuwaletea Injili. 16Basi nawasihi mfuate mfano wangu. 17Kwa sababu hii ninam tuma Timotheo, mwanangu mpendwa na mwaminifu katika Bwana. Yeye atawakumbusha kuhusu maisha yangu katika Kristo ambayo yanakubal iana na mafundisho yangu katika kila kanisa ninalotembelea.
18Baadhi yenu mmekuwa na kiburi mkidhani kuwa sitafika kwenu. 19Lakini kama Bwana akipenda, nitafika kwenu mapema, nami nitapenda kujua, zaidi ya maneno yao hawa watu wenye kiburi wana uwezo gani? 20Kwa kuwa Ufalme wa Mungu si maneno matupu bali ni nguvu. 21Ninyi amueni. Nije kwenu na fimbo kuwaadhibu, au nije na upendo kwa roho ya upole?