1Kwa hiyo mfuateni Mungu kama watoto wapendwa. 2 Muishi maisha ya upendo kama Kristo alivyotupenda sisi akajitoa kwa ajili yetu kuwa sadaka yenye harufu nzuri na dhabihu kwa Mungu. 3 Lakini uasherati, uchafu wa aina zote na tamaa, wala yasitajwe miongoni mwenu, kwa maana mambo haya hayawastahili watakatifu wa Mungu. 4 Kusiwepo na mazungumzo machafu ya aibu, au maneno ya upuuzi au mzaha; mazungumzo ya namna hii hayafai. Badala yake mshukuruni Mungu. 5 Mjue hakika kwamba hakuna mwasherati wala mtu mwenye mawazo machafu, wala mwenye tamaa, yaani mwabudu sanamu, ambaye ataurithi Ufalme wa Kristo na wa Mungu. 6 Msikubali kudan ganywa na mtu ye yote kwa maneno matupu, kwa kuwa hasira ya Mungu huwaka kwa sababu ya mambo kama haya juu ya watu wote wasiomtii. 7 Kwa hiyo, msishirikiane nao. 8 Zamani ninyi pia mlikuwa gizani, lakini sasa mmekuwa nuru katika Bwana; basi muishi kama watoto wa nuru. 9 Kwa maana tunda la nuru hupatikana katika kila lililo jema, lililo la haki na la kweli. 10 Jifunzeni mambo yanayom pendeza Bwana. 11 Msishiriki matendo ya giza yasiyofa a, bali yafichueni. 12 Kwa maana ni aibu hata kutaja mambo wanayofanya kwa siri. 13 Lakini ikiwa jambo lo lote linawekwa katika nuru, huonekana, kwa maana ni nuru inayofanya vitu vionekane. 14 Ndio sababu husemwa, “Amka wewe uliyelala, ufufuke kutoka kwa wafu, na Kristo atakuangazia.” 15 Kwa hiyo muwe waangalifu jinsi mnavyoishi; msiishi kama watu wasio na hekima, bali kama watu wenye hekima, 16 mkitumia vizuri muda mlio nao, kwa maana hizi ni nyakati za uovu. 17 Kwa hiyo msiwe wajinga, bali muelewe yaliyo mapenzi ya Mungu. 18 Pia msilewe divai, kwa sababu huo ni upotovu, bali mjazwe Roho. 19 Zungumzeni ninyi kwa ninyi kwa zaburi na nyimbo na tenzi za rohoni, mkimwimbia Mungu mioyoni mwenu kwa sauti tamu. 20 Wakati wote na kwa kila kitu mshukuruni Mungu Baba katika jina la Bwana wetu Yesu Kristo. 21 Kila mmoja wenu ajinyenyekeze kwa mwenzake kwa sababu ya upendo mlio nao kwa Kristo. 22 Wake, watiini waume zenu kama mnavyomtii Bwana. 23 Kwa maana mume ni kichwa cha mke kama vile Kristo alivyo kichwa cha kanisa, ambalo ni mwili wake, naye mwe nyewe ni Mwokozi wa kanisa. 24 Basi, kama vile Kanisa linavyom tii Kristo, vivyo hivyo na wake pia wanapaswa kuwatii waume zao kwa kila jambo. 25 Ninyi waume, wapendeni wake zenu, kama Kristo alivyolipenda kanisa akajitoa nafsi yake kwa ajili yake ili 26 alitakase. Alifanya hivyo kwa kuliosha kwa maji na kwa neno lake 27 ili ajipatie kanisa linalong’aa, lisilo na doa wala kunjamano wala kitu kingine cho chote kama hicho; liwe takatifu na bila kasoro. 28 Vivyo hivyo waume wawapende wake zao kama miili yao. Anayempenda mkewe anajipenda mwenyewe. 29 Hakuna mtu anayeuchukia mwili wake mwenyewe, bali huulisha na kuutunza vizuri, kama Kristo anavyolitunza kanisa lake. 30 Sisi tu viungo vya mwili wake. 31 “Kwa sababu hii, mwanaume atamwacha baba yake na mama yake, naye ataungana na mkewe, na hawa wawili wata kuwa mwili mmoja.” 32 Hili ni fumbo gumu kueleweka, nami nasema kuwa ni kielelezo kuhusu Kristo na kanisa. 33 Hata hivyo kila mmoja wenu ampende mkewe kama anavyoipenda nafsi yake; na mke naye ahakikishe anamheshimu mumewe. Watoto Na Wazazi