1Kutoka kwa Paulo, mtume wa Kristo Yesu na Timotheo ndugu yetu. 2 Kwa ndugu katika Kristo, watakatifu na waaminifu waishio Kolosai. Tunawatakieni neema na amani kutoka kwa Mungu Baba yetu.
Shukrani Na Maombi
3 Siku zote tunamshukuru Mungu, Baba wa Bwana wetu Yesu Kristo, tunapowaombea. 4 Kwa maana tumepata habari juu ya imani yenu katika Kristo Yesu na upendo wenu kwa watu wote wa Mungu. 5 Imani hii na upendo umetokana na tumaini mlilowekewa mbinguni na ambalo mmelisikia katika neno la kweli, yaani Habari Njema. 6 Duniani kote, hii Habari Njema iliyowajia inaenea na kuzaa mat unda kama ilivyokuwa kwenu mlipoisikia na kuelewa neema ya Mungu kwa kina.
7 Mlijifunza juu ya Habari Njema kutoka kwa mtumishi mwenzenu mpendwa, Epafra. Yeye ni mhudumu mwaminifu wa Kristo ambaye ana fanya kazi kwa niaba yetu, 8 naye ametufahamisha juu ya upendo wenu mliopewa na Roho.
9 Kwa sababu hii, tangu tuliposikia habari zenu, hatujaacha kuwaombea. Tunamsihi Mungu awape kwa wingi, maarifa ya kujua mapenzi yake, kwa njia ya hekima ya kiroho na ufahamu. 10 Ili mpate kuishi maisha yanayomtukuza Bwana na kumpendeza kabisa: mkizaa matunda kwa kila kazi njema na kukua katika kumjua Mungu. 11 Tunawaombea pia muimarishwe na nguvu zote kwa kadiri ya nguvu ya utukufu wake; mpate kuwa na subira na uvumilivu, huku 12 mkimshukuru kwa furaha Baba aliyewafanya mustahili kuwa na fungu katika urithi wa watakatifu, katika ufalme wa nuru. 13 Kwa maana ametuokoa kutoka katika nguvu za giza, akatuweka katika ufalme wa Mwanae mpendwa, 14 ambaye ametukomboa kwa damu yake, tukapata msamaha wa dhambi.
Ukuu Wa Kristo
15 Kristo anafanana kabisa na Mungu asiyeonekana. Yeye ali kuwepo kabla Mungu hajaumba kitu cho chote. 16 Yeye ndiye ali yeumba vitu vyote mbinguni na duniani; vitu vinavyoonekana na visivyoonekana; kama ni viti vya enzi au nguvu, au watawala au milki na mamlaka: vyote viliumbwa na yeye kwa ajili yake. 17 Yeye alikuwapo kabla ya vitu vingine vyote na kwa uwezo wake vitu vyote vinahusiana kwa mpango. 18 Yeye ni kichwa cha mwili, yaani kanisa lake; naye ni wa kwanza na mzaliwa wa kwanza wa wale wote wanaofufuka kutoka kwa wafu, ili yeye peke yake awe mkuu katika vitu vyote. 19 Kwa kuwa ilimpendeza Mungu kwamba ukamil ifu wake wote wa kimungu uwe ndani ya Mwanae; 20 na kwamba kwa njia ya mwanae vitu vyote vilivyoko duniani na vilivyoko mbinguni vipatanishwe na Mungu, kwa ajili ya damu yake iliyomwagwa msala bani kuleta amani.
21 Hapo kwanza ninyi mlikuwa mmefarakana na Mungu na mlikuwa maadui zake kwa sababu ya mawazo na matendo yenu maovu. 22 Lakini sasa Mungu amewapatanisha naye kwa njia ya mwili wa Kristo katika kifo, ili awaweke mbele yake mkiwa watakatifu, bila doa wala lawama. 23 Lakini hamna budi kuendelea kuwa imara na thabiti katika imani yenu, pasipo kuyumba katika tumaini lililomo katika Injili. Hii ndio ile Injili mliyoisikia na ambayo imetan gazwa kwa kila kiumbe duniani na ambayo mimi, Paulo, nimekuwa mtumishi wake.
Huduma Ya Paulo Kwa Makanisa
24 Na sasa nafurahi kuteseka kwa ajili yenu na kwa mateso yangu ninakamilisha kile ambacho kimepungua katika mateso ya Kristo kwa ajili ya mwili wake, yaani kanisa lake. 25 Mimi nime kuwa mtumishi wa kanisa kufuatana na wajibu niliopewa na Mungu, kuwasilisha kwenu neno la Mungu kwa ukamilifu. 26 Hii ni siri ambayo ilikuwa imefichika kwa karne nyingi na vizazi vingi viliv yopita, lakini sasa imefunuliwa kwa watu wa Mungu. 27 Kwao, Mungu amependa kudhihirisha kati ya mataifa utukufu wa utajiri wa siri hii, yaani, Kristo ndani yenu ndiye tumaini pekee la utu kufu.
28 Kwa sababu hii tunamtangaza Kristo, tukiwaonya na kuwa fundisha watu wote kwa hekima yote ili tuweze kumleta kila mmoja mbele ya Mungu akiwa amekamilika katika Kristo. 29 Kwa shabaha hii nina fanya kazi, nikijitahidi kwa nguvu kuu ya Kristo inay ofanya kazi kwa uwezo mkuu ndani yangu.