Jinyenyekezeni Kwa Mungu
1Ni kitu gani kinachosababisha vita na ugomvi miongoni mwenu? Je, si tamaa zenu zinazopingana ndani yenu? 2 Mnatamani lakini hampati kwa hiyo mnaua . Na mnatamani kupata lakini ham pati vile mnavyotaka kwa hiyo mnapigana na kuanzisha vita. Mme pungukiwa kwa sababu hamumwombi Mungu. 3 Mnaomba lakini hampokei kwa sababu mnaomba kwa nia mbaya, ili mtumie mtakavyopata kwa kutosheleza tamaa zenu.
4 Ninyi viumbe wasio waaminifu! Hamfahamu kwamba urafiki na dunia ni uadui na Mungu? Kwa hiyo anayependa kuwa rafiki wa dunia anajitangaza kuwa adui wa Mungu. 5 Au mnadhani Maandiko mataka tifu yanasema bure kuwa, “Anaona wivu juu ya roho aliyemweka aishi ndani yetu”? 6 Lakini yeye anatupatia neema zaidi, ndio maana Maandiko husema, “Mungu huwapinga wenye kiburi lakini huwapa neema wanyenyekevu.”
7 Kwa hiyo, jinyenyekezeni kwa Mungu . Mpingeni shetani, naye atawakimbia. 8 Mkaribieni Mungu, naye atawakaribia. Takaseni mikono yenu, ninyi wenye dhambi; na takaseni mioyo yenu, ninyi wenye nia mbili. 9 Huzunikeni, ombolezeni na kulia. Kicheko chenu kiwe kilio na furaha yenu iwe huzuni. 10 Jinyenyekezeni mbele za
Kuhusu Kuhukumiana
11 Ndugu, msilaumiane ninyi kwa ninyi. Mtu anayesema maovu kumhusu ndugu yake au kumhukumu ndugu yake anailaumu sheria na kuihukumu. Unapoihukumu sheria, basi hutii sheria bali umekuwa hakimu wa sheria. 12 Ni Mungu peke yake ambaye ametoa sheria na pia yeye ndiye hakimu; ni yeye tu awezaye kuokoa na kuangamiza.
Usijivunie ya Kesho
13 Sasa nisikilizeni ninyi msemao, “Leo au kesho tutakwenda katika mji huu ama ule tukae mwaka mmoja huko, tufanye biashara na kuchuma fedha.” 14 Kumbe hamjui litakalotokea kesho! Kwani maisha yenu ni kitu gani? Ninyi ni kama ukungu ambao huonekana kwa muda mfupi tu na baadaye hutoweka. 15 Badala yake mnapaswa kusema, “Bwana akipenda, tutaishi na kufanya hili ama lile.” 16 Lakini sasa mnajisifu kwa sababu ya ujinga wenu. Kujisifu kwa jinsi hiyo ni uovu.
17 Mtu ye yote anayefahamu lililo jema kutenda, lakini asilitende, basi mtu huyo anatenda dhambi.