1 Timotheo 3

Viongozi Katika Kanisa

1Neno hili ni kweli, kwamba mtu akitaka kuwa askofu, anata mani kazi njema. Basi, askofu awe mtu asiye na lawama. Awe mume wa mke mmoja, mwenye kiasi na busara, mtaratibu, mkarimu na aju aye kufundisha. Asiwe mlevi, wala mgomvi bali awe mpole; asiwe mbishi wala mtu apendaye fedha. Aweze kuisimamia nyumba yake vizuri akiwafanya watoto wake kuwa wanyenyekevu na wenye heshima katika hali zote. Kwa maana kama mtu hawezi kuitawala nyumba yake mwenyewe atawezaje kuliangalia kanisa la Mungu? Asiwe mtu aliyeongoka karibuni asije akajiona na kuhukumiwa kama shetani alivyohukumiwa. Kadhalika, awe mwenye sifa njema kati ya watu wa nje ya kanisa, asije akalaumiwa na kuanguka katika mtego wa shetani.

Wasaidizi Katika Kanisa

Vivyo hivyo mashemasi wawe wenye kuheshimika, si wenye kauli mbili au wanywaji mno wa divai au wenye tamaa ya fedha. Wanapaswa kuizingatia ile siri ya imani kwa dhamiri safi. 10 Ni lazima wapimwe kwanza na wakionekana kuwa wanafaa basi waruhusiwe kutoa huduma ya ushemasi. 11 Hali kadhalika, wake zao wawe wenye kuheshimika, si wasengenyaji bali wenye kiasi na waaminifu katika mambo yote. 12 Shemasi awe mume wa mke mmoja; na aweze kuwatawala watoto wake na jamaa yake vema. 13 Watu wanaotoa huduma njema ya ushemasi hujipatia heshima kubwa na uha kika mkubwa katika imani yao kwa Kristo Yesu.

14 Ninakuandikia mambo haya sasa ingawa natarajia kuwepo pamoja nawe karibuni, 15 ili kama nikicheleweshwa, upate kujua jinsi watu wanavyopaswa kuenenda katika nyumba ya Mungu, ambayo ni kanisa la Mungu aliye hai, nguzo na msingi wa kweli. 16 Bila shaka yo yote, siri ya dini yetu ni kuu: Alidhihirishwa katika mwili wa kibinadamu, alithibitishwa katika Roho, alionwa na mal aika, alihubiriwa kati ya mataifa, akaaminiwa ulimwenguni, aka chukuliwa juu katika utukufu.