1Napenda mjue jinsi ninavyofanya kazi kwa bidii kwa ajili yenu na kwa ajili ya watu wa Mungu walioko Laodikia, na kwa ajili ya wengine wote ambao hawajapata kuniona. 2 Shabaha yangu ni kuwa wafarijiwe moyoni na kuunganishwa katika upendo, ili wapate uta jiri wa ufahamu kamili, wajue siri ya Mungu, yaani Kristo; 3 ambaye kwake hupatikana hazina yote ya hekima na maarifa. 4 Nawaambia haya ili mtu ye yote asije akawadanganya kwa maneno ya kuvutia. 5 Maana ingawa mimi niko mbali nanyi kimwili, lakini niko pamoja nanyi kiroho, nami nafurahi mnaendelea vizuri na kwamba imani yenu katika Kristo ni imara.
Maisha Kamili Katika Kristo
6 Basi, kama mlivyompokea Kristo Yesu kuwa Bwana, endeleeni kuishi ndani yake. 7 Muwe na mizizi ndani yake, na kujengwa juu yake; mkiimarishwa katika imani kama mlivyofundishwa na kububu jika kwa shukrani.
8 Angalieni mtu ye yote asiwateke kwa falsafa duni na potofu ambazo hutegemea mapokeo ya kibinadamu na mafundisho ya kidunia, na wala si Kristo mwenyewe. 9 Maana, ukamilifu wote wa kimungu umo ndani ya Kristo katika umbile lake la kibinadamu. 10 Nanyi mmepewa ukamilifu ndani ya Kristo, ambaye yeye ni mkuu juu ya kila uwezo na kila mamlaka. 11 Katika Kristo mmetahiriwa kwa kuondolewa hali yenu ya asili ya dhambi. Hii si tohara inayofa nywa kwa mikono ya binadamu bali inafanywa na Kristo. 12 Mli zikwa pamoja naye katika ubatizo na kufufuliwa pamoja naye kwa kuamini uweza wa Mungu aliyemfufua kutoka kwa wafu.
13 Mlipokuwa mmekufa kwa sababu ya dhambi zenu na kwa sababu ya kutotahiriwa kwa hali yenu ya asili ya dhambi, Mungu aliwafa nya hai pamoja na Kristo. Alitusamehe dhambi zetu zote, 14 baada ya kufuta kabisa hati ya mashtaka iliyokuwa inatukabili na kutu pinga pamoja na masharti yake; aliiondoa akaipigilia msalabani. 15 Na baada ya kuvunja nguvu na mamlaka ya shetani, Mungu alim fedhehesha hadharani kwa kuonyesha ushindi wa msalaba juu yake.
16 Kwa hiyo msimruhusu mtu awahukumu kuhusu chakula au kiny waji, au juu ya kuadhimisha sherehe za dini, sikukuu ya mwezi mpya au siku ya sabato. 17 Maana hizi zilikuwa ni kanuni za muda tu au vivuli vya yale mambo ambayo yangekuja; lakini hakika ya mambo yenyewe ni Kristo. 18 Msikubali kuhukumiwa na mtu ye yote anayejifanya mnyenyekevu na asemaye kwamba ni lazima kuabudu mal aika, mkapoteza tuzo yenu. Mtu kama huyo hufurahia kueleza kwa kirefu maono aliyoona na mawazo yake yasiyo ya kiroho humfanya awe na kiburi. 19 Mtu kama huyo amepoteza uhusiano na Kristo ambaye ni kichwa ambacho kimeunganika na mwili wote na kushika manishwa pamoja kwa mishipa yake na kukua kama Mungu apendavyo.
Kufa Na Kuishi Pamoja Na Kristo
20 Ikiwa mmekufa pamoja na Kristo na hamtawaliwi tena na kanuni za dunia hii, kwa nini bado mnaishi kana kwamba bado mna tawaliwa na masharti ya kidunia? 21 “Usishike hiki! Usionje hiki! Usiguse hiki!” 22 Masharti haya yote hayana budi kuteke tea kwa sababu yanatokana na sheria na mafundisho ya binadamu. 23 Masharti yenyewe yanaonekana kuwa ni ya hekima, maana yana jiwekea namna zake za ibada, unyenyekevu bandia na kuuadhibu mwili. Lakini hayana uwezo wo wote kuzuia tamaa za mwili.