Maisha Mapya
1Basi, kwa kuwa mmefufuliwa pamoja na Kristo, elekezeni mioyo yenu kwenye mambo ya juu, alikokaa Kristo, upande wa kulia wa Mungu. 2 Yafikirini mambo ya juu na siyo mambo ya hapa duniani. 3 Kwa maana ninyi mlikufa, na uzima wenu umefichwa pamoja na Kristo kwa Mungu. 4 Wakati Kristo ambaye ni uzima wetu ataonekana, ndipo na ninyi mtakapoonekana pamoja naye katika utu kufu.
5 Basi, yaangamizeni kabisa mambo yote yanayotokana na asili yenu ya kidunia: uasherati, mawazo machafu, tamaa mbaya, nia mbaya na choyo ambayo ni ibada ya sanamu. 6 Kwa sababu ya mambo haya, ghadhabu ya Mungu inakuja. 7 Ninyi mlikuwa mkitenda mambo haya katika maisha yenu ya zamani. 8 Lakini sasa ni lazima mwa chane kabisa na mambo kama haya: hasira, ghadhabu, nia mbaya, matukano na maneno machafu kutoka vinywani mwenu. 9 Msiambiane uongo kwa maana mmekwisha vua utu wenu wa zamani pamoja na matendo yake 10 na kuvaa utu upya ambao unaendelea kufanywa upya katika ufahamu ili ufanane na Muumba wake. 11 Katika hali hii hakuna tena tofauti kati ya Mgiriki na Myahudi, aliyetahiriwa na asiyetahiriwa, mtu aliyesoma na asiyesoma, mtumwa na mtu huru. Bali Kristo ni yote na yumo ndani ya wote. 12 Basi, kwa kuwa ninyi ni wateule wa Mungu, wapendwa na watakatifu, vaeni moyo wa huruma, wema, unyenyekevu, upole na uvumilivu. 13 Vumilianeni na kusameheana kama mtu ana malalamiko kuhusu mwenzake. Sameheni kama Bwana alivyokwisha kuwasamehe. 14 Juu ya haya yote, vaeni upendo ambao unaunganisha mambo haya kuwa kitu kimoja kilicho kikamilifu.
15 Ruhusuni amani ya Kristo itawale mioyoni mwenu kwa kuwa ninyi kama viungo vya mwili mmoja mmeitiwa amani. Tena muwe na shukrani. 16 Neno la Kristo lidumu ndani yenu kwa wingi, mki fundisha na na kuonyana katika hekima yote; na huku mkiimba zab uri, nyimbo na tenzi za rohoni na mkiwa na shukrani kwa Mungu mioyoni mwenu. 17 Na lo lote mtakalofanya, ikiwa kwa neno au kwa tendo, fanyeni yote katika jina la Bwana Yesu, mkimshukuru Mungu Baba kupitia kwake.
Wajibu Katika Familia
18 Ninyi wake, watiini waume zenu kama inavyopasa katika Bwana. 19 Ninyi waume, wapendeni wake zenu wala msiwe wakali juu yao. 20 Ninyi watoto, watiini wazazi wenu katika mambo yote, kwa maana hii humpendeza Bwana. 21 Ninyi akina baba msiwachokoze watoto wenu wasije wakakata tamaa.
22 Nanyi watumwa, watiini mabwana wenu wa hapa duniani katika mambo yote; fanyeni hivyo kwa moyo safi mkimwogopa Mungu, na wala si kwa kutafuta upendeleo wakati wanapowatazama. 23 Lo lote mfanyalo, lifanyeni kwa moyo kama watu wanaomtumikia Bwana na siyo wanadamu. 24 Kwa maana mnafahamu kwamba mtapokea urithi wenu kwa Bwana kama tuzo yenu.