Onyo Kwa Matajiri
1Sasa sikilizeni, ninyi matajiri: Lieni na kuomboleza kwa ajili ya huzuni inayowajia. 2Utajiri wenu umeoza na mavazi yenu yameliwa na nondo. 3Dhahabu yenu na fedha yenu vimeingia kutu na kutu yake itakuwa ushahidi dhidi yenu na itakula miili yenu kama moto. Mmejilimbikizia utajiri kwa siku za mwisho. 4Angalieni ule ujira mliowadhulumu vibarua waliovuna mashamba yenu unawalilia; na vilio vya wavunaji hao vimeyafikia masikio ya Bwana wa majeshi. 5Mmeishi duniani maisha ya anasa na kujistarehesha. Mmejinenepesha tayari kwa siku ya kuchinjwa. 6Mmemhukumu na kum wua mwenye haki; yeye hakuwapinga.
Subira Na Mateso
7Kwa hiyo, ndugu zangu, muwe na subira mpaka Bwana atakapo kuja. Angalieni jinsi mkulima anavyongojea ardhi itoe mavuno mazuri, jinsi anavyongojea kwa subira mvua za mwanzo na za mwisho. 8Hali kadhalika nanyi muwe na subira. Muwe na mioyo tha biti kwa sababu kuja kwa Bwana kumekaribia. 9Ndugu zangu, msi nung’unikiane wenyewe kwa wenyewe, ama sivyo mtahukumiwa. Hakimu amesimama mlangoni.
10Ndugu zangu, kama mfano wa subira wakati wa mateso, waan galieni manabii walionena katika jina la Bwana. 11Kama mnavy ojua tunawahesabu kuwa wamebarikiwa wale ambao wamevumilia. Mmek wisha kusikia habari za ustahimilivu wa Ayubu na mmeona shabaha ya Bwana, jinsi Bwana alivyo na huruma na rehema.
12Zaidi ya yote, ndugu zangu, msiape, ama kwa mbingu, au kwa dunia au kwa kiapo kingine cho chote. Bali mkisema ‘Ndio’ iwe ndio, na mkisema ‘Hapana
Maombi Ya Imani
13Je, kuna mtu ye yote miongoni mwenu aliye na shida? Basi na aombe. Je, yuko mwenye furaha? Basi na aimbe nyimbo za sifa. 14Je, kuna mtu miongoni mwenu aliye mgonjwa? Basi awaite wazee wa kanisa wamwombee na kumpaka mafuta katika jina la Bwana. 15Na kule kuomba kwa imani kutamwokoa mgonjwa huyo na Bwana atamwinua. Kama ametenda dhambi, atasamehewa. 16Kwa hiyo ungameni dhambi zenu ninyi kwa ninyi na kuombeana ili mpate kuponywa. Maombi ya mtu mwenye haki yana nguvu na huleta matokeo.
17Eliya alikuwa binadamu kama sisi. Aliomba kwa moyo kwamba mvua isinyeshe na mvua haikunyesha juu ya nchi kwa muda wa miaka mitatu na nusu. 18Kisha akaomba tena na mbingu zikatoa mvua na ardhi ikazaa matunda yake.
19Ndugu zangu, ikiwa mtu miongoni mwenu anapotoka kutoka katika kweli na mtu mwingine akamrejesha,